Kutotii wazazi

Egypt's Dar Al-Ifta

Kutotii wazazi

Question

Ni ipi adhabu ya kutotii wazazi?

Answer

Mwenyezi Mungu amekataza kuwaasi wazazi, na akaifanya adhabu yake kuwa kali na mbaya. duniani kuna adhabu kabla ya Akhera. Imepokelewa kutoka kwa Anas Ibn Malik, (R.A), kwamba Mtume, (S.AW), amesema: “Kuna mambo mawili ambayo adhabu yake inaharakishwa katika dunia: uadui na uasi. ” Imepokelewa kutoka kwa Al-Hakim.

Mtume (S.A.W), aliufanya uasi kwa wazazi kuwa kizuizi cha kuingia Peponi. Imepokelewa kutoka kwa Ibn Umar, (R.A), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W) amesema: “Watu watatu Allah hatawatazama Siku ya Kiama: asiyewaheshimu wazazi wake, mwanamke anayejifananisha na mwanamume, na dayuuthi, (ni yule ambaye anakubali uovu kwa mkewe).

Na watu watatu hawatoingia Peponi: mwenye kuwaasi wazazi wake, na mwenye kulewa  pombe, na mwenye kusema sana kwa kile anachotoa”. Imepokelewa kutoka kwa (Al-Nasa’i).

Share this:

Related Fatwas