Dhana ya kuwawezesha Waislamu
Question
Ni ipi dhana sahihi ya kuwawezesha Waisalmu kwa mujibu wa Qur`ani na Sunna, na vipi makundi ya kigaidi walivyopotosha dhana hii?
Answer
Kwa hakika dhana ya kuwawezesha Waislamu katika Qur`ani na Sunna za Mtume inarejelea maana kadhaa zinazotumika kuashiria malengo yake; kama vile; kuwawezesha waumini kwa kuwapa madaraka kwa ajili ya kuwasiadia kusimamisha dini jambo ambalo ni lengo kuu la dhana hiyo, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: "Wale ambao tukiwapa madaraka katika nchi husimamisha Swala, na wakatoa Zaka, na wakaamrisha mema, na wakakataza mabaya" [Al-Hajj: 41], au kuidhalilisha ardhi na yaliyomo ndani yake kuhudumia wanadamu kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu: "Na hakika tumekuwekeni katika ardhi, na tumekujaalieni humo njia za kupatia maisha. Ni kuchache kushukuru kwenu" [Al-Araaf: 10], au kumpa utawala na madaraka kama ilivyo katika kauli yake Mwenyezi Mungu: "Sisi tulimtilia nguvu katika ardhi na tukampa njia za kila kitu" [Al-Kahf: 84], kwa jumla maana za kuwawezesha na kuwapa madaraka zimefungamana na uwezo wa Mwenyezi Mungu na msaada waka kwa waja wake, maana yeye ndiye mwenye uwezo wa kuwawezesha waja wake Apendavyo, kwa hiyo kuwawezesha wanadamu katika ardhi ni sifa mojawapo sifa za pekee za Mwenyezi Mungu (S.W.), na hivyo ndivyo dhana sahihi lakini makundi ya kigaidi na wenye fikra potofu wameibana dhana hii wakaihusisha kwa kuwawezesha viongozi wao na kujipatia utawala na udhibiti wa mambo ya kisiasa, wakidai kuwa hali hiyo inatokana na uwezo wao na nguvu zao si uwezo wa Mwenyezi Mungu, wakaipora dhana hii na kuigeuza kulingana na fikra zao na maslahi yao ya kisiasa wakipotosha dhana kikamilifu.