Kumshawishi mwenye kuswali
Question
Ipi hukumu ya kumshawishi mwenye kuswali wakati wa swala yake kama vile kumchekesha na mfano wa hayo?
Answer
Kumshawishi mwenye kuswali wakati wa kuswali kwake kama vile kumchekesha na yanayofanana na hayo ni haramu Kisharia, na mwenye kufanya hivyo anapata dhambi.
Swala ni nguzo ya dini na msingi wake, yenyewe ina utakatifu wake na utukufu wake, nayo ni mazungumzo na minong’ono inayopatikana kati ya mja na Mola wake Mtukufu, ni lazima kwa mja kuwa na hali ya unyenyekevu ambao unasimama kwenye minong’ono hii na mazungumzo hayo, ili kuwa miongoni mwa wale walioambiwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Hakika wamefanikiwa Waumini * Ambao ni wanyenyekevu katika Sala zao} Al-Muuminun: 1, 2.
Hivyo Uislamu umezuia kila kitu kinacholeta ushawishi kwa mwenye kuswali na kuathiri unyenyekevu wake, ni sawa sawa ndani ya swala au nje ya swala, wala haifai kwa Muislamu kuvamia utukufu wa ibada ya swala kwa kumchekesha mwenye kuswali au mfano wa hayo, ikiwemo ndani yake dhambi kubwa, Wanachuoni hawajatenganisha kati ya ushawishi kwa mwenye kuswali kwa utiifu au kwa maasi, wakaelezea kuzuiliwa kwake na uharamu wake ikiwa kwa utiifu, akafanya kama vile kumchekesha mwenye kuswali ni haramu zaidi.