Taswira ya Uislamu katika nchi za Kimagharibi
Question
Ni nini athari za jinai za makundi ya kigaidi na wenye msimamo mkali juu ya taswira ya Uislamu katika nchi za Kimagharibi?
Answer
Kwa kweli, juhudi za kuboresha taswira ya Uislamu ni jambo linalotakikana katika Sharia, kwa kuwa hutokana na matini za Sharia yenyewe, jambo hilo hufanywa kwa kufuata mbinu na namna maalumu iliyo thabiti na imara, mahusiano ya kimataifa yanapaswa kutegemea misingi sahihi isiyo na hofu, hivyo taswira iwe sahihi na ya kikweli kwa mujibu wa matini ya Qur`ani na Sunna.
Lakini wenye msimamo mkali na magaidi hawajali vidhibiti hivyo, bali wanakwenda kinyume na uongofu wa Mtume (S.A.W.), ambapo wanafanya uhalifu mwingi kama vile; kutuma wapiganaji wao wakijificha miongoni mwa wakimbizi ambao wanaruhusiwa kuingia nchi fulani na kukaa kwa muda, wangeelewa vizuri wasingefanya hivyo, bali huwa wanatakiwa kutangaza kuwa hawatashambulia nchi ambazo zinawapokea ndugu zao Waislamu waliozikimbilia, kwa kufuata muongozo wa Mtume (S.A.W.) alipofanya hivyo kwa watu wa mwanamke ambaye aliwanywesha Swahaba zake maji kuondoa kiu kama ilivyokuja katika Bukhar: "Baada ya tukio hilo Waislamu walikuwa wakiwavamia washirikina waliomzunguka na hawakuvamia kaumu ya yule mwanamke, siku moja mwanamke akawaambia watu wake: naona kuwa Waislamu hawawapigeni kimakusudi, je, mnaonaje kujiunga na Uislamu? Wakamjibu wakajiunga na Uislamu"