Twahara ya mwenye kisalisali cha mk...

Egypt's Dar Al-Ifta

Twahara ya mwenye kisalisali cha mkojo na Swala yake

Question

Muulizaji hutokwa na vimkojo baada ya kutawadha na katika Swala, na anauliza: Je! Atawadhe tena na Swala? Na akisoma Qur`ani nje ya Swala na akatokwa na vimkojo, Je! Aendelee kusoma?

Answer

Twahara ni sharti katika sharti za kusihi Swala, lau ukitoka mkojo japo tone moja kwa mtu mzima, udhu umetenguka; kwa Hadithi ya Abu Hurayra R.A. amesema: amesema Mtume S.A.W.: “Mwenyezi Mungu hakubali Swala ya mmoja atakapojisaidia mpaka atawadhe” (ameipokea Albukhry).

Lakini ikiwa mtu ni mgonjwa, na anatokwa na mkojo na unamtoka bila ya kuweza kuudhibiti; basi atawaze mara moja wala asifikirie vimkojo vinavyomtoka bila ya kuweza kuvidhibiti, na Swala yake na kisomo chake vinazingatiwa kuwa ni sahihi pamoja na kuwepo udhuru huu, mpaka udhu wake utakapo tengenguka kwa kitu kingine kisichokuwa hiki.

Share this:

Related Fatwas