Kuchafua maji.
Question
Ipi hukumu ya kuchafua maji ya mito na mifereji?
Answer
Sharia Tukufu imeamrisha kulinda maji kwa sababu ndio asili ya uhai, yamepokewa maandiko mengi juu ya hilo, kuchafua maji ya mito au mifereji ni kukiuka amri hizi, hukumu ya Kisharia katika hilo ni “Haramu” ambapo kushambulia maji kwa kuyachafua ni kushambulia haki za watu wote, kutokana na kuwa watu wote wanashirikiana kwenye matumizi ya maji, na katika kuyachafua ni kuongeza gharama kwa serikali katika kurekebisha uharibifu huu ili maji yazungushwe tena na kusafishwa ili yawe salama kwa matumizi.