Hukumu ya kutoa Zaka kukata ushuru kutokana na faida
Question
Je, ni wakati gani wa kutoa Zaka juu ya fedha za biashara na ni ipi hukumu ya kukata ushuru kutokana na faida?
Answer
Imefafanuliwa kwa mujibu wa Sharia kwamba mtu anayefanya biashara lazima aweke hesabu ya bidhaa zake, fedha na faida, na kutoa zaka juu ya vyote hivyo. Kwa sharti la kwamba mwaka mmoja umepita kwa vyote, na ushuru wa serikali unaochukuliwa kwa faida haukatwi kutokana nayo. Kwa sababu haki ya serikali haizuii haki ya Mwenyezi Mungu, bali ushuru hukatwa katika pesa kabla ya kuhesabu Zaka.