Mitandao ya Elektroniki
Question
Ipi nafasi ya kurasa za mawasiliano ya kijamii katika kusambaza misimamo mikali na ugaidi?
Answer
Mtandao umekuwa ndio njia kuu na ya kimantiki kwa vikundi vya misimamo mikali ili kufanya kazi ya kupambana na kushindwa kwao mfululizo kwa upande wa kijeshi na kiusalama. Abu Mus’adu Sury mapema kabisa ameweka mikono yake kwenye muundo huo ndani ya kitabu chake: “Wito wa mapambano ya Kiislamu” akielezea umuhimu wa kuwa na mikakati mbadala, akasema ndani ya kitabu chake kilichotajwa hapo juu baada ya kukiri kwake kufeli kwa zoezi la kutoa mafunzo ya kijeshi moja kwa moja, na kuelezea sababu za kuelekea kwenye “Jihadi binafsi” ni kufeli kwa mfumo wa kazi za vikundi kupitia mashambulizi ya kiusalama kimataifa na muungano wa kijimbo na kimataifa, na vikundi kushindwa kuwaleta vijana wa Umma ambao wanataka kutekeleza jihadi na kupambana kwa kushiriki kufanya chochote bila ya kulazimishwa kufuata kujinasibisha na kundi kuu, na wigo wa kupatikana adui na malengo yake tofauti na kupatikana kwake katika maeneo mengi yaliyo magumu kutekeleza mapigano kama ilivyo ngumu kuanzisha makundi makuu, na kudondoka kwa fikra ya vikundi na kupambana na adui, ikiwa ni matokeo ya adui kutumia mkakati madhubuti wa anga kwa mashambulizi ya makombora ya maangamizi na mishale ya anga yenye kuelekezwa kwa kutumia satalaiti ambazo zinadhibiti eneo la ardhi, bali na kuona kilichopo chini ya ardhi kwa kutumia teknolojia ya juu, hilo ni jambo ambalo ni wajibu kulikiri na kuliwekea mipango ya kupambana nalo.
Hivyo mtandao wa kielektroniki ndio uwokozi ambao unalinda kubakia kwa vikundi hivyo vya misimamo mikali na kueneza imani zake, pamoja na kutoka mafunzo ya kijeshi kwa idadi kubwa ya watu wa misimamo mikali ili vitisho vyoa na vitendo vyao viendelee kubakia.