Hukumu ya Wale Ambao Hawakufikiwa n...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya Wale Ambao Hawakufikiwa na Uislamu

Question

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameniongoza kuingia katika Uislamu, nami nina bibi mmoja ambaye anakaribia kufa, naye ni Mkristo mfuasi wa madhehebu ya Kikatoliki tena hajui chochote kuhusu Uislamu hata hajui kwamba kuna dini ya Mwenyezi Mungu inayoitwa Uislamu kwani aliishi katika kijiji cha mbali mno ambacho ndani yake hakikusikika chochote kuhusu Uislamu. Sasa swali langu ni kama ifuatavyo:
Je, bibi yangu huyu atakuwa ni mmojawapo wa watakaokaa milele motoni kwa sababu ya ukafiri ulio wazi (kuamini utatu) au anaweza kuwa kwa kudra ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ni miongoni mwa watu wa Peponi k.v. Wakristo waliokuwepo kabla ya Kuwafikia Uislamu au kwa ajili ya kutojua kwake Uislamu kabisa k.v. waliokufa baada ya kuishi pahala pa kutoweza kufikiwa na Uislamu (k.v. pahala pa kuishi binadamu wa mwanzo na makabila ya Eskimo?).

Answer

Kwa jina la Mwenyezi Mungu, sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, na rehma na amani zimwendee bwana wetu Mtume wa Mwenyezi Mungu, jamaa zake, masahaba wake na wanaomfuata. Na baada ya hayo:
Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Na haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwahisabu watu kuwa wamepotea baada ya kuwa amewaongoza mpaka awabainishie ya kujiepusha nayo (Wakikataa kujiepusha nayo ndipo wanapohisabika kuwa ni waovu). Hakika Mwenyezi Mungu Anajua kila kitu}[AT TAWBA, 115],
Kadhalika Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Na sisi si wenye kuwaadhibisha (viumbe) mpaka tuwapelekee Mtume (awafahamishe yaliyo ya haki. Basi wakiyakataa ndipo wanapoangamizwa)}[BANI ISRAIL, 15].
Tena Amesema Mtume S.A.W.: “Hakuna yeyote anayependelea zaidi kukubali udhuru kuliko Mwenyezi Mungu, na kwa hiyo Mitume walitumwa” (Hadithi hii ilisimuliwa na Imamu Muslim). Wahakiki miongoni mwa watu wa Sunna walielekea kwamba wale ambao hawakufikiwa na Uislamu kwa uwazi, basi watakuwa na udhuru wao kisha kuna kundi la Maulamaa waliosema kuokoka kwa watu kama hao, na Maulamaa wengine wakasema kuwa Mwenyezi Mungu Atawafanyia mtihani katika siku ya Kiyama, kwa hivyo ni juu yako uzidi kumwombea bibi yako huwenda Mwenyezi Mungu akamrehemu kwa ukarimu na msamaha wake, yeye Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyetakasika.
Ama suala la kuharamisha kuwaombea makafiri, basi ni kwa wale ambao sheria imewasifia kuwa ni watu wa motoni kama Alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Haimpasi Mtume na wale walioamini kuwatakia samahani washirikina ijapokuwa ni jamaa (zao); baada ya kuwabainikia kuwa wao ni watu wa (moto wa Jahanamu}[AT TAWBA, 113].
Ama yule ambaye hukumu ya watu wa muda -wale ambao hawakufikiwa na Uislamu - inamjumlisha yeye kuwa katika kundi hilo, na kwa hiyo basi anakuwa na udhuru wake na inajuzu kumwombea dua kama tulivyosema.
Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi ya wote.

Share this:

Related Fatwas