Dhana sahihi ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu
Question
Ni ipi Dhana sahihi ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu katika Uislamu?
Answer
Jihadi katika lugha ya Kiarabu ni neno ambalo linamaanisha taabu na kufanya juhudi, kiistilahi Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu ni istilahi iliyo na maana pana, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Na wanao fanya juhudi kwa ajili yetu, Sisi tutawaongoa kwenye njia zetu} [Al-Ankabut:69], wafasiri wa Qur'ani Tukufu wamesema kuwa maana inayokusudiwa hapa ni wale waliofanya juhudi za kuzuia nafsi zao zisizizama katika ladha na matamanio yake kwa ajili ya Mwenyezi Mungu wakiomba uongofu, hivyo wakastahiki kuongoka kwa njia za Mwenyezi Mungu, pia Jihadi ni istilahi inyaotumika kuashiria mapigano dhidi ya maadui kwa lengo la kuwazuia wasiwaudhi Waislamu na kujibu uadui wao na kutetea nafsi na nchi, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu} [At-Tawbah: 41], na aina hii ya Jihadi ni aina yenye masharti na vidhibiti maalumu, kama vile; kuwepo Kiongozi mwenye mamlaka ya kuruhusu kuanza Jihadi, kuwepo umoja wa kiislamu chini ya uongozi maalumu, kuwepo nguvu na ulinzi, kupangwa na kuendeshwa na watawala wanaozingatiwa peke yao, kwa hiyo hali hii imepewa jina la Jihadi Ndogo, ambapo ilisimuliwa kuwa kundi la wapiganaji vita walimjia Mtume (S.A.W.) akawaambia: "Mmekuja vema kutoka Jihadi Ndogo kuelekea Jihadi Kubwa. Wakamwuliza: ni nini Jihadi Kubwa? Akasema: ni kufanya juhudi za kuituliza nafsi na kupambana na matamanio" [imesimuliwa na Baihaqiy katika kitabu cha Az-Zuhd Al-Kabiir]