Hatua za kuchukua makaburi yanapojaa
Question
Ipi hukumu ya makaburi yanapojaa maiti, na nini tunapasa kufanya?
Answer
Katika hali ya dharura na mahitaji- kama ilivyo katika makaburi mengi- kunajuzu kujenga gorofa ya pili ya makaburi kwa kukusanya mifupa iliyopo.
Pia kunajuzu kufunika maiti ya zamani kwa matofali au mawe kwa namna yasiguse mwili wake, kishwa jiwe hilo linafunikwa kwa mchanga na juu yake anazikwa maiti mwingine.
-pia kunajuzu kutengeneza eneo la kukusanya mifupa ya maiti kisha kuizika tena katika makaburi hayo ikiwa kuna ulazima wa hilo.
Na yote haya kwa sharti la kuchunga hatua za kuheshimu maiti au mabaki ya maiti, kwa sababu heshima ya mwanadamu akiwa maiti ni kama heshima yake akiwa hai.