Fatwa na Da'awa
Question
Ni nini tofauti kati ya Fatwa na Da'awa?
Answer
Tofauti zilizopo kati ya Fatwa na Da'awa ni nyingi ikiwemo kuwa shughuli za Da'awa hutegemea kufikisha ujumbe, kutumia mtindo wa hotuba kwa watu wote kwa lengo la kuwaelemisha misingi ya dini, miamala na tabia, hali ya kuwa Fatwa ni kazi maalumu inayohusiana na matukio na hali maalumu, ambapo hukumu ya sharia hutakiwa kutangazwa. Mufti huenda kuchukua nafasi ya mlinganiaji na kuwalingania watu kwa dini ya Mwenyezi Mungu, hali ya kuwa mlinganiaji hana mamlaka ya kutoa Fatwa kwa watu isipokuwa baada ya kuandaliwa kwa shughuli hiyo muhimu kupitia kwa kupata uzoefu na sifa za Mufti, kwani kutoa Fatwa ni kazi maalumu inayotegemea jitihada na uzoefu kulingana na mbinu na masharti hasa, pia huenda msomaji kuwa na uwezo wa kutoa mawaidha lakini aliye na sifa za Mufti anaweza kuwa na mapungufu fulani kuhusu kutoa hotuba mbele ya watu, vile vile, Da`awa huasisiwa mahojiano na mjadala unaofaa, hali ya kuwa Fatwa haizingatii misingi hiyo kwa kuwa mwomba Fatwa huwa anakusudia kuelewa hukumu ya kisheria si kujadiliana na mtoa Fatwa, vile vile, Fatwa na Da'awa zinashirikiana kuwa zote zinahitaji kuangalia na kujali hali ya muuliza kwa mujibu wa wakati, mahali na mabadiliko.
Mlinganiaji hujali zaidi mawaidha na kutuliza nyoyo za watu walengwa wake, lakini mufti hujali zaidi kuwaelemisha Waislamu namna sahihi ya kutekeleza ibada, pamoja na kuwaelekeza kwenye miamala mizuri akiwafafanulia hukumu za kisharia.