Masharti ya kutoa Fatwa

Egypt's Dar Al-Ifta

Masharti ya kutoa Fatwa

Question

Ni nini masharti ya kutoa Fatwa katika Uislamu?

Answer

Kwa hakika Fatwa ni kutoa habari au maelezo yanayohusu hukumu ya kisharia kuhusu tukio au hali fulani, kwa kuwa jukumu la mtoa Fatwa ni kubwa na muhimu, wataalamu wakaweka masharti na vigezo maalumu yanayopaswa kupatikana kwa anayeshughulikia kutoa Fatwa, ambapo anapaswa kuwa na elimu ya kutosha kuhusu elimu ya Fiqhi na Vyanzo vyake, akielewa maoni ya wataalamu wa Fiqhi na madhehebu yao, anatambua hali halisi ya watu na kuwa na uwezo wa kutofautisha kati ya yaliyo thabiti na yanayobadilika, mwenye kujua mambo yaliyo muhimu zaidi (vipaumbile) na namna za kuchukua hukumu za kifiqhi kutokana na dalili za kisharia.

Kutoa Fatwa pasipo na elimu ni jambo lililokatazwa kisharia kwani ni kusema uongo juu ya Mweneyzi Mungu na Mtume wake (S.A.W.) na kupotosha fikra za watu.

Mwishoni, tunasisitiza kuwa katika zama kama hii tuliyo nayo inapaswa kuongeza sharti ya kuwa na elimu hasa na mbinu iliyo sahihi ambayo humsaidia mtu kupata elimu kutoka taasisi husika za kutoa Fatwa, yaani; mtoa Fatwa awe anatambulika kwa taasisi rasmi za kiislamu za kutoa Fatwa.

Share this:

Related Fatwas