Ukiritimba na matumizi mabaya

Egypt's Dar Al-Ifta

Ukiritimba na matumizi mabaya

Question

Ipi hukumu ya ukiritimba na kuwapotosha wauzaji katika bei za bidhaa na kutumia vibaya hali za kiuchumi?

Answer

Wafanya biashara ambao hufanya ukiritimba kwenye bidhaa au wanaziuza kwa bei ya juu zaidi ya kawaida yake wakitumia vibaya hali za kiuchumi na kubadilika badilika kwake Kisharia hao ni wenye dhambi, na wanunuzi wanapaswa kutowasaidia hao kwenye hilo, hivyo mnunuzi asinunue isipokuwa kile anachokihitaji kwake. 

Share this:

Related Fatwas