Yanayosemwa wakati wa kuchanganyiki...

Egypt's Dar Al-Ifta

Yanayosemwa wakati wa kuchanganyikiwa.

Question

Ni yapi mwanadamu anaweza kusema wakati wa kutokewa na hali ya kuchanganyikiwa kutokana na hali ya tetemeko na mfano wake?

Answer

Imepokewa katika Sunna Takatifu kuwa mwanadamu anapofikwa na kile kinachomchanganya aseme:

 “Huwa Allah, Allahu Rabby laa shariika lau: Yeye ndiye Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu ndio Mola wangu hana mshirika”.

Hadithi hii inaonesha Sunna ya kuleta duwa wakati mwanadamu anapofikwa na jambo miongoni mwa majanga asilia na mengineyo, vile vile Wanachuoni wamependekeza kuswali wakati wa kutokea jambo la mfano huu, kutokana na yaliyomo kwenye Swala ni pamoja na kufikiwa hali utulivuu. Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema:

{Hakika mwanadamu ameumbwa na papara * Inapo mgusa shari hupapatika * Na inapo mgusa kheri huizuilia * Isipokuwa wanao swali * Ambao wanadumisha swala zao} Al-Maariji: 19 – 23.

Share this:

Related Fatwas