Hukumu ya kubadilisha upande wa kutumia michango
Question
Je, inaruhusiwa kubadilisha upande wa kutumia michango?
Answer
Kimsingi haijuzu wala haikubaliki kubadilisha upande wa kutumia michango kwa pande tofauti na zilizoainishwa na mtoaji michango ila baada ya kuomba ruhusa kutoka kwake, ambapo asasi au jumuiya ya kugawa sadaka michango ni wakili ya mtoaji sadaka hizo haina haki ya kubadilisha pande za matumizi ya sadaka hizo kwa mujibu wa uwakala huu, kwa hiyo michango iliyotolewa na mtu kwa ajili ya kufikishwa mahali fulani, basi hairuhusiwi kugeuzwa kwa upande au mahali pengine isipokwa kwa idhini ya wachangiaji na kuomba ruhusa yao ya kufanya hivyo, kwa hiyo tunatoa shauri la:
Kwamba wito wa kukusanya michango waelezee uwezekano wa kubadilisha pande za matumizi kulingana na mabadiliko na mahitaji.
Kwamba taasisi za kukusanya michango na misaada ziwe na uhuru wa kutosha kuchagua pande zinazohitaji zaidi misaada hiyo na kuwa na haki ya kufanya la kufaa zaidi.