Kujiombea mabaya mwenyewe mtoto na mali.
Question
Ipi hukumu ya kujiombea mabaya kwako kwa mtoto na mali?
Answer
Mtume S.A.W amekataza mwanadamu kujiombea mabaya yeye mwenyewe au kwa mtoto wake au mali yake au mtumishi wake, kutoka kwa Jabiri Ibn Abdillah R.A amesema: Mtume S.A.W amesema:
“Wala msijiombee mabaya wenyewe, wala kwa watoto wenu, wala kwa watumishi wenu, wala kwenye mali zenu, isijeikaenda sambamba kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na saa ya kukubaliwa maombi mkajibiwa”. Imepokewa na Imamu Muslimu.