Hukumu ya kumswalia Mtume (S.A.W.) ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Hukumu ya kumswalia Mtume (S.A.W.) baada ya adhana

Question

Ni ipi hukumu ya kumswalia Mtume (S.A.W.) baada ya adhana?

Answer

Kumswalia Mtume (S.A.W.) baada ya adhana ni jambo ambalo waadhini wengi wa Swala  wamelizoea sana, na lililo sahihi ni kuwaacha watu waendelee na waliyoyazoea na kuyapenda zaidi (sharti liwe sahihi au mubaha), basi wale waliozoea kumswalia Mtume baada ya adhana haina shida kuendelea na hilo, na wale waliozoea kutomswalia Mtume baada ya adhana hawalaumiwi, kwa yote, maneno ya adhana yanajulikana na haiwezekani kuchanganyika na maneno mengine, na la msingi hapa ni kuridhika kwa moyo wa Muislamu, bila ya kusababisha kutofautiana wala mfarakano kati ya watu.

Wala haijuzu kuwa suala kama hili liwe sababu ya kuchochea fitina na mfarakano baina ya Waislamu, bali tunatakiwa kuwajibika kwa adabu za kutofautiana kama walivyokuwa wakifanya wahenga wetu wema ambao walikuwa wanatofautiana katika masuala ya kifiqhi wakiwa wakiheshimiana na kupendana.

Share this:

Related Fatwas