Usufi sahihi unaokubalika

Egypt's Dar Al-Ifta

Usufi sahihi unaokubalika

Question

Baadhi ya watu wanadai kwamba Usufi wa kweli zama zake zimepita, na hakuna Usufi sahihi wa kisharia kwa sasa, je! hili ni sahihi?

Answer

Mtume S.A.W. anasema: “Kundi moja katika Umma wangu litaendelea kusimama kwa amri ya Mwenyezi Mungu, hakuwadhuru waliowatenga au waliowageuka, mpaka litakapokuja jambo la Mwenyezi Mungu  ...”[Inakubali na wote], na anasema Mtume S.A.W.: “Umma wangu ni kama mvua, haujulikani heri ipo mwanzo wake au mwisho wake”[Al-Muujam Al-Awsat], hivyo heri ipo katika Umma wa Kiislamu mpaka Siku ya Kiyama, na Usufi wa sasa ni sehemu tu ya mlolongo mrefu, mwanzo wake ni kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W. kisha Masahaba watukufu, kisha Maimamu waliowafuatia Masahaba mpaka kwa kiongozi wa kundi Al-Junaydi, Al-Ghazaly, na Abdul-Qadir Jaylany, kisha baada ya hao Abul-Hassan Al-Shazily, na mwanafunzi wake, Abul-Abbass Al-Mursy, na kuendelea mpaka leo, na mpaka Siku ya Kiyama, ama makosa na kwenda kinyume ni jambo la kawaida lipo katika juhudi za kibinadamu, inaweza kuzuka leo yaliyozuka zamani, jibu ni kuyatatua na kuyanyoosha, si kudai kuwa Usufi zama zake zimepita au kitu kama hicho. 

Share this:

Related Fatwas