Nuksi za siku na idadi
Question
Nini hukumu ya kutarajia mabaya wakati wa kuona idadi maalumu au ujio wa siku maalumu au tukio katika kile kinachoitwa “nuksi”?
Answer
Nuksi za nambari, siku, n.k zimekatazwa katika Sharia. Kwa sababu mambo hutokea kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, na mambo haya hayahusiani na mema anayopata mtu au mabaya yanayompata. Kisheria nuksi na uchuro zimekatazwa kwa ujumla, kwani ni tabia ya kijahiliya. Katazo la nuksi limepokelewa kutoka kwa Mtume pia liliripotiwa kutoka nyakati na miezi fulani kuhusu hilo. Kama ilivyopokelewa katika “Al-Sahihayn” kutoka kwa Abu Hurairah, (R.A), kutoka kwa Mtume, (S.A.W), ambaye amesema: “Hakuna maambukizo, wala Mfungo Tano, wala bundi (hata zama zetu zinaamini nuksi kumuona au kumsikia bundi, au kumuona paka mweusi).” Sababu ya makatazo haya ni yale yaliyo katika nuksi na uchuro kutokana na dhana mbaya kwa Mwenyezi Mungu, na kuchelewesha nia ya mtu katika kutenda, kama vile inavyovuruga moyo kwa wasiwasi na udanganyifu.
Na Mwenyezi Mungu pekee ndiye Anayejua Zaidi.