Kumwombea dua marehemu
Question
Je, kumwombea dua marehemu huwa kwa sauti au kisiri siri?
Answer
Hakika dua huweza kuwa kwa sauti au kisiri siri na kwa tamko lolote kama Mwenyezi Mungu Anavyomwongoza mwombaji, na kubana ile namna iliyopanuliwa na Mwenyezi Mungu (S.W.) na Mtume wake (S.A.W.) ni jambo linalochukiwa, pia kuzozana kuhusu suala hili hakukubaliki hata kidogo na Mwenyezi Mungu (S.W.) na Mtume wake (S.A.W.), ambapo Mtume (S.A.W.) alikataza kugombana kati ya waislamu, akabainisha kuwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Akinyamazia kitu bila ya kutangaza kulikataa, basi huwa kwa maslahi na kuhurumia waislamu, Mtume (S.A.W.) alisema: “Hakika Mwenyezi Mungu Alifaradhisha mambo, basi msiyapoteza, Akaharamisha mambo, basi msiyakiuke, Akaweka adhabu, basi msizikaribia, Akanyamazia mambo kwa kuwahurumia si kwa kuyasahau, basi msiyapelelezia” imesimuliwa na Al-Dar Qutny.
Kwa ujumla, dua na kumtaja Mwenyezi Mungu kwa pamoja huwa karibu zaidi kukubaliwa, kuiamsha nyoyo na kuchocheza juhudi na hamu, kuzidisha unyenyekevu mbele ya Mwenyezi Mungu, hasa wakati wa kuwa na mawaidha, naye Mtume (S.A.W.) alisema: “Baraka na uwezo wa Mwenyezi Mungu iko pamoja na jamaa” imesimuliwa na Al-Tirmidhy kutoka kwa Ibnu Abbas (R.A.)