Kufuatilia aibu
Question
Ipi hukumu ya kufuatilia aibu na kukiuka yaliyoharamu na kuyachapisha?
Answer
Baadhi ya watu huvamia maisha binafsi ya watu wengine pasi ya wao kufahamu, na kuelezea kwa njia mbalimbali yaliyofichika, mfano:
Kuwapiga picha kwa kutumia vifaa vya teknolojia ya sasa.
Kuchunguza kwa macho
Kuiba kwa kusikiliza.
Au nyingi zingine zisizokuwa hizo.
Na kurusha kwenye majukwaa ya vyombo vya habari vya kidijitali, au mitandao ya mawasiliano ya kijamii, hayo huzingatiwa ni kufuatilia aibu zinazopaswa kufichwa, na ukiukaji unaopaswa kulindwa, na fedheha na mambo ya aibu yanayopaswa kustiriwa, vyote hivyo ni vitendo vichafu kwa watu wenye akili, na haramu Kisharia, yasiyotakiwa kisheria, yanayopelekea dhambi na adhabu kali, mwanadamu anapaswa kujiweka mbali na kuingia kwenye ukiukaji huu, ili kulinda nafsi yake na kulinda jamii yake na nchi yake.