Kutumia manyoya ya wanyama kuzalisha bidhaa.
Question
Ipi hukumu ya kutumia matandiko yaliyotengenezwa na manyoya ya wanyama?
Answer
Inafaa kutumia manyoya asili yanayochukuliwa kwa mnyama, kwa matumizi yote na kutengenezea vitu mbalimbali kwa manyoya hayo, na hilo ni kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na Mwenyezi Mungu amekujalieni majumba yenu yawe ni maskani yenu, na amekujalieni kutokana na ngozi za wanyama nyumba mnazo ziona nyepesi wakati wa safari zenu na wakati wa kutua kwenu. Na kutokana na sufi zao na manyoya yao na nywele zao mnafanya matandiko na mapambo ya kutumia kwa muda} An-Nahli: 80.
Mwenyezi Mungu Anajua zaidi.