Kuweka wazi miguu wakati wa Swala kwa mwanamke
Question
Ni ipi hukumu ya mwanamke kuweka wazi miguu yake wakati wa swala?
Answer
Wakati wa Swala ni lazima mwanamke awe na dhamira ya kujifunika mwili wake wote isipokuwa uso na mikono, ikiwa kufunika miguu yake kunaweza kuwa ni tabu au mazingira ya maisha hayastahiki, basi afuate wale Wanachuoni wa Fiqhi waliohalalishia kufunua miguu, na Swala zake ni sahihi.