Jihadi kubwa zaidi na uhusiano wake na kubeba silaha
Question
Je, Jihadi kubwa zaidi ni ipi? Je, kubeba silaha ni kutoka kwenye jihadi kubwa zaidi?
Answer
Hapana shaka kuwa adui mkubwa wa mwanadamu ni nafsi yake mwenyewe, na kupambana nayo ndiyo jihadi kubwa zaidi, kama alivyosema Mtume (S.A.W.), na Mwenyezi Mungu humuongoza amtakaye kwenye njia iliyonyooka... Mwenyezi Mungu amesema: {Na anaye mpinga Mtume baada ya kumdhihirikia uwongofu, na akafuata njia isiyo kuwa ya Waumini, tutamuelekeza aliko elekea, na tutamuingiza katika Jahannamu. Na hayo ni marejeo maovu.} [An-Nisaa’: 115]. Vile vile Mtume wa Mwenyezi Mungu anasema: “Anayebeba silaha dhidi yetu si miongoni mwetu” [Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari na Muslim]. Pia Mtume (S.A.W.), anasema: “Muumini atabakia katika duara la matumaini na Imani madamu hatamwaga damu iliyoharamishwa” [Imepokelewa kutoka kwa Al-Bukhari]. Na bwana wetu Abdullah bin Al-Abbas (R.A) alipokwenda kujadiliana na Makhariji, aliwaambia: Je, mmeona kwamba nikikusomeeni kutoka katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu kinachopambanua na nikikusomeeni kutoka katika Sunna za Mtume wake (S.A.W), kwa msiyoyapinga je, mtarudi? Wakasema: Ndiyo. Alipowaeleza, watu elfu ishirini walirudi, wakabaki elfu nne, nao wakauawa. [Imepokelewa kutoka kwa Abdur Raziq]. Na hakuna kinachomzuia mtu kufuata haki baada ya kumdhihirikia isipokuwa mwenye ugonjwa katika nafsi yake, kama vile kiburi na husuda. Mgonjwa wa kwanza ulimpotosha Shetani, na wa pili uliwapotosha Mayahudi wa Madina wakati wa Mtume (S.A.W.).