Ughali wa mahari na athari zake.

Egypt's Dar Al-Ifta

Ughali wa mahari na athari zake.

Question

Ipi hukumu ya Kisharia katika ughali wa mahari na athari zake?

Answer

Ughali katika mahari si katika Sunna ya Uislamu, kwa sababu asili ya lengo la kuoa ni kulinda tupu kwa mvulana na msichana, na Mtume S.A.W amesema:

“Wanawake wenye baraka zaidi ni wale waliolewa kwa mahari nyepesi zaidi”.

Kilichokuwa cha lazima ni kutofanya ghali mahari, na mzazi wa mtoto wa kike kufanya wepesi kwa binti yake kuoelewa pindi akipata mume mwema, ili kulinda vijana wetu wa kiume na wakike kujiingiza kwenye maasi, kwani Mtume S.A.W ametupa nasaha kwa kauli yake:

“Pindi anapokujieni mtu mnayemridhia dini yake na tabia zake basi muozesheni, ikiwa hamkufanya itakuwa ni fitina katika ardhi na uharibifu mkubwa”.

Share this:

Related Fatwas