Kazi ya Wanachuoni

Egypt's Dar Al-Ifta

Kazi ya Wanachuoni

Question

Je, inapaswa kuwauliza Wanachuoni katika masuala yote, ama inawezekana kwa mtu ajiulize na kufuata aliyoyasoma?

Answer

Kwa kweli Wanachuoni ni wale watu ambao Mwenyezi Mungu Amewafanya walinzi wa hukumu za dini yake, kwa hiyo wakapaswa kuwaelimisha watu na kuwaonya kutoka shari wachukue tahadhari zao hasa kutokana na wale ambao wanachocheza fitina, maovu na ukafiri katika jamii, zipo dalili nyingi za kuthibitisha umuhimu wa Wanachuoni katika jamii, kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na waliopewa Kitabu kuwa: Lazima mtawabainishia watu, wala hamtokificha, walikitupa nyuma ya migongo yao, na wakanunua kwacho thamani duni. Basi ni kiovu hichowalicho nunua} [A'al-Imran: 187]

Imamu Al-Qurtuby amesema kuwa Aya hii imeteremka kwa kuashiria kila aliyepata elimu kutoka katika Kitabu, atoe elimu hiyo, na kutahadharisha kuficha elimu kwani ni sababu ya kuangamizwa kwa anayefanya hivyo. Naye Mohammed bin Ka'ab amesema: haijuzu kwa mwenye elimu kukaa kimya bila ya kutoa elimu aliyo nayo, wala haijuzu kwa asiye na elimu kukaa kimya bila ya kutafuta njia ya kujipatia elimu, Abu Hurairah amesema: Kwa kweli Mwenyezi Mungu Asingaliwaagiza wenye elimu kutoa elimu yao nisingaliwahadithieni kitu, akasoma Aya hii: {Na pale Mwenyezi Mungu alipo fungamana na waliopewa Kitabu…}.

Kwa hiyo, inapaswa kuzingatia maoni ya Wanachuoni katika masuala nyeti ya umma, kwani Wanachuoni wanatarajiwa kuwa waaminifu na wenye mamlaka ya kuamua hatima ya umma nao pia ni watu wa ujuzi waliotajwa katika kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Basi waulizeni wenye ukumbusho kama nyinyi hamjui} [An-Nahl: 43], Mwanachuoni mzima ni yule mwenye elimu ya kuelewa sharia kikamilifu na pia kuelewa hali halisi ya watu pamoja na hali ya desturi na mila zao.

Share this:

Related Fatwas