Ushabiki wa kidini na misimamo mikali
Question
Vipi Sharia tukufu inaonya dhidi ya ushabiki na misimamo mikali ya kidini?
Answer
Sharia tukufu ilikataza kupita kiasi, ushabiki, na misimamo mikali katika dini. Hali ambayo hupelekea kueneza chuki na maudhi miongoni mwa watu, hudhoofisha amani na mafungamano ya kijamii, na huvuruga usalama na utulivu wa mataifa. Njia ya Uislamu katika kulingania kwa Mwenyezi Mungu inategemea kuwa mwema kwa wengine, na kutomdhalilisha yule anayeipinga. ikiwa anatofautiana katika madhehebu, imani, au dini. Ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: “Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walioongoka” [An-Nahl: 125].