Uzuri wa kuwa na idadi kubwa ya wanaosalia jeneza
Question
Je, kuna fadhila yoyote kuwa na idadi kubwa ya wanaosalia Jeneza?
Answer
Kuwa na idadi kubwa ya waislamu wanaosalia Jeneza huwa ni sababu ya kuomba shafa’a na maghufiraha kwa marehemu, na pia malipo mema kwa wanaosali, imesimuliwa kutoka kwa Ibnu Abbas (R.A.) kuwa alisema: nimemsikia Mtume (S.A.W.) anasema: “Mwislamu yeyote afariki akasaliwa na waislamu arobaini wanaomwamini Mwenyezi Mungu pekee, huwa anastahiki shafaa na dua yao” imesimuliwa na Muslim. Na kutoka kwa Bi. Asha (R.A.) kuwa Mtume (S.A.W.) alisema: “Mwislamu yeyote akifariki akasaliwa na umati wa waislamu walio chini ya mia moja na kumwombea dua ya msamaha na maghufirah, basi Mwenyezi Mungu Anakubali dua yao kwake” imesimuliwa na Ahmed.