Kutoa Zaka ya Fitri Mali

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutoa Zaka ya Fitri Mali

Question

Kutoa Zaka ya Fitri Mali

Answer

Mwenyezi Mungu Ameweka Sharia ya Zaka ya Fitri ili kumtakasa mfungaji na kumsafisha kutokana na machafu na kauli chafu, lakini pia kuwatosheleza watu masikini kuto ombaomba siku ya Idi ambayo Waislamu wanakuwa kwenye furaha kwa kufika kwake, na Mtume S.A.W. anasema: “Watoshelezeni na kutozunguka mitaani kuombaomba ndani ya siku hii”([1]).

Na Zaka ya Fitri ni sadaka inamlazimikia mfungaji wa funga ya Ramadhani kwa kiwango maalumu kwa kila nafsi ya Muislamu, anaitoa mtu kwa ajili yake mwenyewe pamoja na wale wanaomlazimu kuwahudumia. Imamu Ibn Al-Mundhir amesema: “Wamekubaliana Wanachuoni kuwa Zaka ya Fitri ni lazima”([2]).

Zaka ya Fitri hutolewa kwa kuwapa watu masikini na mafakiri vilevile na waliobakia katika watu wa makundi manane ambayo yametajwa na Mwenyezi Mungu ndani ya Aya ya matumizi ya Zaka. Mwenyezi Mungu Amesema: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Mwenyezi Mungu, na wasafiri. Huu ni wajibu uliolazimishwa na Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua Mwenye hekima} [AT TAWBAH: 60].

Katika utafiti huu tunaelezea rai na mitazamo ya Wanachuoni kuhusu utoaji wa Zaka ya Fitri, na je inafaa kutoa thamani au hapana?

Madhehebu ya Wanachuoni kuhusu utoaji wa Zaka ya Fitri na maelezo ya kile kinachoruhusiwa na kisichoruhusiwa.

Madhehebu ya Jamhuri:

Jamhuri ya Wanachuoni wa madhehebu ya Imamu Malik na Imamu Shafi pamoja na Imamu Hanbal wamesema kuwa Zaka ya Fitri ni pishi moja, na yenyewe haifai kutolewa thamani wala sehemu kwa sababu hakuna Andiko kwenye hilo.

Watu wa Imamu Malik wanaona kuwa Zaka ya Fitri ni pishi moja kwa kila mtu, na pishi moja ni vibaba vinne, ambapo ni jambo la lazima lenye kuthibiti kwenye Sunna, kwa maneno ya Mtume S.A.W.: “Mtume wa Mwenyezi Mungu Amelazimisha Zaka ya Fitri pishi moja ya tende au pishi moja ya ngano kwa mtu huru, mtumwa, mwanamume, mwanamke, mtoto mdogo na mtu mkubwa katika Waislamu”([3]). Ikiwa Zaka ya Fitri imelazimishwa na aliyelazimishwa akakosa uwezo wa kutoa pishi mzima bali ana uwezo wa kutoa sehemu ya pishi basi atatoa hiyo sehemu ni kauli ya wazi ya madhehebu kwa kauli ya Mtume S.A.W.: “Pindi ninapokuamrisheni jambo basi litekelezeni kiasi mwezavyo”([4]).

Mtu anatoa chakula kinachotumiwa sana na watu wa mji ambapo ni moja kati ya aina zifuatazo: Ngano, nganombichi, zabibu, ngano iliyokobolewa, tende, mchele, mahindi, maziwa yaliyokaushwa, wala haitoshelezi kutoa isipokuwa chakula kinachotumika sana au kitakachokuwa bora zaidi, kama vile ikiwa chakula kinacholiwa sana ni vyakula vya ngano kisha akatoa ngano, kama vile haifai kutoa kisichokuwepo kwenye aina hizi kama vile mtu kutoa maharage au adesi na dengu isipokuwa kama kitakuwa ndio chakula cha watu wengi na wakaacha hizi aina zilizotajwa, pindi mtu akitaka kutoa Zaka yake sehemu ya nyama na ikazingatiwa inatosha kuitoa, kwa mfano ikiwa kibaba kimoja cha ngano kinatosheleza kwa watu wawili ikiwa watatengeneza mkate basi ni lazima kutoa nyama inayotosheleza watu wawili([5]).

Na Imamu Malik amesema katika kitabu cha Al-Mudawwana: “Haitoshi kwa mtu kutoa sehemu ya Zaka ya Fitri vitu katika vitu, akasema: Na wala hilo Mtume S.A.W. hajaamrisha([6]).

Na wakaeleza watu wa Imamu Shafi kuwa, Zaka ya mtu mmoja ni pishi moja kwa Hadithi iliyotokana na Ibn Umar R.A. amesema: “Mtume wa Mwenyezi Mungu Amelazimisha Zaka ya Fitri pishi moja ya tende au pishi moja ya ngano kwa mtu huru, mtumwa, mwanamume, mwanamke, mtoto mdogo na mtu mkubwa katika Waislamu” na Hadithi kutoka kwa Abu Said R.A. amesema:  “Tulikuwa tunatoa Zaka ya Fitri wakati Mtume S.A.W. tukiwa naye pishi moja ya chakula, au pishi moja ya tende, au pishi moja ya nganombichi, au pishi moja ya zabibu, sikuacha kutoa hivyo kama nilivyokuwa natoa kipindi chote cha maisha yangu”([7]).

Na aina ya pishi iliyo lazima ni chakula cha sehemu ya kumi, kwa maana ambacho lazima kutolewa sehemu ya kumi au nusu yake, kwa sababu nusu imepokelewa katika baadhi ya vitu vya sehemu ya kumi kama vile nganonzima, ngano, tende na zabibu, na linganisha vyakula vilivyobaki, na katika madhehebu ya zamani ya Imamu Shafi yanasema kuwa haifai kutoa Zaka adesi na humus kwa sababu zenyewe huliwa na mkate, vilevile haifai kutoa ufuta kwa kauli ya wazi, kwa kuthibiti kwake ndani ya sahih mbili Hadithi inayotokana na Abu Said Al-Khudry R.A. Hadithi iliyoelezewa hapo mwanzo([8]).

Imamu An-Nawawy amesema kwenye kitabu cha Al-Minhaaj: Kilichowajibu kutoa ni nafaka, kauli hii ikaelezewa na Sheikh Khatib Sharbiny akasema: Ambapo ameainisha hivyo haitoshelezi thamani kwa makubaliano, wala kutoa mkate wala unga na mfano wa hivyo([9]).

Na watu wa Imamu Hanbal wanaona kuwa kilicholazima katika Zaka ya Fitri ni kutoa pishi moja ya ngano nayo ni vibaba vinne kwa pishi ya Mtume S.A.W. ni viganja vinne vya mtu wa umbile la kati na kati, au pishi moja ya tende au zabibu au ngano kwa Hadithi ya Abu Said Al-Khudry iliyotangulia, na inatosha kutoa unga baada ya ngano kukaushwa kisha kusagwa, akapinga Imamu Ahmad kwenye sehemu ya unga na akawa na rai ya peke yake Ibn Aiinah katika Hadithi ya Abu Said: “Au pishi moja ya unga wa ngano”, wala haitoshi kutoa Zaka mkate kwa sababu si katika vitu vya kupimwa kwenye mizani na kuhifadhiwa kwa muda mrefu, lakini unafaa kutolewa mkate panapokosekana kingine, kwa maana ya kukosekana aina tano kile kinachochukua nafasi yake katika nafaka zinazoliwa, na katika tende yenye kupimwa kama vile mahindi adesi mchele tinikavu na mfano wake, kwa sababu vinafanana na aina iliyoelezewa, basi imekuwa ni bora zaidi kutoa tende kwa mujibu wa Andiko na kwa kulifanya hilo Ibn Umar, Nafii amesema: “Ibn Umar alikuwa anatoa tende isipokuwa ndani ya mwaka mmoja zilikosekana tende akatoa ngano”. Na akasema Abu Majaz: “Hakika Mwenyezi Mungu Amekunjua zaidi na ngano ni bora zaidi, Mtume S.A.W. akasema: “Hakika Masahaba wangu wamepita njia na mimi napenda nipite”, uwazi ni kuwa: Masahaba walikuwa wanatoa Zaka ya Fitri tende kwa sababu ni chakula chenye utamu na zinapatikana kwa ukaribu zaidi na gharama yake ni ndogo, na zabibu zenyewe ni chakula chenye utamu na gharama yake ni ndogo, hivyo zenyewe zinafanana na tende kwa sababu ulinganishi hufanywa kwa vitu vyote, lakini kuacha kuwafuata Masahaba katika kutoa tende na vinavyoshiriki pamoja kwenye maana, nayo ni zabibu basi ina manufaa zaidi katika chakula na kuondoa hitaji la mtu masikini, ikiwa inalingana kwenye manufaa basi ngano, na kilichobora ni kutopungua kilichotolewa Zaka robo ya pishi au nusu ya pishi ili kumtosheleza na vitendo vya kuomba hiyo siku([10]).

Na katika kitabu cha Iqnaa na sherehe yake cha Bahwaty katika vitabu vyao kinasema: “Haitoshi kutoa Zaka ya Fitri tofauti na aina hizi tano pamoja na kuwepo uwezo wa kuzipata” kwa maelezo yaliyotangulia hakuna kutoa Zaka kwa thamani, kwa sababu katika hilo hakuna tamko lake, na pia:  Amesema Abu Daud alisema kumuuliza Ahmad: Je naweza kutoa Dirham katika Zaka ya Fitri? Akasema: Ninahofia kutofaa ni tofauti na Sunna ya Mtume S.A.W.([11]).

Madhehebu ya Imamu Abu Hanifah

Abu Hanifah anaona kuwa ni lazima katika Zaka ya Fitri kutoa nusu ya pishi ya ngano au unga au zabibu au pishi ya tende, ama sifa yake ni wajibu ulioelezewa na Maandiko kwa sababu ni mali yenye kuthaminiwa moja kwa moja na wala si kwa upande wa vitu, hivyo inafaa kutoa katika vitu hivyo vyote thamani ya Dirham au Dinar au pesa au kitu cha thamani au mtu anachotaka([12]).

Imamu As-SarkhasIy amesema: Ikiwa atatoa thamani ya ngano basi kwetu sisi inafaa, kwa sababu kinachozingatiwa ni kupata toshelezo na hilo ni pamoja na kupata thamani kwa maana ya pesa kama vile anavyopata hiyo ngano, na kwa upande wa Imamu Shafi R.A. anasema haifai kutoa thamani, asili ya tofauti katika Zaka Imamu Abubakr Al-Aamash anasema: Kutoa ngano ni bora zaidi ya kutoa thamani kwa sababu kutoa ngano kuko karibu zaidi na utekelezaji wa amri na kuko mbali na tofauti za Wanachuoni hivyo kutoa thamani kumekuwa ni sehemu ya akiba, na Mwanachuoni Abu Jafar anasema: Kutoa thamani ni bora zaidi kwa sababu kuko karibu zaidi na manufaa ya mtu masikini kwa sababu atanunua kwa hivi sasa kile anachokihitaji, na kutajwa kwa ngano na nganonzima ni kwa sababu vitu vya kuuzwa wakati huo ndani ya mji wa Madina vilikuwa hivyo, ama ndani ya nchi zetu mauziano yanafanyika kwa kulipia pesa, nayo ndiyo mali inaheshimika zaidi hivyo kutumia pesa ni bora zaidi([13]).

Na haya pia madhehebu ya Wanachuoni wa kundi la Taabiin, kama vile ni kauli ya kundi la Wanachuoni wanaofahamika miongoni mwao: Al-Hassan Al-Basry ambapo imepokelewa akisema: “Hakuna ubaya kutoa Dirham katika Zaka ya Fitri”([14]), na Abu Isaka As-Sabii kutoka kwa Zuheir amesema: Nimemsikia Aba Isaka anasema: “Nimewakuta katika Zaka ya Fitri wanatoa Dirhamu kama thamani ya chakula”([15]), na Umar Ibn Abdulaziz kutoka kwa Wakii kutoka kwa Qurrah amesema: Ilitufikia barua ya Umar Ibn Abdulaziz kuhusu Zaka ya Fitri: “Nusu pishi kwa kila mtu au thamani yake nusu Dirham”([16]), nayo ni madhehebu ya Thawry, na katika hilo amesema Isaka Ibn Rahawiyah na Abu Thawr, isipokuwa hao wawili wameliweka hilo katika hali ya dharura([17]), maelezo haya yanakubaliana kwa ukaribu na madhehebu ya Isaka na Abu Thaur, Sheikh Taqiyyuddeen Ibn Taimia ameeleza: “Kutoa thamani pasi na kuwepo haja ya kufanya hivyo wala masilahi yanayozingatiwa ni jambo lisilofaa”([18]), imefahamika kutoka kwake kuwa kutoa thamani kwa uwepo wa haja na kuwepo masilahi basi si jambo lenye kuzuiwa, kauli hii kwake ni katika Zaka za aina zote ikiwa ni pamoja na Zaka ya Fitri pia, kama vile kauli ya kutoa sehemu ya thamani katika Zaka ya Fitri ni mapokezi yaliyotoka pia kwa Imamu Ahmad ameelezea hilo Imamu Mardawey katika kitabu cha Insaaf([19]).

Fatwa tunayopitisha sisi ni kufaa kutoa Zaka ya Fitri mali, na haya ndiyo madhehebu ya Abu Hanifa, na kwa kutoa mali ndiko kumefanyiwa kazi na kutolewa Fatwa na watu wa Abu Hanifa katika Zaka zote na katika kafara, nadhiri, kharaj na vinginevyo kama vile Fatwa hiyo ni ya madhehebu ya Wanachuoni katika Taabiin kama ilivyoelezewa.

Miongoni mwa walioipa nguvu kauli hii na kuitetea miongoni mwa Wanachuoni waliokuja baadaye ni Ahmad Ibn Siddiq Al-Ghumary ambaye alitunga ujumbe wake maarufu na muhimu pia wenye faida katika hili, na ambao ameuita: “Kufikia matumaini kutoa mali katika Zaka ya Fitri” ametaja ndani yake dalili thelathini na mbili za uhalali wa kutoa Zaka ya Fitri mali, na miongoni mwa waliotia nguvu jambo hili na pia kulitetea katika Wanachuoni waliokuja baadaye ni Sheikh Mustafa Zarka, anao utafiti mrefu akitetea ndani yake kauli ya kufaa kutoa mali katika Zaka ya Fitri.   

Na yafuatayo ni maelezo ya dalili muhimu ambazo zimetumika katika kuruhusu kutoa mali katika Zaka ya Fitri, ambapo sehemu haitoshi kutaja dalili zote([20]).

Kwanza: Asili katika sadaka ni mali. Mwenyezi Mungu Amesema: {Chukua sadaka katika mali zao} Attawbah: 103. Na mali kwa asili ni inayomilikiwa miongoni mwa madini ya dhahabu fedha, katika maelezo ya Mtume S.A.W. kuhusu Zaka ya Fitri na yaliyotamkwa ni kwa njia ya kurahisisha na kuondoa uzito na wala si kufungamanisha ulazima na kukomea makusudio, kwa sababu asili ya watu wa mijini wanapendelea fedha.

Pili: Kuchukua thamani katika Zaka ni jambo lililothibiti kutoka kwa Mtume S.A.W. na kwa Masahaba ndani ya zama zake na baada ya zama zake, miongoni mwa hayo ni pamoja na yaliyopokelewa kutoka kwa Taawsi. Muadhi amesema kuwaambia watu wa Yemen: Nileteeni nguo au mavazi katika utoaji wa Zaka sehemu ya ngano na mahindi ni wepesi zaidi kwenu na ni bora kwa Masahaba wa Mtume S.A.W. huko Madina.

Imamu Bukhari amesema ndani ya Sahihi yake kwenye mlango wa Zaka. Taawus amesema: Muadhi amesema kuwaambia watu wa Yeman: “Nileteeni nguo katika Zaka sehemu ya ngano na mahindi ni wepesi zaidi kwenu na bora kwa Masahaba wa Mtume S.A.W. huko Madina”([21]). 

Al-Hafidh amesema katika kitabu cha Al-Fathu katika kauli yake: Mlango wa mali ya Zaka, kwa maana inafaa kuchukua mali, Ibn Rashiid amesema Imamu Bukhari amepitisha katika masuala ya Imamu Abu Hanifah pamoja na kupingana nao lakini ameongoza kwenye kauli hiyo. “Na kauli yake Tauus amesema, amesema Muadhi kuwaambia watu wa Yemen…” maelezo haya ni sahihi kuhusishwa kwa Taaus lakini Taaus hakusikia kutoka kwa Muadhi hivyo ni mwenye kukatika kwenye mnyororo wa wapokezi, hivyo hakuna mazingatio kwa kauli ya mwenye kusema ametaja Imamu Bukhari kwa maelezo ya moja kwa moja hiyo ni sahihi kwake, kwa sababu hilo halimaanishi isipokuwa usahihi wa mwenye kusema, ama mapokezi mengine hapana isipokuwa upokezi wake kwake ni sehemu ya kupingwa kunahitaji nguvu yake kwake kana kwamba ameshikilia Hadithi ambazo amezitaja kwenye mlango huu, na tumepokea maelezo ya Taaus aliyetajwa ndani ya kitabu cha mambo ya Kharaaj cha Yahya Ibn Adam kutokana na upokezi wa Ibn Taimia kutoka kwa Ibrahim Ibn Maisarah na Amru Ibn Dinar Taaus amewaelezea kila mmoja peke yake([22]).

Na Imamu Shafi amesema: “Taaus ni mwenye kufahamu amri za Muadh, pamoja na kuwa hajakutana naye sana kama walivyokutana naye wale waliomwahi Muadh miongoni mwa watu wa Yemen”([23]).

Muadhi alifanya hivyo na kukubalika na Mtume S.A.W. kwenye hilo ni dalili ya kufaa kwake na uhalali wake.

Na katika hayo pia: Yaliyopokewa na Ibn Abu Shaibah katika kitabu cha Musannaf ambapo amesema: Jarir Ibn Abdilhamid ametuzungumzisha kutoka kwa Laith kutoka kwa Ataa kuwa Umar R.A. alikuwa anachukua mali za Zaka([24]).

Na yaliyopokelewa pia kutoka kwa Wakii kutoka kwa Abu Sinan kutoka kwa Antara: Kuwa Ali alikuwa anachukua mali katika Fidia kwa watu wa fedha huchukua fedha na kwa watu wa mazao huchukua mazao([25]).

Tatu: Pindi inapothibiti kufaa kuchukua thamani katika Zaka ya lazima ya vitu basi kufaa huko katika Zaka ya lazima kwa kila mtu ni bora zaidi, na hilo ni kwa sababu Zaka ya Fitri ni lazima kwa mwanamume, mwanamke, mtu huru, mtumwa, mtu mzima, mtoto mdogo, tajiri na masikini, pindi hali ilipokuwa hivyo hekima na busara imepelekea kuamrisha watu kutoa chakula ili kuwezesha watu wote kutekeleza amri hii bila uzito wala ugumu wowote unaoweza kupelekea watu kuacha kutekeleza, kwa sababu fedha zilikuwa ni chache kupatikana katika nchi za Kiarabu ndani ya zama hizo, hivyo lau ingeamrishwa watu kutoa fedha katika Zaka ya lazima kwa kila mtu ingeleta ugumu kwa watu masikini kutoa hiyo Zaka, na ingekuwa uzito pia kwa matajiri wengi ambao utajiri wao mwingi ulikuwa kwa kumiliki wanyama wengi watumwa na chakula kama vile ilivyokuwa hali ya watu wa vijijini na maeneo mengine leo hii, fedha ni chache mikononi mwao tofauti na chakula chenyewe ni chepesi kwa watu wote, hivyo ikawa masilahi makubwa na hekima kubwa ya chakula kuchukua nafasi ya fedha ni wepesi wa uwepo wake na kuweza kutolewa na watu wote.

Nne: Ni kuwa Mtume S.A.W. alibadilisha kati ya kiwango cha lazima cha vitu vilivyotajwa pamoja na usawa wake katika kutosheleza mahitaji hivyo hilo likaonesha kuwa amezingatia thamani na wala hajazingatia vitu, ambapo amelazimisha tende na nganonzima pishi moja lakini unga wa ngano nusu pishi.

Imamu Ahmad Ibn As-Siddik alirekebisha mapokezi ambayo yameelezea nusu pishi, bali akaelezea kuwa kupokelewa nusu pishi kutoka kwa Mtume S.A.W. kuna mapokezi mengi([26]).

Tano: Imepokelewa kutoka kwa Masahaba kutolewa kiwango cha lazima katika Zaka ya Fitri ni kwa njia ya jitihada kutoka kwa baadhi yao, na hii ni dalili kuwa wao walifahamu kutoka kwa Mtume S.A.W. mazingatio ya thamani na kuchunga masilahi na katika hilo kuna dalili na athari, miongoni mwa dalili hizo: Maelezo yaliyopokelewa na Maimamu sita kutoka kwa Abu Said Al-Khudry amesema: “Tulikuwa tunatoa Zaka ya Fitri wakati wa Mtume S.A.W. kila mtu mkubwa na mdogo huru au mtumwa pishi ya chakula au pishi ya nganonzima au pishi ya tende au pishi ya maziwa ya mgando au pishi ya zabibu, tuliendelea kutoa vitu hivyo mpaka alipotujia Muawiyah Ibn Abu Sufyan akitokea Hija au Umra, akazungumza na watu kwenye mimbari, miongoni mwa aliyowaambia watu ni pamoja na kusema: Mimi naona kuwa vibaba viwili vya huko Sham ni sawa sawa na pishi moja ya tenda, hivyo watu wakachukua hivyo, Abu Said amesema: Ama kwa upande wangu mimi bado niliendelea kutoa kama nilivyokuwa natoa kwa siku zote nilizoishi”([27]).

Sita: Mtume S.A.W. amesema: “Watoshelezeni waepuke kuomba siku hii”([28]).

Katika Hadithi hii kuna dalili nyingi:

Miongoni mwa hizo: Ni kuwa Mtume S.A.W. alieleza wazi sababu ya ulazima wa Zaka, nayo ni kuwatosheleza watu masikini siku ya Idi. Na hilo kwa mali ni bora zaidi kuliko kitu kingine, kwa sababu ndiyo asili inayoungana na kila kitu katika mahitaji muhimu ya maisha, isipokuwa chakula katika zama hiyo kilikuwa ndio bora zaidi, kwa upande wake Mtume S.A.W. kutaka kutosheleza mahitaji ya watu masikini kwa kuhusisha siku hii ya Idi na kuwazuia na vitendo vya kuzunguka mitaani kuomba na kutaabika kupata chakula cha siku hiyo, kwa sababu wakati huo masokoni hakukuwa na unga wa ngano wala mikate wala chakula kilichopikwa bali inawezekana pia nafaka zilikuwa hazipatikani sokoni, na wala hazipatikani isipokuwa ndani ya nyakati maalumu pale wafanyabiashara wanapohitaji kutoka nje na huenda siku ya Idi masoko yakawa yamefungwa, lau Mtume S.A.W. angeamrisha kutumika Dirham makusudio ya kumtosheleza masikini kutohangaika na mahitaji ya chakula siku ya Idi yangekosekana,  hivyo Mtume S.A.W. akaamrisha kutolewa chakula ili kuondoa uzito wa kutafuta na kuhangaishwa na kuomba, ama ndani ya zama zetu hizi tulizonazo hali ni tofauti na wakati huo, kwani chakula kinapatikana kwa wepesi masokoni na madukani hivyo kila anachokihitaji masikini anakipata bila ya matatizo yoyote pindi tu anapokuwa na fedha mkononi mwake, bali kadhia ipo kinyume tabu na uzito vimehamia kwenye kunufaika na hizo nafaka ikawa suala la kutoa pesa ni bora zaidi kwa ajili ya lengo hili.

Miongoni mwa dalili pia: Ni kuwa Mtume S.A.W. amefungamanisha na kutosheleza watu masikini siku ya Idi ili furaha isambae kwa Waumini wote na kuwa sawa tajiri na masikini na Waumini wote kuwa na muda wa kumtaja Mwenyezi Mungu kumwabudu kumsifu na kumshukuru kwa neema alizoneemesha, na maana hii haipatikani hiyo siku kwa kutoa nafaka ambayo si chakula cha masikini na watu wote, wala si katika uwezo wao kunufaika nacho katika siku hiyo hata kama watataka kula – tofauti na mazoea yao – kwa kukosekana kwa morali majumbani mwao, kisha pindi wakitaka kuuza hawataweza, hivyo makusudio ya Sharia hayapatikani ikiwa ni pamoja na kuwatosheleza mahitaji ya siku hiyo, bali makusudio yanafikiwa kwa kutolewa mali kwa maana fedha ambayo masikini inamnufaisha, ikawa kutoa fedha ni vizuri na bora zaidi.

Na dalili nyingine: Ni kuwa Mtume S.A.W. amesema: “Watoshelezeni” kutosheka ni kuwepo kitu kinachomfikisha mwanadamu kwenye mahitaji yake, na mahitaji kama yanavyokuwa kwenye chakula yanakuwa pia kwenye mavazi na vitu vingine vya lazima katika maisha, na kutoa fedha kunaziba mianya kwa pande zote, nayo fedha hufikia toshelezo linalokusudiwa na Sharia, na ndiyo inayohusishwa na iliyobora.

Saba: Mtume S.A.W. amelazimisha Zaka ya Fitri ili kulisha watu masikini kama ilivyokuja kwenye Hadithi, na nafaka sio chakula cha watu hii leo.

Nane: Mtume S.A.W. ameainisha chakula ni kutokana na uchache wake masokoni ndani ya zama hizo na watu masikini kuhitaji sana chakula na wala si fedha.

Tisa: Mwenyezi Mungu Amesema: {Kabisa hamtafikia wema mpaka mtoe katika vile mnavyo vipenda} Aal-Imraan: 92, na mali leo hii ndiyo inayopendwa sana kwani watu wengi hawana umuhimu sana na ulishaji chakula na kuupa uzito utoaji fedha kwa masikini, hali enzi za Mtume S.A.W. ni tofauti na hii, hivyo kutoa chakula ni bora zaidi kwa upande wao na kutoa fedha ni bora zaidi ndani ya zama zetu kwa sababu ndizo zenye kupendwa sana.

Kumi: Kusudio la Sharia kulazimisha Zaka siku ya Idi ni kuleta furaha kwa watu masikini kwa kuwepo chakula cha kuwatosheleza ili furaha iende kwa Waumini wote na wala isiwe kwa matajiri tu.

Kwa sababu hiyo imewekwa sharti la kutolewa kwake kabla ya Swala na akasema S.A.W.: “Mwenye kutoa kabla ya Swala basi hiyo ni Zaka yenye kukubaliwa, na mwenye kuitoa baada ya Swala hiyo ni sadaka miongoni mwa sadaka” na hilo ili iwezekane kugaiwa kabla ya Sala na masikini awe na utulivu wa kuwepo chakula chake ndani ya siku hii, na lau kama si kwa maana hii basi Mtume S.A.W. asingeweka sharti la kuitoa kabla ya Swala, na kubadilika hukumu yake kati ya kabla ya Swala na baada ya Swala, kwa kuifanya ya kwanza ndiyo lazima na ya pili kuwa sadaka miongoni mwa sadaka, na hekima ni ile tuliyoitaja, na kama sio hivyo basi inafahamika kuwa kunufaika masikini kwa kibaba cha chakula kabla ya Swala ni sawa sawa kwake na kuchukua baada ya Swala bila ya kuwepo tofauti yoyote, na kusudio hili halifikiwi hii leo kwa masikini kwa kuwapa nafaka, kwa sababu pamoja na kuwa si chakula chao hivyo wao ni wenye kuhitaji kitu chengine kitakacho wawezesha kupata pia na nyama siagi za mikate mbagomboga na vingine, miongoni mwa vitu vinavyowatia huzuni sana kwa kuvikosa siku ya Idi, na kwa sababu hii Mtume S.A.W. akafanya vitu mbalimbali kwenye kutoa Zaka ya Fitri miongoni mwa hivyo chakula kama vile ngano na nganonzima, pia miongoni mwazo vipo ambavyo ni chakula na vitu vitamu kama vile tende na zabibu, katika zama zetu za sasa hakuna kuhitajika sana aina hizi ni kwa sababu ya kutotumika kwake kwa wingi, ikiwa mahitaji yatabadilika au yakawa tofauti itafaa kutoa Zaka chakula au thamani yake ambayo inayopeleka kwenye hiko chakula.

Kumi na Moja: Mtume S.A.W. hakuishia ulazima katika vilivyotamkwa na kusema haifai kutoa visivyokuwa hivyo vilivyotajwa, bali amezungumzia sababu ambayo inakusanya fedha kwa hatua ya kwanza, hivyo Masahaba katika zama za Mtume S.A.W. walitoa zabibu, ngano iliyokobolewa na maziwa ya mgando pamoja na kuwa hawakulazimishwa zaidi ya tende nganonzima na ngano ya kawaida miongoni mwa vyakula hivyo vilikubaliwa na wala havikurudishwa kwao, ikawa ni dalili kubwa ya kutohusisha idadi maalumu katika aina zilizotajwa, na kusudio alilolitaja katika sababu nalo ni: Kuwatoshelezea masikini mahitaji siku ya Idi, hivyo Masahaba wakaja na kila kinachozingatiwa toshelezo katika zama zao hata kama hakijatajwa na Mtume S.A.W. na kutosheleza katika zama zetu ni kwa fedha hivyo ikawa kutoa Zaka kwa fedha ndiyo bora zaidi.

Kumi na Mbili: Ni kuwa lau lisingepokelewa tamko la sababu basi akili na ushahidi wa hali ya leo na msingi wa Sharia vingehukumu kwa mazingatio yake, na kilichopitishwa katika msingi wa Sharia ni kuwa asili katika hukumu ya Kisharia ni kukubaliana na akili na wala si nadharia ya ibada, ni sawa sawa katika hayo yanayofungamana na ibada au mashirikiano, kwani hukumu inapokuwa maana yake inakubaliana na akili inakuwa karibu zaidi na utekelezaji na kupelekea kukubalika, kwani utekelezaji wa kitu kinachokubaliana na akili kipo karibu zaidi tofauti na visivyokuwa hivyo, na nafsi kwenye kukubali hukumu inayotekelezwa na masilahi inaelekea zaidi huko na kukubali hukumu inayotumika na kuwa mbali na mtazamo wa kufuata tu, na ikawa inatosheleza zaidi kwenye makusudio ya hukumu ya Sharia([29]).

Ibn Dakiku Al-Abdi amesema: “Wakati wowote hukumu inapokuwa kati ya kufuatwa tu au yenye maana inayokubaliana na akili hufuatwa kwa kuwa maana yake inakubaliana na akili ni bora zaidi kutokana na uchache wa hukumu za kufuata tu kwa upande wa hukumu zenye maana inayokubaliana na akili([30]).

Zaka ya Fitri asili yake ni yenye maana inayokubaliana na akili kama vile Zaka ya Mali ambayo ni jukumu la kimali la kijamii kwa masilahi ya watu masikini ambao wanapaswa kuendelezwa na matajiri, jamii ya Kiislamu haiwezi kuwa makundi mawili wala kuwa na wakati yao, kundi la matajiri na kundi la masikini waliokosa kipato.

Sharia ya Zaka ya Fitri na Zaka ya Mali maana zake zinakubaliana na akili, na pindi zinapofanana ni lazima kuangalia kilicho na manufaa zaidi kwa masikini au kilichochepesi zaidi kwa mtu kutekeleza, wala haisemwi kuwa Zaka ni kama vile idadi ya rakaa za Swala kuwa zimeshapangwa akili haipaswi kuziangalia, bali tofauti kati yake na idadi ya rakaa za Swala ni kubwa sana.

Hivi unaona kuwa kuainisha viwango katika Zaka ya Fitri kwa makubaliano ya Wanachuoni wa madhehebu kuwa ni mpangilio wa kiwango cha chini ambacho haifai kutoa chini zaidi ya hapo, lau mtu mwenye jukumu la kutoa Zaka akaongeza zaidi ya kiwango basi ana fadhila na malipo, wakati ambapo lau mtu mwenye kuswali akazidisha idadi ya rakaa za Swala ya lazima haifai kwake na wala Swala yake haikubaliki.

Kumi na Tatu: Kilichotamkwa ni maelezo ya kiwango cha lazima kutolewa na wala sio kitu chenyewe, ambapo lau ingekuwa maelezo ya wajibu wa kitu basi Masahaba wasingetofautiana na wala Tabiin Maimamu na Wanasheria, wametaja vitu havijapokelewa tamko lake katika Sharia, na ikiwa itathibiti hivyo basi inafaa kutoa mali.

Kuni na Nne: Kutoa mali katika zama hizi inakusanya uletaji masilahi na kuondoa uharibifu hivyo hutangulizwa zaidi ya utoaji wa nafaka ambayo ina masilahi yanayokutana na uharibifu wa kupoteza mali, kwa sababu masikini wanauza hizo nafaka kwa thamani ndogo hivyo hupoteza mali nyingi kati ya mnunuzi kwa ajili ya Zaka na muuziaji masikini, masikini wangapi wasio na kitu kinachowatosheleza kuuza hivyo hupoteza bila ya kunufaika.

Kumi na Tano: Kuchunga masilahi ni katika msingi mkubwa wa Sharia na hukumu zake zimetoa sababu ambazo hujengewa na Sharia zote, popote yanapozunguka masilahi hayo huzunguka pamoja, kwani Sharia zote zimejengwa kwa kuleta masilahi na kuondoa uharibifu, na kwa kanuni hii Ezz Abdilsalaam amejenga kanuni zake kubwa ambazo Mwanachuoni na Mufti wanapaswa kujengea hukumu kwenye kanuni hizo.

Mwenye kuzingatia amri atakuta Sharia imeamrisha kwa kuwepo masilahi ya kidunia na kiakhera, na mwenye kuzingatia makatazo pia atakuta yamekatazwa kwa kuwepo uharibifu kidunia na Akhera, kwa mujibu wa kusisitiza masilahi na ukubwa wake ndio kunakuwa na jambo la Wajibu Sunna na Kupendelewa na Wanachuoni, na kwa ukubwa wa uharibifu ndio kunakuwa na kitu Haramu na kuchukiza, kutokana na hayo yapo yaliyowazi hufahamika na kila mtu na yapo yaliyojificha hayafahamiki isipokuwa kwa watu waliotangulia katika ufahamu na elimu.

Kwa mfano uongo ambao ni katika haramu ambapo Sharia imeahidi adhabu kali kwa mwenye kuutumia pindi ulipoonekana uharibifu wake unaleta masilahi makubwa ambayo ni kujenga kati ya watu basi Sharia wakati huo ukauhalalisha, bali uongo unaweza kuwa ni jambo la lazima kuna adhabu kwa mwenye kuuacha, kama uongo huo utapelekea kuzuia umwagaji damu ya Muislamu asiye na hatia.

Na kama hivyo hukumu zote za Sharia hujengwa kwa kuchunga masilahi na huzunguka na masilahi hayo popote pale, kama yanavyofahamika hayo kwa mwenye kuyafuatilia na kwa mtazamo wa kina zaidi, pindi linapothibiti hilo basi masilahi yanapelekea kutoa mali na kutanguliza utoaji mali kuliko utoaji wa nafaka.

Kumi na Sita: Kusimama na Andiko na kushikamana na yaliyowazi katika yale ambayo yameelezewa sababu, hekima ya wazi, ni kiini cha ukweli na kinyume cha makusudio ya Sharia, kwani mwenye kuisikia kauli ya Mwenyezi Mungu: {Hakika wanao kula mali ya mayatima kwa dhuluma} [AN-NISAA: 10], inabeba ulaji tu na kunufaisha upande wa mavazi chombo cha usafiri makazi na vingine, inakuwa ni kwenda kinyume na Aya na kuingia kwenye adhabu kwa makubaliano ya Wanachuoni wa Umma bali na kwa watambuzi pia pamoja na kushikamana na maana ya nje na akasimama na Andiko, vilevile mwenye kusikia kauli ya Mwenyezi Mungu kwa upande wa haki za wazazi wawili: {Basi usimwambie hata: Ah! Wala usiwakemee} [AL-ISRAA: 23], kuwatemea mate usoni mwao kuwadhuru na kushikamana na Andiko la lawama na karipio inakuwa ni kikwazo kinaingia katika katazo na ahadi ya adhabu bila ya tofauti yoyote kwa watu wenye utambuzi, kinachoegemewa ni dhamira ya mzungumzaji na makusudio yake na wala si matamshi kwa sababu matamshi hayajajikusudia yenyewe bali yamedhamiria maana na kufikia kufahamu makusudio, hivyo zingatio ni manufaa na makusudio na wala si njia na sababu.

Ufupi wa Utafiti:

Ambalo tunamalizia mwishoni mwa utafiti ni kuwa kutoa Zaka ya Fitri chakula ndio asili ya Matamko katika Sunna Takatifu za Mtume S.A.W., na kwa hilo limeungwa mkono na Jopo la Wanachuoni wa madhehebu yanayofuatwa, isipokuwa kutoa thamani ni jambo lenye kufaa na kuruhusiwa, na hili limesemwa na Wanachuoni wa madhehebu ya Abu Hanifa na kundi la Wanachuoni katika Tabiiin na kundi la watu wa elimu wa zamani na wasasa, nayo pia ni upokezi uliotokana na Imamu Ahmad bali na Imamu Ramly katika Maimamu wa watu wa Shafi ametoa Fatwa katika Fatwa zake inafaa kumfuata Imamu Abu Hanifa R.A. katika kutoa badala ya Zaka ya Fitri Dirhamu kwa aliyemuuliza hilo([31]). Na sisi tunaona kuwa madhehebu haya yenye kusema inafaa na kuruhusiwa kutoa thamani ni yenye kufikia zaidi masilahi na ndiyo kauli yenye nguvu zaidi katika zama zetu hizi.

Naye Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi

Imeandikwa Na: Mustafa Abdul Kariim Muhammad

              20/09/2007. 

 

([1]) Sunanu DaaruQutuny 2/152, na Sunan Al-Kubra cha Imamu Baihaqy 4/175, na kitabu cha Tabakatul-Kubraa cha Ibn Saad 1/248, na kitabu cha Maarifatul-Uluumil-Hadithi cha Haakim 1/197, na tamko la Ibn Saad.

([2]) Kitabu cha Madhehebu ya Wanachuoni 3/61.

([3]) Imekubaliwa na Maimamu wote: Kwenye Sahih Bukhari ni Hadithi ya 1432. Sahih Muslim ni Hadithi 984.

([4]) Imekubaliwa na Maimamu wote: Kwenye Sahih Bukhari ni Hadithi ya 6858. Na kwenye Sahih Muslim ni Hadithi 1337.

([5]) Angalia: Sherehe fupi ya Khalil Makhrashy 2/228 na kuendelea, na sherhe ndogo ya Sheikh Dardiir 1/675 na kuendelea.

([6]) Al-Mudawwanah 1/392.

([7]) Imekubaliwa na Maimamu wote: Kwenye Sahih Bukhari ni Hadithi ya 1437. Na kwenye Sahih Muslim ni Hadithi 985.

([8]) Kitabu cha Mughny Muhtaaj 2/111

([9]) Marejeo yaliyopita 2/119.

([10]) Ni sherehe ya kitabu cha Muntaha Al-Iraadaat cha Bahwaty  1/442: 444.

([11]) Kitabu cha Kashaaf Al-Qinaa 2/254. 2/195 kwa mpangilio.

([12]) Kitabu cha Tabyeen Al-Hakaik. Sherehe ya kanzu dakaik cha Zailai 1/308, kitabu cha Badaii Sanaaii cha Kasany 2/72.

([13]) Kitabu cha Al-Mabsuut 3/107. 108.

([14]) Kitabu cha Musannaf cha Ibn Abu Shaibah 2/398.

([15]) Marejeo yaliyopita.

([16]) Marejeo yaliyopita.

([17]) Kitabu cha Majmuui sherehe ya Al-Muhadhibu cha An-Nawawy 6/112, n a kurejewa na Al-Ishraaf  alaa madhehebu Al-Ulamaa cha Ibn Al-Mundhir 3/80.

([18]) Kitabu cha Majmuu Al-Fatawa, 25/82.

([19]) Rejea kitabu cha Insaaf 3/182.

([20]) Dalili hizi ambazo tutazitaja nyingi zake zimetokana na watafiti wawili waliotajwa, na kwa sifa maalumu utafiti wa mwanachuoni Ahmad Ibn Sidiki Al-Ghumary.

([21]) Sahih Bukhari 2/525 na mfano wake katika sunan Al-Kubraa ya Baihaqy 4/113, na kitabu cha Mughny.

([22]) Kitabu cha Fathul-Baary sherehe ya Sahih Bukhari 3/312, na kwa kuangalia kitabu cha Kharaji cha Yahya Ibn Adam Al-Qarshy, uk. 169 nambari 525, 526.

([23]) Kitabu cha Al-Ummu 2/9.

([24]) Kitabu cha Ibn Abu Shaibah 2/404.

([25]) Marejeo yaliyopita.

([26]) Kitabu cha Tahkiik Al-Aamal, uk. 83.

([27]) Imamu Bukhari Hadithi nambari 1437. Imamu Muslim Hadithi nambari 985. Abu Daud Hadithi nambari 1616. Imemu Tirmidhy Hadithi nambari 673. Imamu An-Nisaai Hadithi nambari 2513. Na Ibn Maja Hadithi nambari 1829 na tamko la Muslim.

([28]) Kitabu cha Tabakatul-Kubraa cha Ibn Saad 1/248. Na Sunani Dar Qutniy 2/152. Na kitabu cha Maarifatul-Uluum Al-Hadithi cha Hakim 1/197. Kitabu cha Sunanil-Kubraa cha Baihaqy 4/175 na tamko la Ibn Saad.

([29]) Kitabu cha Mahsuulu cha Imamu Ar-Razy 5/427 na kitabu cha Al-Ihkaam cha Aamadiy 3/279 sherehe ya kitabu cha Kaukabu Al-Muniir 4/172, 173 na kitabu cha kanuni cha Makray 1/296.

([30]) Kitabu cha Ihkaam Al-Ahkaam 1/75.

([31]) Kitabu cha Fatawa Ramly 2/55, 56.

Share this:

Related Fatwas