Msingi wa uhusiano kati ya mtawala ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msingi wa uhusiano kati ya mtawala na watawaliwa

Question

Ni upi msingi wa uhusiano kati ya mtawala na watawaliwa?

Answer

Kwa hakika, uhusiano kati ya mtawala na watawaliwa ndio mkataba uliopitishwa kati ya pande mbili, ambayo ni kutii na kuwajibika kwa upande zote mbili, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Enyi mlio amini! Mt'iini Mwenyezi Mungu, na mt'iini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi} [An-Nisa'a: 59], naye Mtume (S.A.W.) amesema: "Sikilizeni na mtiini, hata mkitawaliwa na mtumwa aliyetoka uhabashi mwenye kichwa cheusi kama zabibu" [Imesimuliwa na Bukhary], kwa upande wa mtawala anapaswa kuwatawala raia wake kwa mujibu wa maslahi ya umma na makusudio ya Sheria akihakikisha uadilifu na kuondoa udhalimu, kuilinda dini, kutunza amani na utulivu wa jamii kutokana na  hatari yoyote ya ndani na nje, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Ewe Daudi! Hakika Sisi tumekufanya wewe uwe Khalifa katika nchi. Basi wahukumu watu kwa haki, wala usifuate matamanio} [Saad:26], Uislamu haukufanya uadilifu wa mtawala uwe kwa sharti la kutiiwa na raia, ingekuwa hivyo mambo ya umma yasingekuwa ipasavyo, kwa hiyo Mtume (S.A.W.) amesema akiwausia umma wake: "yeyote anayepatwa na adha kutoka kwa mtawala wake, basi asubiri, kwani anayejitenga na jamaa kidogo, akifa hali ya kuwa katika hali hii, basi amekufa kijahiliya" [Imekubaliwa na wote]

Share this:

Related Fatwas