Kukusanya Swala
Question
Je! Kunajuzu kukusanya Swala kwa udhuru?
Answer
Asili ni kutekeleza Swala za faradhi katika wakati wake, nayo ni miongoni mwa ibada azipendazo zaidi Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Na ruhusa ya kukusanya kati ya Swala mbili za Adhuhuri na Alasiri, Magharibi na Isha kwa sababu ya maradhi au safari ni jambo linalojuzu kisharia kwa makubaliano ya wanazuoni walio wengi.
Na kukusanya kwa udhuru usiokuwa huo kama kukidhi haja au kushughulika kwa kazi na mengineyo, kunajuzu kisharia kwa sharti kwamba hilo lisiwe ndio mazoea, pamoja na kuchunga kunuia kukusanya Swala mbili katika wakati wa Swala ya kwanza akitaka kukusanya kwa kuchelewesha, na wakati wa kuhirimia Swala ya kwanza au katikati yake akitaka kukusanya kwa kutanguliza, na kutokuwa na kitambo kirefu kati ya Swala mbili.