Qiyasi “Ulinganishi” katika Ibada
Question
Qiyasi “Ulinganishi” katika Ibada
Answer
Katika kulinganisha ibada na yanayotokana na huko kulinganisha ni moja ya masuala muhimu kati ya Wanafiqhi na watu wa Usuul-Din, huathiri hali ya mtafiti wa masuala ambayo hutokea na kuhitajika kulinganisha na kuzingatia au kupuuza na kuondoa.
Ndani ya kipindi cha hivi karibuni kumekuwa na matumizi makubwa ya kanuni ya (Hakuna kulinganisha katika Ibada) kabisa, na si sehemu yake, na huitoa kwenye wigo wa Kifiqhi na Kiusuul ambapo Wanachuoni wamezungumzia, kutokana na hayo imekuwa ni lazima kuweka wazi msimamo wa Wanachuoni wa Sharia ya Kiislamu kwenye suala hili, kwanza kwa kupande wa Usuul, pili kwa upande wa Fiqhi.
Tutazungumzia maudhui hii kupitia uchambuzi ufuatao:
Uchambuzi katika maana ya Qiyasi na ibada kwa upande wa lugha na kimsamiati:
Qiyasi: Katika lugha huitwa, Makadirio, kwa maana hukadiriwa kitu kwa kitu kingine, kama vile kusema: “Nimepima nguo kwa dhiraa moja”, pia huitwa: Usawa kati ya vitu viwili, ni sawa sawa usawa ukiwa wa kimaana, kama wanavyosema: “Fulani halingani na fulani”, au usawa wa kihisia, kama wanavyosema: “Nimepima nguo kwa nguo” ([1]).
Kwa upande wa kimsamiati: “Kuthibiti hukumu inayofahamika kama inavyofahamika kwa mwingine kwa kushirikiana katika sababu na hukumu kwa mthibitishaji” ([2]).
Ibada: Kwa upande wa lugha ni utiifu, kufuata, kunyenyekea, Ibn Al-Athiir amesema: “Maana ya ibada katika lugha: Utiifu na unyenyekevu” ([3]).
Na katika msamiati: Sheikh Al-Islaami Zakaria Al-Ansaary R.A amesema: “Ibada ni njia ya kuabudia kwa sharti la kuwa na nia na kumfahamu mwabudiwa” ([4]).
Uchambuzi: Tofauti wa Ibada Ukaribu Utiifu na Kuabudu:
Wanachuoni wametenganisha kati ya ibada ukaribu utiifu na kuabudu, Ibn Aabideen R.A anasema akimnukuu Sheikh Zakaria Al-Ansaary R.A na kuongeza ufafanuzi na sherehe:
Utiifu: “Kitendo kinachopelekea kupata thawabu, kinasimama kwa nia au bila ya nia, hufahamika mtendaji wake au hafahamiki.
Ukaribu: “Kitendo kinachopelekea kupata thawabu baada ya kumfahamu anayekaribiwa, hata kama hakutakuwa na nia.
Ibada: “Mtendaji wake hupata thawabu, na hutekelezwa kwa nia, mfano: Swala tano, Funga, Zaka, Hija - na mfano wa kila kinachotekelezwa kwa nia – ikiwa kujiweka karibu kutii na kuabudu. Kusoma Qur`ani, Waqfu, kuacha huru mtumwa, kutoa sadaka – na mfano wake miongoni mwa zisizosimama kwa nia – ikiwa kujiweka karibu na utiifu, si kwa ibada. Na mtazamo unaopelekea kumfahamu Mwenyezi Mungu ni Utiifu, si kujiweka karibu wala Ibada” ([5]).
Ikiwa tutatumia neno “Ibada” lenyewe ndani yake kinaingia kila kinachoitwa “Misingi ya Ibada”, nayo ni Swala, Funga, Zaka na Hija, vilevile huingia katika ibada yanayokutana na hizi nguzo miongoni mwa ibada, na huitwa matawi ya hizi ibada, kama vile hukumu za Twahara, mafungu ya Zaka, Itikafu, Umra na zinginezo ([6]).
Misingi ya Ibada: Ni kuingia katika kuabudu kama vile kuswali, tofauti na kafara ([7]).
Ama kuabudu maelezo yake yatakuja, pamoja na tofauti kati yake na ibada chini ya anuwani huru, kutokana na umuhimu wake.
Uchambuzi: Je asili ni sababu au kutokuwepo sababu?
Kumekuwa na tofauti kati ya Wanachuoni: Je kanuni katika misingi ya hukumu ([8]) ni kutokuwa na sababu kama hakuna dalili ya kuwa na sababu, au asili yake ni kuwa na sababu ila kwa dalili yenye kuzuia?
Kauli mbili zimeelezewa na Maimamu wawili Imamu Dabuusi na Maimamu wa madhehebu ya Abu Hanifa R.A. wamesema: Kinachokubaliana zaidi na Madhehebu ya Imamu Shafi kwa asili ni kuwa na sababu, isipokuwa ni lazima ili sababu ifae katika kila asili kuwepo na dalili inayoweka wazi.
Wamesema: Madhehebu ya Wanachuoni wetu – kwa maana ya Wanachuoni wa Madhehebu ya Abu Hanifa – ni lazima kuwepo dalili inayoonesha hivi sasa kuwa na sababu ([9]).
Imamu Shatibiy R.A. amejaribu kutuelezea udhibiti wa mlango huu akasema: “Dalili zote za Kisharia zimethibiti ndani ya Qur`ani na wala hazijawekewa kanuni wala udhibiti maalumu, basi yenyewe inarejea katika maana inayokubalika iliyoegemezwa kwenye mtazamo wa mpewa amri, sehemu hii inapatikana sana kwenye mambo ya kawaida ambayo yenye maana inayokubalika, kama vile uadilifu, wema, usamehevu, subira, shukrani, shuluma, ubaya, uovu, kuvunja makubaliano katika jumla ya mambo yaliyokatazwa.
Kila dalili iliyothibiti ndani yake sharti na wala si ya moja kwa moja na kuwekewa kanuni na udhibiti basi dalili hiyo inarejea kwenye maana ya kufuatwa tu, haihitaji mtazamo wa mpewa amri lau utaegemezewa mtazamo wake, ambapo Ibada asili zake hazina nafasi ya kufikiri kiakili kuongea pia na namna ya utekelezaji wake, vilevile katika mambo yanayojitokeza kwenye hizo Ibada, kwa sababu yenyewe ni katika jinsi yake na ni mambo mengi yanayopatikana ya kiibada, hii ni sehemu ya pili ya misingi mingi ya kawaida, kwa sababu mara nyingi huwa na masharti ya baadhi yaliyoelezewa au kuanzisha hukumu zilizopatikana kwa sababu ndogo ndogo”([10]).
Uchambuzi: Tofauti kati ya Ibada zenye sababu na zisizo na sababu:
Tumeelezea huko nyuma kusudio la Ibada, ama Ibada za kutekeleza tu huitwa na kukusudiwa maana ya Ibada, na Wanachuoni wengi hutumia – kwa inavyoonekana kwetu sisi – ni kuwa huitwa hivyo na kukusudiwa hukumu za Kisharia ambazo hazioneshi sura ya hekima ya kuwekwa kwake zaidi ya kufanyiwa kazi na kuonesha utekelezaji, hukumu katika Ibada au isiyokuwa ya Ibada inaweza kuwa ya kutekelezwa kwa asili yake, kama vile kuutakasa Umma ambao umenunua na kuuza katika kikao cha mauzo, na kurudi kwake kwa kuvunja makubaliano kabla ya kuonekana na mnunuzi wake.
Kama vile Ibada kuna aina nyingi, miongoni mwake ni Swala, Zaka, Funga, Hija, na hukumu zake nyingi ni za kimaana, Sharia imebainisha hukumu zake, au Wanafiqhi wameleta hekima zake kupitia maandiko ya Sharia, miongoni mwa hekima hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu kuhusu Ibada ya Swala: {Na ushike Sala. Hakika Sala inazuilia mambo machafu na maovu} [Al-Ankabout: 45]. Na kauli yake kuhusu Ibada ya Hija: {Ili washuhudie manufaa yao} [Al-Hajj: 28]. Na kauli ya Wanachuoni katika hekima ya kuruhusu kula mchana ya Ramadhani kwa msafiri wakati wa safari yake: Yenyewe ni kuondoa uzito, katika hekima hiyo hakuna kitu cha kutekelezwa tu bila ya kufahamika hekima yake hata kama kitakuwa kinahusiana na Ibada.
Baadhi ya hukumu za Ibada hazikubaliki pia maana zake hazikubaliki hivyo huingia katika Ibada za kutekelezwa tu bila kufahamu hekima zake, kama vile Ibada ya kutawadha kwenye viungo maalumu, kuswali kwa mfumo wa kuinua mikono kusimama kurukuu na kusujudu, na kuwa kwake kwa hatua tofauti, kuhusisha kufunga mchana na sio usiku, kupangiliwa Swala ndani ya nyakati maalumu na sio nyakati zingine za mchana na usiku, kuhusisha Ibada ya Hija na matendo yake yanayofahamika, katika maeneo yanayofahamika na kwenye Misikiti Maalumu, na mfano wa hayo katika yale akili haiyaelekei([11]).
Uchambuzi: Maelezo kuwa mambo ya kutekelezwa tu yana hekima zake hata kama imefichikana kwetu:
Kutofahamu kwetu maana ya kuwekwa kwa hekima ndiyo ina maanisha kufichika kwetu hekima, hapana hekima zimewekwa si kwa uwepo hekima, kwani amri zote za kutekelezwa – kama Al-Qurafi anavyosema – maana yake kuna maana hatujaijua, si kwa maana haina hekima ([12]), na anasema pia: “Kanuni ya Sharia ipo kusimamia masilahi kwa upande za amri. Na kuondoa uharibifu kwa upande wa makatazo kwa njia ya ubora na wala si njia ya wajibu wa kiakili – Kama Muutazila anavyosema – lazima tuamini katika yale si ya uharibifu wala masilahi ikiwa kwa upande wa amri kuna masilahi, na ikiwa kwa upande wa makatazo kuna uharibifu, kama kusema kuhusu nyakati za Swala: Zenyewe zimekusanya masilahi hatuyajui, vilevile kila amri isiyo na hekima maana yake ndani yake kuna masilahi hatuyafahamu” ([13]).
Baadhi ya Wanachuoni wanayasisitiza haya wanasema: “Amri nyingi zinatajwa na Wanachuoni zisizo na hekima za kutelezwa tu, maana ya hukumu hizo ambazo hekima zake hazionekani upande wetu pamoja na sisi tunapitisha kuwa lazima kuwe na hekima zake, na hilo kwa sababu sisi tumejiridhisha kawaida ya Mwenyezi Mungu tumekuta ni yenye kuleta masilahi na kuondoa uharibifu, kwa hili Ibn Abbas R.A. amesema: Pindi unaposikia wito wa Mwenyezi Mungu basi huwa unakuita kwenye kheri, au kukuondoa kwenye shari kama vile wajibu wa Zaka na matumizi ili kuondoa mianya, kuharamisha kuu,a uzinzi, ulevi, wizi, tuhuma ya uzinifu ili kulinda nafsi kizazi akili mali na heshima kutokana na uharibifu… kwani Mwenyezi Mungu Anapoleta hukumu tunafahamu kuwa ameiweka kwa hekima kisha ikionekana kwetu tunasema: Inakubalika kimaana, na kama haitoonekana tunasema hiyo ni amri isiyo na hekima ya kutekelezwa tu” ([14]).
Imamu Ibn Aabidiin mtu wa Madhehebu ya Hanafi anasema: “Wanachuoni wametofautiana katika mambo yasio na hekima je yamewekwa kwa hekima itokayo kwa Mwenyezi Mungu na kufichwa kwetu au hapana? Wengi wanasema kauli ya kwanza, nayo yenye mwelekeo wa dalili ya kusoma kawaida ya Mwenyezi Mungu kuwa kwake Mwenye kuleta masilahi na kuondoa uharibifu, alichokiwekea Sharia ikiwa kwetu itaonekana hekima yake tunasema: Hiyo inakubalika, na kama haitoonekana tunasema: Hiyo haina hekika ni kutekeleza tu” ( [15]).
Sheikh Al-Bujairami mtu wa Madhehebu ya Imamu Shafi amesema: “Si maana yenye kukubalika kiuhalisia ina sababu hata kama hatujaiangalia” ([16]).
Al-Futuhi mtu wa Madhehebu ya Hanbal amesema: “…Masilahi yote yamepewa hekima, na si kila kilichopewa hekima ni masilahi, kwa kufaa kupewa hekima kwa sifa ya amri ya kufanyiwa kazi tu, hakuonekani sura ya masilahi ndani yake, kisha kuwa na wasifu wa masilahi, kwa sababu huenda yakawa ni masilahi ya Umma, kwa maana yanakusanya manufaa tu, na huenda yakawa ni masilahi maalumu, kwa maana kuwa kwake upande wa umuhimu kuhitajika na kukamilisha” ([17]).
Hekima zenye kuelezewa ndizo ambazo huonekana kwetu, nazo ndizo zilizoelezewa na Jamhuri ya Wanachuoni kwa kauli yao: “Yenyewe inakubalika kimaana”.
Ama hekima zisizoelezewa nazo ndizo ambazo huelezewa kwa kauli yao: “Zenyewe ni za kutekelezwa tu” kwa maana: hazifahamiki kimaana ([18]), nayo ndiyo ambayo Sharia haijazungumzia sababu zake na hekima zake, si jambo lenye kuwezekana na akili kufikia sababu zake, na hilo ni kama vile hekima ya idadi ya Swala kuwa tano na idadi ya rakaa zake, pia idadi ya mzunguko wa kutufu Kaaba, kuhusisha viungo maalumu kutawadha na yasiyokuwa hayo.
Mmoja wa Wanachuoni ameelezea sifa ya Ibada kuwa yenyewe ni ya kutekelezwa na inakuwa ni jambo la kufanya jitihada ([19]), kwani uelewa hutofautiana katika kufahamu Ibada kwa sehemu hii au nyingine, na hilo linarejea katika kutofautiana uelewa na ufahamu, kwani Mwanachuoni anaweza kusoma kitu hajasoma mwingine, na anaweza fikia sababu na hekima haijafikiwa na mwingine ([20]).
Wakati wowote tukisema kuwa hukumu fulani ya kufanyiwa kazi tu haina hekima kanuni inakuwa: Ni kutoulizwa maana yake ([21]), ni katika milango ya Fiqhi baadhi yake inakuwa ni ya kutekelezwa tu na baadhi yake ina eleweka kimaana, kama mlango wa Eda kwa Madhehebu ya Imamu Hanbal ([22]) kama vile maelezo yake yatakavyoelezewa.
Mwenye kuangalia Ibada nyingi na maandiko yaliyopokewa kwenye Ibada hizo, pamoja na kauli za Wanachuoni katika kuelezea ufahamu wake na hekima zake atakuta: Ibada nyingi zina sababu, kila hukumu ina sababu yake na hekima yake maalumu, ameifahamu mwenye kuifahamu na ameshindwa kuifahamu aliyeshindwa kuifahamu ([23]), kama vile Ibada ya Zaka ni katika Ibada inayofahamika sababu za asili ya uhalali wake, na sababu zake zimetamkwa. Mwenyezi Mungu Anasema: {Chukua sadaka katika mali zao, uwasafishe na uwatakase kwazo} [Attawba: 103.] Lengo la kuchukuwa mali ya Zaka ni kusafisha na kutakasa, nayo ni moja ya maana zinazoeleweka katika uwekwaji wa Ibada ya Zaka, Imamu Abu Hanifa R.A amesema: “Zaka imewajibishwa kwanza ni Ibada ya Mwenyezi Mungu, na imewekwa ili kuiridhisha nafsi kwa kupunguza mali ambapo kujitosheleza kwa mali ni sababu ya upotofu na kuingia kwenye uharibifu” ([24]).
Na kuna maana nyingine inafahamika ni katika uwekwaji wa Ibada ya Zaka, nayo imeelezewa katika Hadithi: “Huchukuliwa kutoka kwa matajiri wao na kupelekwa kwa masikini wao”([25]), Qur`ani Tukufu imebainisha matumizi ya Zaka katika kauli yake: {Wa kupewa sadaka ni mafakiri, na masikini, na wanao zitumikia} [Attawbah: 60]. Aya imeweka wazi kuwa makusudio ya Zaka ni kuziba mahitaji ya watu wa makundi manane.
Zanjani anasema: “Inaaminika kwa watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi R.A kuwa Zaka ni mali, imewajibishwa kwa matajiri kuwapa watu masikini kwa ukaribu wa Uislamu ili kuwaliwaza, na maana ya Ibada ni kufuata hivyo, na Sharia imeithibitisha ikiwa kupendezesha katika utekelezaji wake, ambapo nafsi imezoea ubahili, hivyo ikaamrishwa kujiweka karibu kwa Mwenyezi Mungu kwa utoaji Zaka, ili kupata thawabu, na kufanya haraka kufikia makusudio” ([26]).
Na katika hilo pia: Jihadi yenyewe hata kama ni katika Ibada, nayo inafahamika kimaana, na hekima yake inafahamika, hivyo jihadi imewekwa ili kuondoa fitina na uharibifu duniani, pia kuliinua neno la Mwenyezi Mungu, Imamu Shatibiy anasema: “Jihadi hata kama itakuwa ni matendo maalumu katika Ibada, kwa ukweli nayo ni inafahamika kimaana, kama vile faradhi zenye kutosheleza ambazo ni masilahi ya dunia” ([27]).
Na italetwa mifano ya kifiqhi juu ya ulinganisho katika Ibada.
Uchambuzi: Ubora kati ya hukumu zisizo na hekima na hukumu zenye hekima:
Baadhi ya Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi wamesema kuwa ibada zisizo na hekima ni bora zaidi ya zilizo na hekima kwa sababu kuzitekeleza kwake kumehimizwa sana, na ikasemwa: Kwa sababu ndani yake kuna kuilazimisha nafsi, na imesemwa: Kwa sababu ni kutakiwa kuzifuata tu tofauti na zile zinazoonesha sababu yake kwani mtekelezaji wake anaweza kutekeleza kwa ajili ya kupata sababu yake, na ikasemwa: Kutokana na kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu pamoja na kutofahamu sababu yake ([28]).
Na wengine wakasema miongoni mwa watu wa madhehebu ya Imamu Shafii na Imamu Abu Hanifa: Wakati wowote inapokuwepo hukumu kati ya kuwa kwake haina hekima yake au kufahamika hekima yake, basi kuchukuliwa kuwa yenye kufahamika hekima ni bora zaidi, kutokana na uchache wa hukumu zisizo na hekima ukilinganisha na zile zenye kufahamika hekima ([29]).
Ibn Aabideen Al-Hanafi anasema: “Tamartashiah aliulizwa: Je hukumu isiyofahamika hekima yake ni bora au zenye kufahamika hekima? Akajibu, sijaona kwa Wanachuoni wetu zaidi ya kauli yao katika asili: Asili ya maandiko kuwa na sababu, akiwa anaashiria juu ya ubora wa hukumu zenye kufahamika hekima, na nimeona hivyo katika Fatwa ya Ibn Hajar amesema: Suala la maelezo ya Ibn Abdulsalaami kuwa hukumu isiyofahamika hekima ni bora, kwa sababu hutekelezwa tu, tofauti na ile inayofahamika sababu yake kwani mtekelezaji wa anaweza kutekeleza ili kupata faida iliyopo, lakini ameeleza kinyume Al-Balqiiny akasema: Hakuna shaka kuwa yenye kufahamika maana kwa upande wa jumla ni bora zaidi, kwa sababu Sharia nyingi zipo hivyo, kwa kuangalia moja moja inaweza kuwa isiyofahamika hekima ni bora zaidi kama vile kutawadha na kuoga Janaba kwani kutawadha ni bora zaidi, na inaweza kuwa yenye kufahamika hekima ni bora zaidi kama vile kutufu na kurusha vijiwe, kwani kutufu ni bora zaidi([30]).
Uchambuzi: Kusudio la kulinganisha katika Ibada:
Kulinganisha katika Ibada hufanyika wakati wa kufahamika maana yake, na hii maana kuwa ndiyo makusudio ya asili ya kuwekwa hukumu, hupelekea maana hiyo kufahamika kwa wasifu, ambapo huwa ndiyo sababu ambayo hujengewa ulinganisho, kisha kwa kulinganisha asili ya hukumu hukamilika kuhamishiwa kwenye tawi – pamoja na kukamilisha masharti ya ulinganisho – ambayo hayajaeleza juu ya hukumu, Zarkashy anasema: “Kila hukumu ya Kisharia inasababu yake inayofanyiwa ulinganisho” ([31]).
Ulinganisho hufanyika katika Ibada zisizofahamika hekima na zinazofahamika, kwa sababu ulinganisho sehemu ya kufahamika maana, ama ibada isiyofahamika maana yake inakuwa haifahamiki hekima haifanyiwi ulinganisho, wala haijafahamika tofauti ya zisizofahamika hekima na zingine miongoni mwa hukumu zenye sababu maalumu, zaidi ya kushindwa kufahamika sababu kwa njia yenye kuzingatiwa, inayofahamika katika chambuzi za ulinganishi katika elimu ya Usuul, hivyo Ibn Aabideen anasema: Hukumu iliyowekwa na Mwenyezi Mungu ikiwa itaonekana hekima yake tunasema: Inafahamika kimaana, na kama haitaonesha tunasema: Yenyewe si ya kihekima, hapa kauli za Wanachuoni zimetofautiana katika kuzingatia baadhi ya hukumu zisizofahamika hekima au zenye kufahamika, kinachoonekana na baadhi ya Wanachuoni zisizofahamika hekima baadhi ya wengine wanaona zina hekima kwenye masilahi ya watu wake ([32]).
Yanayofikiwa katika maelezo haya ni yale yaliyokuwa hayafahamiki hekima hayafahamiki maana yake hayalinganishwi, na yanayofahamika maana hufanyiwa ulinganishi na wala hayawi ya kutekelezwa tu, hilo ni sawa sawa katika ibada au au mambo mengine.
Huenda kauli ya kutofahamika hekima ya jambo ni kwa upande wa ujumla, hilo halizuii kufanyiwa ulinganisho katika baadhi ya ufafanuzi wake au katika baadhi ya yanayokusanywa na kwenye matawi, baadhi yao wamesema: “Hukumu jumuishi hazielezi sababu, kwa sababu mwanadamu pindi anaposafiri kwenye nchi nyingine analazimika kutembea na kukata masafa, kisha hatoi sababu za kutokuwa makini na hatari zake, hii ni sahihi kwa upande wa mwanadamu, ama katika hukumu za Kisharia hakuna, kwa sababu Mwenye kuweka hukumu hana anachohofia hivyo hufikia masharti ya ziada kwenye masilahi, kwa sababu sharti la ziada haliwi isipokuwa kujua na kuwa makini na hatari” ([33]), kwa upande wa watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi – kwa mfano – wanasema uharamu wa riba ni jambo lisilofahamika hekima, na mambo yasiyofahamika hekima hata kama hayaingii kwenye ulinganisho, lakini hukumu kuwa haifahamiki hekima ni hukumu ya mjumuisho ambapo haiongezwi aina ya tatu, hivyo haipingani na ulinganisho kama ilivyoelezewa kwenye vitengua udhu ([34]), miongoni mwa mifano yake pia kulinganisha kwao mbwa na nguruwe katika kuosha chombo mara saba, pamoja na hilo kuwa asili ya isiyofahamika hekima([35]), na maelezo yake yakina yatakuja.
Wala sio kusudio la ulinganisho wa Ibada:
Kuleta Ibada mpya zaidi ya Ibada zilizopo, kwani haifai kuthibitisha Ibada iliyoanzishwa, kama vile Swala ya sita au Hija nyingine, kwani hufikiwa kujulikana kwake kwa kuthibiti na wala si kwa rai na jitihada, kwani haifai kuthibitisha Ibada kwa njia ya kulinganisha,
Au kuthibiti namna maalumu ya Ibada zilizopo ([36]).
Uchambuzi: Kukubaliana kati ya kauli ya Wanachuoni kuwa sababu huleta hukumu na kati ya kauli ya wanaozungumza kuwa hukumu za Mwenyezi Mungu hazina sababu:
Sharia – kama anavyosema Imamu Sarkhasy Al-Hanafi R.A. - imeweka ishara kwa upande wa kuwa haijiwajibishi yenyewe, lakini huwajibisha hukumu kwa kuifanya Sharia yenye kuwajibisha kufanyiwa kazi, inafahamika kuwa haiwezekani kufanyiwa kazi isipokuwa baada ya kufahamika Sharia yenyewe, njia ya kufahamika huko ni kwa andiko au kuchimbuliwa kwa rai, wala hailetwi rai pindipo hukumu haikuwa inafahamika kimaana, kwa sababu kufahamika ni njia ya kufahamika, kama vile hisia njia ya kufahamika kinachohisiwa pasi na kisichohisiwa, hii si sehemu ya hukumu iliyothibiti kwa andiko isiyofahamika kimaana, kwa sababu tamko hujiwajibisha lenyewe, kwani ni maneno ya mwenye kuthibitisha elimu yakinifu kwa kauli yake, imepatikana huko maana kwa andiko, kuwa kwake si yenye kufahamika kimaana haitushindishi kufanyia kazi, ama sababu za baadhi ya wasifu zenyewe hazijiwajibishi, bali ni lazima kufanyiwa kazi kwa njia kuwa ni kufanyia kazi rai ili kufika kwenye hoja katika hukumu ya kisharia, na isiyofahamika kimaana ndani yake haifanyiwi kazi rai([37]), bali inafaa kufanyia kazi rai wakati wa kufahamu maana ya andiko au tamko, na hili linakuwa katika yanayofahamika kimaana, ama yasiyofahamika kimaana sisi hatupitishi kufanyia kazi rai kwa hukumu yake kuvuka kwenda kwenye hukumu isiyo na tamko([38]).
Taji Sabkiy Al-Shafi anasema: “Swali linabakia wanaloulizwa Masheikh nalo ni kuwa yanayofahamika kuhusu wazungumzaji ni kuwa hukumu za Mwenyezi Mungu hazielezewi sababu, na inafahamika kwa Wasomi wa sababu kuwa sababu kwa maana ya kisababishi, na wengi miongoni mwao hudhania ndiyo sababu ya uwekaji wa hukumu kama vile ndiyo inayoondosha na tumeeleza ubatilifu wake, kumekuwa na mgongano kati ya maneno ya Wanafiqhi na Wazungumzaji, Sheikh Al-Islami bado anaendelea kukusanya kati ya maneno yao na akasema: Hakuna mgongano kati ya maneno ya pande mbili kwa sababu kusudio la sababu ndiyo inayosababisha kitendo cha mwenye kuamrishwa, mfano wake ni kama kulinda nafsi kwani ni sababu inayopelekea kisasi ambacho ndiyo amri iliyohukumiwa kwa upande wa Sharia, hukumu ya Sharia haina sababu wala kisababishi, kwa sababu inauwezo wa kulinda nafsi pasi na sababu, lakini amri yake imefungamana na kulinda nafsi nayo ndiyo kusudio, na kisasi kwa kuwa kwake njia ya kuelekea kulinda nafsi, hivyo makusudio na njia vyote ni makusudio ya Sharia, Mwenyezi Mungu Amepitisha kawaida kuwa kisasi sababu ya kulinda nafsi, ikiwa mtu ametenda kosa basi Sultani na Hakimu pamoja na Msimamizi wa mambo ya nchi lazima watekeleze damu ya kisasa, na kumkosoa muuaji ikiwa ni kutekeleza amri ya Mwenyezi Mungu kwenye hilo, na ni njia ya kulinda nafsi, basi wanakuwa na malipo ya aina mbili, malipo ya kutekeleza kisasi na malipo ya kulinda nafsi, na yote mawili yameamrishwa na Mwenyezi Mungu, amri ya kwanza ni katika kauli yake: {Mmepewa ruhusa kulipa kisasi} [Al-Baqarah: 178], na amri ya pili ima kwa kwa kuleta hukumu ima kwa imani katika kauli yake:
{Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi} [Al-Baqarah: 179], hivi ndio hutumika katika Sharia zote.
Kwa maelezo hayo inabainika kuwa hukumu zote zenye kufahamika hekima Sharia ina makusudio mawili:
Kusudio la Kwanza: Hiyo hekima. Kusudio la Pili: Kitendo ambacho ndiyo njia ya kuelekea, kuamrishwa kufanya kitendo hicho kusudio lake na hiyo hekima, hivyo hekima ndiyo msukumo kwa muamrishwa kufanya kitendo na wala si kwa kuwekwa Sharia.
Hivyo anafahamu kuwa hukumu yenye kufahamika hekima ina malipo zaidi kuliko hukumu isiyofahamika hekima, ndiyo hukumu isiyofahamika hekima ina maana nyingine, nayo ni kuwa nafsi yenye kutambua, inaweza kuwa malipo moja ni zaidi ya malipo mawili ambayo yapo kwenye hukumu inayofahamika hekima, na anafahamu pia kuwa sababu ni sawa sawa imetamkwa au imefahamika ina faida, na watu wametaja faida zake, na tuliyotaja ni faida zaidi nayo ni kusudio la mwenye kuamrishwa kufanya kwa ajili yake hivyo kuongezeka malipo yake, angalia faida hii kubwa na tumia katika kila masuala yanayoletwa kwako na tenganisha kati ya nafasi tatu, nazo: Hukumu ya Mwenyezi Mungu kwenye kisasi, kisasi chenyewe, kulinda nafsi nayo ni sababu ya pili na wala si ya kwanza, vilevile kulinda mali kwa kuzuia wizi, na kulinda akili kwa kuiepusha na ulezi” ([39]).
Imamu Zarkashy R.A. anasema: “Fahamu kuwa Madhehebu ya Watu wa Sunna ni kuwa hukumu za Mola Mtukufu hazina sababu, kwa maana Mwenyezi Mungu hafanyi kitu au jambo kwa lengo, wala hapeleki kitu au jambo kwa kufanya kitu, bali Yeye Mwenyezi Mungu ni Mwenye uwezo wa kuleta masilahi bila ya sababu ya kuondoa madhara bila ya msukumo wowote, Wanachuoni wamesema: Hukumu zenye sababu wala Watu wa Sunna hawakwenda kinyume na hili, bali wamemaanisha sababu kwa maana ya hekima, watu wa Muutazila pamoja na wale wanaowafuata wamesema: Matendo ya Mola Mtukufu yamefungamana na hekima iliyobanwa kwa sura ya masilahi, na katika maelezo ya watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa yanakubaliana na hayo, kwa sababu hiyo kwetu sisi kazi ya maji ni katika kuondoa uchafu tofauti na wao, vilevile mvinyo wa tende hautawadhiwi tofauti na wao, ukweli ni kuwa kuangalia hekima kwenye matendo ya Mwenyezi Mungu na hukumu zake ni jambo linalofaa na wala halijapingwa na yeyote, bali watu wa Al-Ashariya wamepinga sababu malengo kuboresha akili na kusimamia masilahi, tofauti kati ya kuangalia hekima ipo wazi, kuficha lengo kumetokea mgongano.
Unapotaka kufahamu hekima katika mambo ya ulimwengu au ya kidini au Kisharia basi angalia yanayotokana na malengo katika sehemu za ulimwengu na kidini, utafahamu kutokana na nukuu sahihi kama vile kauli ya Mwenyezi Mungu: {ili tumuoneshe baadhi ya Ishara zetu} [Al-Israa: 1], katika hekima ya Mtume S.A.W. kupelekwa usiku kati ya Msikiti wa Makka na ule wa Al-Aqsaa, na kwa kufupisha hii kanuni inaonesha matatizo mengi na kuonekana upole na huruma ya Mwenye Utukufu.
Ibn Rihhal ameeleza katika sherehe ya kitabu cha Al-Muqtarah jambo kwa njia nyingine akasema: Watu wetu wamesema, dalili kuwa hukumu zote za Kisharia zipo kwa masilahi ya waja, Wanachuoni wa Umma wamekubaliana hilo, ima kwa upande wa huruma na ubora kwenye asili yetu, au kwa upande wa wajibu kwenye asili ya kundi la Muutazila, sisi tunasema: Hilo hata likiwa linazingatiwa katika Sharia lakini si kwa njia ya wajibu, na wala si hukumu kuepukana na masilahi yasionekana katika akili kama wanavyosema watu wa Muutazila, bali tunasema kuchunga masilahi haya ni jambo lipo katika Sharia, na akili inafaa kutoingia kama mambo mengine ya kawaida.
Kisha mwenye kusema ni wajibu hana anachohitaji ni nini maana ya wajibu Kisharia, lakini kwake maana yake ni kuwa kinyume kwa Muumba haifai, kama ilivyo kwenye elimu kinyume chake - ni ujinga –haifai, kwa njia hii maneno ya Ibn Al-Hajibu na wengine yanaondoka na kuleta matatizo….
Imamu Al-Hirasy Al-Shafii amesema: Katika hukumu za Kisharia je zina sababu za kihekima au hapana? Baadhi yao wamesema haifai Mwenyezi Mungu kuabudiwa na waja wake kwa Ibada isiyo na mafanikio ndani yake, kauli hii inahitajika.
Sisi pamoja na kupitisha Mwenyezi Mungu kuabudiwa na waja wake vile anavyotaka, lakini tuliyoyafahamu kutokana na Sharia ni kuwa zimewekwa kwa manufaa, Aya za Qur`ani na Hadithi pamoja na makubaliano ya Wanachuoni yameonesha Sharia kukubaliana na desturi njema na siasa zilizobora, na zenyewe haziachani na masilahi ya sasa na ya baadaye. Mwenyezi Mungu Amesema: {Mitume hao ni wabashiri na waonyaji, ili watu wasiwe na hoja juu ya Mwenyezi Mungu} [An-Nisaa: 165]. Na Mola Anasema tena: {Na ili Mwenyezi Mungu amjue anaye mnusuru Yeye na Mitume wake kwa ghaibu} [Al-Hadid: 25]. Na Akasema: {Kwa hakika tuliwatuma Mitume wetu kwa dalili waziwazi} [Al-Hadid: 25]. Yote haya yanaonesha kuwa Mwenyezi Mungu Anaabudiwa kwa Sharia kwa mafanikio ya waja, na hili halifahamiki isipokuwa kwa Sharia, na akili haioneshi wakati wa kutokea moja ya vitendo viwili kitendo kingine kinatokea kwa njia ya hiyari ikiwa kilichoteuliwa miongoni ni katika iliyothibiti hekima yake, hilo likiwa ni sahihi basi kimoja kinakuwa ni Qiyas kama tutakavyoeleza.
Hukumu za Kisharia zinagawanyika:
Katika hukumu za Kisharia tulizoziangalia na kwa upande wa hekima kwa dalili zilizopo kwenye andiko kwa upande mmoja, na zingine hazijaangaliwa kwa upande wa hekima zilizojificha, hiyo ni katika wema wa Mwenyezi Mungu ambao hauonekani, hivyo ni kuhusisha amri kwa wakati mmoja bila ya wakati mwingine, na kuhusisha baadhi ya vitendo kuwa Sunna na vingine kuwa wajibu, haya ni masilahi kama inavyofahamika kwa upande wa watu wa Ibada…
Mwenyezi Mungu Ameweka mambo ya waja wake kwa kuwafahamisha maana zake na ujumla wake, na kuwaficha maana za ndani na za kina, kama tulivyoona watu wawili wametoa sababu na kutafautiana sababu zao tumefahamu sura ya kutafautiana kwao, lau tutauliza kuhusu tofauti hatutafahamu… ikiwa utafahamu hilo basi tuliyoyataja miongoni mwa kujumuika mambo makuu ya Sharia na yale madogo madogo kwenye masilahi na kugawanyika kwake kwenye yale yanayoonekana kwa waja na yasiyo onekana kwao hakuna tofauti katika hayo, lakini wametofautiana nyuma ya hayo katika ulinganisho wa Kisharia na ni katika uelewa wa hukumu, na wale ambao wamejibu kuhusu Qiyasi “Ulinganishi” wametofauti, wakasema: Haifai kabisa kwenye mambo ya kuabudu, na wakasema: Inafaa lakini inazuiliwa kwenye mambo ya kuabudu, wakasema: Inazuiliwa ulinganishi kwenye mambo ya kuabudu katika matukio yote kwa sababu ni lazima kuwepo asili ya sababu na kuchukuliwa na matawi, kwa hili tumesema:
Hiyo ni dhana ambapo upande wa masilahi umefichwa kwetu, hakuna kufika kwenye maana moja kati ya maana mbalimbali kwa sura anayofahamu kuwa ina manufaa zaidi bila ya nyingine, na kwa ajili hiyo rai na mitazamo imetofautiana, bali tumezingatia asili ya kusikia ya kufaa ulinganishi kwa sababu haifai kiakili kurudisha tawi kwenye asili, wala haifai kufikiwa hukumu zake kwa ishara ambazo hufikia mfano wake kwenye masilahi ya dunia, kwa sababu kuna ishara zenye kufahamika kwa kawaida ([40]).
Uchambuzi: Asili katika hukumu kukubalika kiakili, na asili katika Ibada kuabudu:
Asili – Kama anavyosema Al-Aamidy Al-Shafi – hukumu kuwa inafahamika kimaana ([41]), na Al-Futuhi Al-Hanbaly amesema: “Mara nyingi katika hukumu ni kufahamika kiakili tofauti na mambo ya kuabudu” ([42]).
Lakini baadhi ya Wanachuoni wamesema kuwa: “Asili katika Ibada ni kuabudu” ([43]), na Ibara hii sio kama ilivyotolewa kama inavyodhaniwa na wengi, ambapo kusudio ya hilo: “Kusimama kwenye kiwango cha Kisharia, kwa maana kuwa Sharia imekusudio kusimama kwenye mpaka wake ambapo aliyeamrishwa asiuvuke, hivyo makusudio ya Kisharia ni kumuabudu Mwenyezi Mungu kwenye mipaka hiyo, bila kuzidisha au kupunguza.
Haya yameelezwa na Mwanachuoni Ibn Dakiki Al-iid katika kauli yake: “Ibada kwa upande wa Sharia kuwa imepangiliwa kwa sura maalumu, baadhi ya watu wanataka kuleta jambo lingine halijapokewa na Sharia, wakidhani kuwa itaingizwa katika jumla ya Ibada, hili haliwezi kusimama kwa sababu Ibada nyingi ni kuabudiwa, na chanzo chake ni amri tu”([44]).
Mwenye kupewa amri anapofanya kitendo kwa mujibu wa Sharia ilivyoweka –hupata thawabu, na hubatilika tendo na kustahiki adhabu anapofanya tofauti, hivyo ni lazima kusimama kwenye mipaka yake iliyowekwa na Sharia pasi na kuzidisha au kupunguza bila kuwepo andiko.
Maana hii haipingani kulinganisha na kitu kingine, na kupitisha hukumu ya amri hiyo na amri nyingine, mfano wa hilo ni pamoja na yaliyokuja katika Ibada ya Swala ambayo imehusishwa na vitendo maalumu kwa sura maalumu, kama vile Swala ya kukamatwa kwa jua, watu wa Madhehebu ya Imamu Hanbal mara zote wamelinganisha Swala ya tetemeko la ardhi na Swala ya kukamatwa kwa jua – kwa kukusanya kuwa matukio yote hayo ni alama zenye kutisha kwa waja ili wapate kuacha maasi na kurejea kwenye kumtii Mwenyezi Mungu ili kuwaondolea tatizo – na hilo ni pamoja na kutekeleza kwa umbile lilopekewa katika Swala ya kukamatwa kwa jua bila ya kuzidisha wala kupunguza([45]).
Kisha kauli ya baadhi yao: “Hakuna ulinganishi katika Ibada” – moja kwa moja – si yenye kufuatwa, kilichobora kusema: “Hakuna kulinganisha katika amri za kuabudu” nazo ndizo hazifahamiki maana yake, na kulinganisha katika Ibada ni jambo lenye kupendeza, kwa sababu kila hukumu ya Kisharia inawezekana sababu yake hufanyiwa ulinganishi ([46]).
Uchambuzi: Madhehebu ya Wanachuoni katika Ibada kuziwekea sababu na ulinganishi, na kubainisha sababu ya tofauti.
Wanachuoni wametofautiana Madhehebu mawili katika sababu za Ibada na kuzilinganisha:
Madhehebu ya Abu Hanifa wao wanazuia katika asili za Ibada, Sheikh Al-Asmandy Al-Hanafi anasema: “Watu wametofautiana katika kuthbitisha asili ya Ibada na mengine katika yanayokadiriwa – kama vile adhabu na kafara – kwa kulinganishwa: Al-Karakhy na idadi ya wazungumzaji wameelezea kuzuiliwa, na Al-Karkhy amefuata maelezo ya Abu Hanifa R.A. ([47]). Na Imamu Fakhr Ar-Razy kuzuia akakunasibisha kwa Imamu Jubbany ([48]).
Ameelezea Imamu Shafi na watu wake kufaa kulinganisha kwa yale yanayofahamika moja kwa moja kimaana, ni sawa sawa ya kwenye Ibada au si Ibada, na akazuia kulinganisha katika yasiyofahamika kimaana, nayo ni Madhehebu ya Jamhuri ya watu wa Usuul, na kukubalika rai hiyo na Imamu Ar-Razy na wafuasi wake pamoja na Taaju Al-Sabaky([49]), kwa kauli hii Imamu Shafi anakubaliana na wanaozuia kama yaliyomo kwenye idadi za rakaa hayafahamiki maana, hivyo haiwezekani kuleta sababu, na kila kisichofahamika kimaana hakifai kukilinganisha kwa sababu ya kukosekana kufahamika sababu([50]), miongoni mwa sharti zao za kulinganisha ni kitu kinacholinganishwa kutokuwa kuabudiwa, na mambo ya kuabudiwa hayaingii kwenye ulinganishaji([51]).
Imamu Hanbal anasema, miongoni mwa masharti ya kulinganisha ni hukumu kuwa yenye kufahamika kimaana, ambapo kulinganisha ni hukumu kupita kutoka sehemu kwenda sehemu nyingine kupitia kinachohukumiwa, na kisichoeleweka maana yake kama vile nyakati za Swala na idadi za rakaa haviwezekani kupitishiwa hekima ([52]).
Maelezo ya Madhehebu ya Jamhuri:
Imamu Al-Haramaini amezungumzia suala hili kwa mapana, miongoni mwa aliyoyasema: “Watu wa makala wamenukuu kutoka kwa watu wa Abi Hanifa kuwa wao hawaoni kulinganisha katika mambo ya adhabu kafara na yanayokadiriwa, na kufuatwa na Madhehebu ya Imamu Shafi, na kubainika kuwa wao hawajakanusha chochote katika hayo – kisha akataja mifano ya yaliyofanyiwa ulinganishi katika adhabu na kafara… na akaweka wazi kwa tuliyoeleza yenye sababu na yasiyo na sababu, na sisi tunachukuwa asili hiyo tukizingatia katika kukanusha na kuthibitisha, ikiwa kutapitishwa sababu katika kukanusha na kuthibitisha tutafanya, na ikiwa itazuiliwa tutahukumu kwa kukanusha sababu, sababu inaweza kuzuiliwa kwa andiko la Sharia la wajibu, na kama ingekuwa bila ya andiko ingewezekana kupata sababu, nayo kauli ya Mwenyezi Mungu: {Kama mwenyewe Mtume akitaka kumuoa. Ni halali kwako wewe tu, si kwa Waumini wengine} [Al-Ahzab: 50].
Na Mtume S.A.W. amesema: “Kwa hakika nimehalalishiwa wakati wa mchana, kisha ukarudishwa uharamu wake kama siku Mwenyezi Mungu Alipoumba mbingu na ardhi” ([53])... Andiko vyovyote litakavyotuzuia na kulinganisha tutajizuia, vilevile ikiwa makubaliano yatalazimisha hivi, nayo ni kama makubaliano kuwa mgonjwa hapunguzi Swala, na kuwa sawa kwa msafiri kula mchana wa Ramadhani, ikiwa pande hizi hazijazuiwa basi chenye kufuatwa katika kufaa kulinganisha ni uwezekano wake kwenye udhibiti wa masharti, yenye kufuatwa katika kuzuiwa kwake ni kujizuia nayo na kutoyaleta yalivyowekewa sharti”.
Kisha Imamu Al-Haramaini anataja kuwa kuna milango inafanyiwa ulinganishi katika baadhi ya hukumu zake, na mengine kuzuiliwa, kama vile ndoa kukodi kukopa na kumwangilia, amesema: “Haki ya mwangaliaji kuzingatia hali hizi, na kubaini maeneo ambayo yanafanyiwa ulinganishi, na maeneo ambayo hayafanyiwi, wala ulinganishi hauondoshwi na kuwa sehemu ya amri, vilevile haitwi uthibiti kutokana na sehemu ya kulinganishwa, maelezo yote yameelezwa kwa kina katika maudhui zake, kukanushwa na kuthibitishwa ndani yake kuna tofauti”… kisha akaelezea kwa kina katika ufafanuzi wa hilo, kisha akataja vigawanyo vya sababu na asili kuwa yenyewe inagawika sehemu tano: “Ya kwanza yake ni ile inayofahamika maana yake nayo ndiyo asili…. Na aina ya tano katika asili: Inayofahamika kwa mwenye kuelewa asili ya maana wala kinachopelekea umuhimu na haja, na hii ni chache sana kufikiriwa, yenyewe hata kama itazuiliwa kufahamika sehemu ya maana, basi wala haizuiliwi kufikiriwa yote, mfano wa sehemu hii ibada za kimwili, zenyewe hazifungamani na malengo ya kuondoa wala kunufaika, lakini hazipo mbali na kusemwa: Kuendelea kafanya kazi kunaondosha mabadiliko ya wake kwenye kufuata hukumu, na kumtajataja Mwenyezi Mungu kunazuia maovu na machafu, kisha maneno sehemu hii yanapomalizikia kwa yanayokadiriwa kama vile idadi za rakaa na yaliyo kwenye maana hiyo hayajamtumainisha mlinganishi katika kufahamu maana inayopelekea kukadiria yale yasiyokadiriwa kwa asili yake…hivyo Ibada za kimwili ambazo hazifahamika maana inayohusishwa lakini hufikiriwa mambo ya jumla yanayobeba uvumilivu kwenye kazi za mambo ya kheri, mambo haya ya jumla hatuyapingi kwa ujumla kwa sababu yenyewe ni malengo ya Sharia katika kuabudu Ibada za kimwili….
Na ujuzi huu haudhibitiwi na ulinganisho…ama yanayothibiti kwa amri ya Sharia, na wala hayakuwa ya kufahamika maana basi hayafanyiwi ulinganishi, haya ni kama ujio wa Sharia na Takbira wakati wa kunuia Swala, na kutoa salamu wakati wa kumaliza Swala, na mfano wa haya kuungana rukuu na idadi za kusujudu, mwenye kutaka kuzingatia isiyokuwa takbira kwa takbira na kufikia kuwa ni utukufu na utukuzaji basi atakuwa amekwenda mbali sana” ([54]).
Jamhuri – kama ilivyowazi kwenye maelezo ya Imamu Al-Haramain – hawafanyi ulinganishi katika Ibada au katika mambo mengine, wala hawazuii kabisa, bali wana masharti yao, kama vile wanakubaliana na wanaozuia katika baadhi ya sura hawafanyi ulinganishi, nayo ni katika yanayokadiriwa ambayo Sharia imeyaelezea, Sheikh Sharbini Al-Shafi anasema: “Hatuzuii, kwa maana adhabu kafara yanayoruhusiwa na kukadiriwa, bali tunaweka sharti ikiwa maana haitafahamika” ([55]).
Ibn Hajib Al-Maliky anasema: “Miongoni mwake – kwa maana ya masharti za hukumu asili – kutovuka mwenendo wa ulinganishi, kama vile idadi ya rakaa, makadirio ya adhabu na kafara”.
Na Shamsu Al-Asfahani amesema akisherehesha: “Hukumu ya asili isiwe yenye kurekebishwa mbali na mfumo wa ulinganishaji, kwa maana isiwe tofauti na kanuni katika Sharia, wala isiwe isiyofahamika hekima yake, kama vile kukubalika ushahidi wa Khuzaima peke yake na kuutolea hukumu, hilo ni tofauti na kanuni ya ushahidi ambayo imepitishwa na Sharia bila kufahamika hekima yake, na kama vile idadi ya rakaa na makadirio ya adhabu na kafara, vyenyewe hata kama vitakuwa tofauti na kanuni iliyopo katika Sharia lakini hekima yake haifahamiki”([56]).
Kwa maana haifahamiki hekim aya idadi za rakaa na hukumu zinazokadiriwa, kama vile Swala ya Al-Fajiri kuwa na rakaa mbili, Swala ya Adhuhuri kuwa na rakaa nne, Swala ya Magharibi kuwa na rakaa tatu, na kafara ya kiapo kufunga siku tatu, au kafara ya Dhihar “Kumwambia mke wewe ni kama mama yangu” kufunga miezi miwili mfululizo, hizi rakaa na hizi hukumu za makadirio hazina ulinganishi, na hii haizuii kufanya ulinganishi katika milango ya Ibada na adhabu ambapo hufahamika kimaana.
Chanzo cha tofauti ya ulinganishi katika Ibada:
Wanachuoni wametofautiana kuhusu kufaa kulinganisha katika Ibada na kutofaa, kunarejea kwenye sababu mbili ([57]):
Sababu ya Kwanza: Kutofautiana kwao ikiwa Ibada ni yenye kufahamika maana basi inafaa kufanyiwa ulinganishi, au kama haifahamiki maana basi haifai kufanyiwa ulinganishi? Pamoja na makubaliano yote – kama inavyoonekana kwenye maandiko yao ambayo baadhi yake yameelezwa – kuwa Ibada yenye kufahamika maana hulinganishwa, na isiyofahamika maana hailinganishwi, wametofautiana katika vipengele hivi, je ni katika kufahamika maana ndiyo hulinganishwa au isiyofahamika maana haifanyiwi ulinganishi.
Ni kwa katika Ibada kunaweza kujitokeza hali isiyo na andiko kuhusu hukumu yake, kama vile mtu kukosa maji na jiwe la kustanji, bali anapata tofauti na hivyo kinachoweza kuondoa najisi “Uchafu” ambacho si halali, je inafaa kwake kutumia kitu hiko kwa kufanana kwake na kile kilichoelezewa sababu ya kutumika?
Au linaweza kujitokeza kosa ambalo halina tamko lake pia, mfano: Maeneo ya sijida ya kusahau katika Swala ambayo haijapokewa kutoka kwa Mtume S.A.W. na wala hajasujudu, je mtu anaweza kusujudu?
Wenye kuzuia wanaona kuwa Ibada isiyofahamika maana haina hekima, na kwa vile haina hekima yake hivyo haifai kulinganishwa, na hukumu walizothibitisha ambazo hazina matamko yake, wameelezea kwa njia ya “Dalili ya Andiko” wala si kulinganisha kama yatakavyokuja maelezo yake.
Na waliopitisha wanaona kuwa Ibada zisizofahamika maana katika hukumu zake nyingi, zinafaa kuziwekea sababu na kulinganisha kama Ibada zingine.
Samarkandy Al-Hanafi anasema: “Sahihi kauli ya Wanachuoni wenye kusema: Kwa asili andiko lina sababu, kwa sababu hukumu ya Mwenyezi Mungu inajengeka kwa hekima na masilahi ya waja, ikiwa maana yake inafahamika basi lazima kusema hekima yake, na hukumu zingine zinafaa kutozifahamu kwa akili zetu” ([58]).
Jambo la pili ambalo linatokana na la kwanza:
Je! Maana ya andiko ni ya kulinganisha: Kwa mfano hukumu yenye kuthibiti pia imethibiti kiulinganishi, au yenyewe ni kimatamshi: Kwa mfano hukumu yenye kuthibiti si yenye kuthibiti kiulinganishi?
Ufafanuzi wa hilo: Maana ya andiko kwa watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa([59]) ni: Linalothibitisha maana ya tamko kilugha si kijitihada wala kimtazamo, nayo ni maana ya tamko juu ya kuthibiti hukumu iliyotamkwa tofauti na isiyotamkwa, kwa kushirikiana kwao katika sababu ya hukumu ambayo inaweza kufahamika kwa njia ya lugha bila ya kuhitajika jitihada ya Kisharia, hilo ni sawa sawa ikiwa kilichonyamaziwa kipo sawa na kilichotamkwa kwa kuwa sawa katika sababu au kuwa na hukumu bora kwa nguvu ya sababu iliyopo.
Kwa watu wa Abu Hanifa, hukumu yenye kuthibiti kwa maana ya andiko haijathibiti kwa sura ya lenye kufumika kama katika ibara ya andiko, kama vile sio thabiti kwa njia ya jitihada na mtazamo ili kuwa lenye kuthibiti kiulinganishi, lakini imethibiti kwa njia ya sababu ya hukumu, na hii kwa sababu maana inayofahamika kwa tamko kilugha ni sehemu ya sababu iliyotamkwa Kisharia kwa upande wao.
Nayo ni maana inayotegemea maana ya tamko na kinachofahamika kwa mujibu wa lugha, nayo ni kimatamshi na wala si kiulinganishi, huthibiti hukumu za Ibada tofauti na ulinganishi wa kimisingi.
Ama kwa watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi na baadhi ya watu wa Imamu Hanbal wanasema, hukumu iliyonyamaziwa hufahamika kwa njia ya jitihada au ulinganishi wa Kisharia, na wala si kwa ufahamu tu wa lugha, na ulinganishi ni maana inayopatikana kwa rai na mtazamo, hivyo Wanachuoni wamejikita kwenye ufahamu wa utoaji wa rai.
Kwa maelezo hayo ni kuwa “Maana ya Andiko” kwa upande wao ni ya kulinganishwa, wakati wowote hukumu za Ibada zinapothibiti kwa “Maana ya Andiko” inafaa kusema kuwa ulinganishi umethibiti.
Zarkashy amesema: “Faida ya kutofautiana katika masuala haya ni kuwa, je hufanya kazi ya andiko? Na je hufanyiwa kazi katika adhabu na kafara?” na Ibn Najjar pia amesema: “Miongoni mwa faida za tofauti ikiwa tutasema: “Maana ya kimatamshi” inafaa kufuta, na tukisema: “Maana ya kiulinganishi haifai” ([60]).
Baadhi ya watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa wanaona kuwa kisichowezekana kupitishwa kwa njia ya ulinganishi basi kinawezekana kwa njia ya maana kwani kuwa kwake kinafahamika si sharti ([61]).
Ufafanuzi: Dalili za waliopitisha ulinganishi katika Iibada:
Wanaopitisha kufanyika ulinganishi kwenye Ibada wametumia dalili nyingi miongoni mwazo:
Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Ammar Ibn Yasir R.A. amesema: Mtume S.A.W. alinituma kwenye jambo nikawa na Janaba na sikupata maji, nikapangusa kwenye udongo kama anavyopangusa mnyama, kisha nikaja kwa Mtume S.A.W. nikamuelezea yaliyotokea, Mtume S.A.W. akasema: Kwa hakika ilikutosha kufanya kwa mikono yako kama hivi, kisha akapiga mikono yake pigo moja kwenye ardhi, kisha akapangusa kwa mkono wa kushoto mkono wa kulia, na akakunjua viganya vyake na kupangusa uso wake ([62]).
Sura ya Dalili: Ni kuwa Ummara alitumia ulinganishi kwenye Ibada ambapo alilinganisha utwahara kwa udongo badala ya maji, kama vile maji katika kuoga Janaba huenea mwilini, vile vile hulinganishwa vumbi la udongo na kuenezwa kwenye mwili.
Dalili hii imejadiliwa kuwa, haifai kwa sababu Mtume S.A.W. hakukiri, bali alimueleza kuwa kitendo chake alichofanya ni kosa, kwani ilitosha kwake kupiga mikono yake miwili pigo moja kwenye ardhi, kisha kwa mkono wa kushoto atafuta mkono wa kulia na matumbo ya viganja vyake uso wake.
Inajibiwa: Mtume S.A.W. hakumpinga Ammara kutumia kwake ulinganishi kwenye Ibada, isipokuwa alimfahamisha kuwa ulinganishi wake si sahihi, na kosa katika masuala haioneshi kubatilika hali ya ulinganishi, bali huko ni kukiri kwa Mtume S.A.W. ambapo hakupinga ulinganishi kwenye Ibada kwa kile alichokiona kwa Ammara amelinganishia, hii ikaonesha kufaa kulinganisha katika Ibada, kwa sababu haifai kuchelewesha maelezo na wakati wa kuhitajika.
Kuthibitisha hukumu za Ibada inafaa kwa Hadithi ya wapokezi wengi, vile vile inafaa kuthibitisha kwa maandiko ya wazi, hata kama njia hii ya dalili itakuwa na dhana kubwa na inafaa kukosea, pindi ilipofaa kuthibitisha hukumu za Ibada kwa Hadithi ya wapokezi wengi na uwazi wa andiko basi inafaa kuthibitisha kwa kulinganisha.
Ujumla wa dalili ni hoja ya kulinganisha, kwani zenyewe huonesha juu ya kufaa kulinganisha hukumu zote za kifiqhi, na wala haijatenganisha kati ya yanayohusu Ibada au kutendeana au mambo mengine, marejeo katika hayo ni kufahamu sababu ambayo kwa ajili yake imewekwa hukumu, wakati wowote tunapofahamu sababu katika hukumu iliyotamkwa hekima zake, na tukaikuta sababu hii katika tawi, basi inafaa kufanya Qiyasi kwa maana ya kulinganisha na kukamilisha masharti ya kulinganisha ([63]).
Uchambuzi: Dalili za wenye kuzuia ulinganishi kwenye Ibada na majibu yake:
Ibada zimekusanya mambo yanayokadiriwa yasiyofahamika maana yake, kama vile idadi ya rakaa za Swala na mafungu ya Zaka, yamekuwa ni katika mambo ya kiibada ambayo hatufahamu sababu za kuwekwa kwake, hivyo hayafanyiwi ulinganishi, kwani kulinganisha ni sehemu ya kufahamika maana, yasiyofahamika sababu zake hayalinganishwi, kwani Al-Asmandi Al-Hanafi anasema: “Dalili ya usahihi wa tuliyoyaelezea – kwa maana ya kuzuia kulinganisha katika misingi ya Ibada – kuwa kulinganisha ni kuthibitisha hukumu kwa ishara ya dhana kubwa ya kuthibiti hukumu ikiwa itapingana na akili, akili haiongozi kwenye ulazima wa Swala ya sita, na kwenye kiwango cha ngamia wa zaka kuanzia miaka mitano… haiwezekani kuthibitishwa hilo kwa kulinganisha”([64]).
Dalili hii inajibiwa: Kuwa sisi hatulinganishi katika makadirio ya ibada au mambo mengine isipokuwa pindi tunapofahamu sababu ambayo kwa ajili ya sababu hiyo imewekwa hukumu, ikiwa tutafahamu sababu katika asili ya masuala, na tukakuta sababu ni hiyo hiyo katika tawi – pamoja na kukamilika masharti yaliyobaki – tunakamilisha kazi za ulinganishi, ama ikiwa hatufahamu sababu basi hakuna tofauti kuwa haifai kulinganisha katika masuala ya mfano huo, kwa sababu imekuosekana nguzo muhimu, nayo ni sababu.
Wenye kuzuia wanaona kuwa kutumia ulinganishi katika Ibada huthibiti mwanzo wa Ibada zingine, kwa sababu hii wanazuia, mfano wa kuswali kwa ishara ya kope na yanayofanana na hilo miongoni mwa mambo muhimu yenye nukuu nyngi, lau lingekuwa jambo halali basi Mtume S.A.W. angewajibisha kulibainisha, na kunukuliwa kwetu mpaka liwe linafahamika moja kwa moja kwetu, kwa vile haliko hivyo tumefahamu kuwa kauli ya hilo ni kauli batili.
Hoja hiyo inajibiwa kuwa, kutonukuliwa hakuoneshi kutokufaa, vile vile yale mnayokosoa yanapingwa na wajibu wenu wa Swala ya witri, ambapo Swala ya witri kwenu ni wajibu na wajibu wake haujafahamika kabisa ([65]).
Makadirio yapo sawa hivyo haiwezi kuonekana akili tofauti ya kadirio na kadirio lingine.
Dalili hii inajibiwa kuwa: Sisi hatufanyi ulinganishi isipokuwa inapoonekana tofauti, ikiwa makadirio yapo sawa basi hayawezi kupewa nguvu baadhi dhidi ya mengine hivyo hakuna kulinganisha, kama Abu Hanifa alivyosema katika makadirio ya kupangusa kichwa kwa kutumia vidole vitatu kwa kulinganisha na kufuta kwenye khofu.
Makadirio ya Ibada yamewekwa kwa masilahi anayeyafahamu Mwenyezi Mungu, nayo ni haki ya Mwenyezi Mungu kama vile idadi ya Swala na idadi ya rakaa za Swala pamoja na mafungu ya Zaka, kwa vile sisi hatufahamu wala hatujui masilahi ambayo yamewekwa kwenye makadirio haya na ibada zake, wala hakuna kulinganisha katika kufahamu masilahi na haki za Mwenyezi Mungu, kisha haifai kulinganisha katika makadirio ya Ibada.
Hoja hii inajibiwa kuwa, dalili zenu hizi ni kukanusha kulinganisha katika hukumu za Ibada kunapelekea kubatilisha kutumia ulinganishi katika hukumu zote za Kisharia, na hilo ni kuwa hukumu zote zimejengwa kwa masilahi ambayo hakuna anayeyafahamu isipokuwa Mwenyezi Mungu, kwa hakika dalili hii imebatilika, na imejibiwa hoja hii wakati wa kujibu wapinga ulinganishi katika hukumu zote ([66]).
Katika maelezo yaliyotangulia inafahamika ni kwa kiwango gani kauli ya baadhi ya wanaopinga ulinganishi katika Ibada iliyodhaifu kwa kauli ya: “Hakuna ulinganishi katika Ibada, kwa sababu Ibada zimewekwa kwa Maandiko ya Qu`rani na Sunna hivyo haziwezi kuingiziwa mtazamo wala mazingatio” kwani kujengewa kwa Maandiko ya Qur`ani na Sunna hakuhusishi Ibada peke yake, bali kujengewa huko kunaendelea katika hukumu zote za Kisharia miongoni mwa Ibada mashirikiano mambo ya ndoa….n.k, kwa maelezo haya dalili ya kuzuia ulinganishi katika Ibada kwa kuwa Ibada zimewekwa kwa Maandiko ya Qur`ani na Sunna, ni maneno yasiyo kamilika.
Uchambuzi: Kutaja mifano ya ulinganisha katika milango ya Ibada adhabu kafara na mifano yake:
Tofauti na mifano iliyotangulia ya ulinganishi katika Ibada, kuna masuala mengi ya kifiqhi yanayohusu Ibada adhabu kafara na mfano wake na ambayo Wanafiqhi wametofautiana je yanalinganishwa au hapana?
Tutaeleza mifano mingi ambayo imetajwa kwenye Madhehebu manne yanayofuatwa yaliyoelezewa na Wanachuoni wa Madhehebu haya au baadhi yao kwa kufanya ulinganishi wa masuala au kutolinganisha kwa kuwa ni masuala ya kiibada, bila ya kuelezea Madhehebu mengine katika kila masuala ili kuepusha kurefusha maneno kwa kutaja mifano mingi ambayo ni dalili ya wazi juu ya mashirikiano sahihi ya Wanachuoni wa Madhehebu manne pamoja na kununi ya kufanyia ulinganishi na zile zisizofanyiwa.
Kutumika maji kwa ajili ya usafi na kuondoa uchafu pamoja na najisi:
Jamhuri ya Wanachuoni wa Madhehebu ya Imamu Shafi wanaona kuwa maji yanafanya kazi ya Twahara kuondoa uchafu na najisi, na hilo ni jambo la kiibada halifahamiki kimaana, wakati ambapo watu wa madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wanaona kuwa kuondoa uchafu na najisi ni jambo linalofahamika kimaana ambapo lengo ni kutokomeza najisi pamoja na athari zake, vyovyote itakavyotokea kwa kizuizi chochote chenye kuondoa na kung’oa maana inafahamika([67]).
Mwanamume kuzuiwa kutumia mabaki ya kujitwaharisha mwanamke:
Watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa wanaona kuwa mwanamume kuzuiliwa kutumia mabaki ya kujitwaharisha mwanamke ni jambo la kiibada halifahamika maana yake, hivyo ni halali kwa mwanamke mwingine, anaweza kujitwaharishia na uchafu najifi na yasiyokuwa hayo, kwa sababu kukatazwa ni maalumu kwa mwanamume nalo ni jambo lisilofahamika hivyo linapaswa kuishia kwa aliyekusudiwa ([68]).
Kustanji bila ya maji na kijiwe:
Jamhuri ya Wanachuoni wa – Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa Imamu Malik Imamu Shafi na Hanbal – wameelezea kufaa kustanji bila ya kutumia maji na kijiwe katika vitu visafi visivyo na uhai ([69]), tofauti na kauli ya Ibn Hazm ([70]), analinganisha na kijiwe: Kila kilichosafi katika vitu visivyo na uhai chenye kuondoa uchafu kama karatasi kitambaa na vinavyofanana na hivyo.
Andiko ambalo limekuja katika masuala haya linafahamika maana, na maana ni kujisafisha kwa kuondoa najisi, na hili linafikiwa bila ya kutumia vijiwe kama linavyofikiwa kwa kutumia vijiwe hivyo – Kwani kijiwe sio kusudio lake – hivyo inapaswa kuvuka na kufikia kila kinachofanya kazi hiyo kwa mfano: Kitambaa karatasi na mfano wake, huu ndio ukweli wa ulinganishi, ama kinyesi na mfupa limekuja andiko la kuzuia kutumika.
Je hulinganishwa nyama ya ngamia katika kuvunja udhu:
Watu wa Madhehebu ya Imamu Hanbal wanaona kuwa kula vyakula vitukufu hakuvunji udhu, ama nyama mnyama mchafu halali kwa dharura kama nyama ya nyoka kuna tofauti kwani nyama ya ngamia kutengua udhu ni jambo la kiibada wala haliwezi kuvuka kwenye nyama zingine, au maana yake inafahamika hivyo hupewa hukumu yake bali yenyewe ni zaidi ya hivyo, kauli sahihi kwao ni kuwa: Kuvunjika kwa udhu kwa nyama kula nyama ya ngamia ni jambo la kiibada ([71]).
Kulinganisha kilemba na khofu katika kufaa katika kufuta:
Wanachuoni wametofautiana kufaa kufuta juu ya kilemba kwa kuali tofauti:
Madhehebu ya Abu Hanifa wameeleza kuwa haifai kufuta juu ya kilemba, kwa sababu hakuna ugumu kukivua ([72]).
Watu wa Madhehebu ya Imamu Malik wamesema kuwa inafaa kufuta juu ya kilemba ikiwa ni muhimu, kama hofu yake ya kudhurika kichwa kwa sababu ya kuvua kilemba, kama itawezekana kufuta sehemu ya kichwa chake atafuta na kukamilisha juu ya kilemba chake ni jambo la lazima ([73]).
Watu wa madhehebu ya Imamu Shafi wamesema: Inafaa kufuta juu ya kilemba ikiwa amevaa akiwa hana udhu ni sawa sawa imekuwa ni ngumu kwake kuvua au hapana, kwa kutokuwepo amri ya kuvua, wala haitoshi kuhusisha kwenye kilemba bali hufutwa kwa vinavyofana na khofu pamoja na kilemba, kilichobora zaidi ni kutohusisha kilichochini zaidi.
Watu wa madhehebu ya Imamu Hanbal wamesema inafaa kufuta juu ya kilemba ([74]), waliopitisha wakachukua dalili ya kufaa kufuta juu ya kilemba kwa andiko na kwa kulinganisha:
Kwanza kwa Andiko: Ni Hadithi iliyopokewa kutoka kwa Mtume S.A.W. kutokana kitendo chake kufuta, miongoni mwa Hadithi hizo:
Imamu Bukhari amepokea Hadithi kwa upokezi kutoka kwa Jafari Ibn Amru Ibn Umayyah Adhamary kutoka kwa baba yake amesema: Nimemuona Mtume S.A.W. anafuta juu ya kilemba chake na khofu yake ([75]).
Imamu Muslim amepokea Hadithi kwa upokezi kutoka kwa Al-Mughira Ibn Shaaba R.A. kuwa Mtume S.A.W. alitawadha, na akafuta kwenye khofu yake na juu ya kilemba chake ([76]).
Pili kwa Kulinganisha: Na hugawanyika sehemu mbili:
Kulinganisha kilemba na khofu mbili, na sura yake ni kuwa kilemba kinafunika sehemu iliyokuja kwenye Sharia kufutwa kwake, na kupelekea uzito kukivua, basi inafaa kupangusa juu yake kama vile kupangusa juu khofu mbilli.
Kulinganisha kichwa na juu ya miguu miwili, na sura yake ni kuwa kichwa ni kiungo ulazima wake umeondoka katika kutayamamu kama vile miguu miwili huondoka ulazima wake katika kutayamamu, hivyo ikafaa kuhusisha kufuta juu ya kitu kilichofunika tofauti na kichwa, kama vile inafaa kufuta juu ya kitu kilichofunika tofauti na miguu miwili([77]).
Kuosha mkono baada ya kuamka na kabla ya kuuingiza kwenye chombo cha maji je ni jambo la kiibada:
Wanachuoni wametofautiana katika jambo hilo “Kuosha mkono baada ya kuamka na kabla ya kuuingiza kwenye chombo cha maji” je ni jambo la kiibada au linafahamika kimaana, baadhi yao wakasema: Ni jambo la kiibada hata kwa mtu aliyefikia usafi wa mkono wake akiwa amelala kwa kuufunika na nguo au kitambaa kilichosafi na akaamka, naye pia ameamrishwa kuuosha kwa ujumla wa amri ya mwenye kuamka, nayo ni moja ya sura mbili kwa mtazamo wa Imamu Shafi, nalo ni jambo linalofahamika kwenye Madhehebu ya Imamu Malik kuwa ni Sunna hata kama atakuwa na uhakika wa usafi wa mkono wake, na kuonekana sura mbili kwa Madhehebu ya Imamu Shafi – kama Raafi alivyosema – kuwa haichukizi kuingiza mkono kwenye chombo cha maji kwa mwenye kuamka hata kama atakuwa na uhakika usafi wa mkono wake, kwa sababu amri ya hilo ni kutokana na uwezekano wa kupata uchafu kwa dalili ya kauli ya Mtume S.A.W. mwishoni mwa Hadithi: “Kwani hawezi kufahamu mkono wake ulilala wapi” amri imekuwa na sababu ya uwezekano wa mkono wake kupata uchafu. Mwenyezi Mungu Anajua zaidi
Hivyo imeelezwa kuwa hilo linafahamika maana, na Sharia imeashiria sababu ya hilo kwa kauli yake: “Kwani hafahamu mkono wake ulilala wapi” kumekuwa na tofauti katika sababu ya hilo Imamu Shafi R.A. akasema: Maana yake ni kuwa watu wa Hijazi walikuwa wanastanji kwa kutumia vijiwe na nchi yao ilikuwa na joto kali, mmoja wao anapolala hutokwa na jasho hivyo mwenye kulala hana uhakika mkono kupita kwenye maeneo machafu au tofauti ya hayo, na Abu Waliid Al-Baaji amesema: Wametofautiana katika sababu ya mwenye kuamka kuosha mkono, Ibn Habibi akasema: Huenda akawa amegusa najisi iliyotoka kwake bila ya kujua au kugusa uchafu, na ikasemwa: Ni kwa sababu wengi wao walikuwa wakitumia vijiwe, huenda mtu akagusa athari ya uchafu kwa mkono wake, akasema: Hilo halipo wazi sana, kwa sababu najisi mara nyingi hazitoki bila ya kufahamu mtu mwenyewe, na asiyefahamu basi hana hukumu, na sehemu ya kutumia kijiwe mkono wa mtu aliyelala haupafikii isipokuwa kwa kukusudia hilo, na kama ingekuwa kuosha mikono miwili ili kuhalalisha hilo basi angeamrishwa kuosha nguo kwa kufaa hilo, akasema: Kilichowazi zaidi ni kile kilichoelezwa na watu wa Iraq miongoni mwa watu wa Imamu Malik na wengine kuwa, mwenye kulala mkono wake hauachi kujikuna mwili wake na sehemu ya jasho lake na maeneo mengine hivyo ikasuniwa kwake kuosha moja kwa moja mkono wake([78]).
Je kuosha maiti ni jambo la kiibada?
Imamu Hanbal ameeleza kuwa kuosha maiti ni jambo la kiibada halifahamiki maana yake, lakini wao wametofautiana katika hukumu ya baadhi za masuala, miongoni mwayo: Ikiwa atatokwa na kitu baada ya josho la tatu, kauli iliyosahihi ya Madhehebu ni kuwa ataoshwa mara tano, ikiwa atatokwa na kitu baada ya hapo ataoshwa mara saba, wala hakuna zaidi ya hapo, Abu Al-Khattwabi na Ibn Aqiil wamesema: Si lazima kurejea kuoshwa baada ya josho la tatu bali ataoshwa ile najisi na kutawadhwa ([79]).
Watu wa Imamu Malik wametofautiana, kauli maarufu ni jambo la kiibada, na wala si la usafi, ikasemwa: ni jambo la usafi, na faida ya tofauti inaonekana kwao pindi Muislamu anapofariki na ikawa hakuna Muislamu bali kuna mtu wa dhimmiy, hivyo kauli kuwa ni jambo la kiibada mtu dhimmiy hamuoshi, kwa sababu si katika watu wa Ibada, na kauli ya kuwa ni jambo la usafi basi mtu dhimmiy anaweza kumuosha ([80]).
Watu wa Imamu Shafi pia wametofautiana: Baadhi yao wamesema: Hilo si jambo lenye kufahamika, bali limefanywa ili kufuata Sharia, na wengine wakasema: Bali linafahamika maana, mwenye kusema hivi ametofautiana katika maana yake kwa sura mbili: Ya kwanza: Ni kuwa maana ni maiti kuwa na uchafu, kuoshwa kutokana na uchafu ni katika mambo yaliyosuniwa kwake ikiwa mkavu, na jambo la lazima akiwa na maji maji. Sura ya Pili: Ni kuwa maana iliyopo ni kumuheshimu maiti kama inavyolazimishwa kutawadha kwa kugusana na mwanamke waliohai kutokana na heshima zao na kufika kwa maiti kwa ukamilifu wa usafi ([81]).
Usafi: Ni jambo la kiibada kwa kutumia maji tu ili kuondoa uchafu bila ya kuondoa najisi kwa upande wa Imamu Abu Hanifa:
Amesema katika kitabu cha Al-Inayaah: “…. Haifai kwa kilichokamuliwa kwenye mti na tunda” kwa sababu si maji moja kwa moja, na hukumu wakati wa kukosekana kwake hupelekea kwenye kutayamamu, na kazi katika viungo hivi ni kiibada hivyo haiwezi kufanyika sehemu isiyotamkwa.
Ama maji yanayodondoka kutoka kwenye zabibu yanafaa kutawadhia, kwa sababu ni maji yanatoka si kwa kukamua, yametajwa kwenye kitabu cha Jawaamii cha Abu Yusuf R.A, na kauli yake: “Ni kwa sababu sio maji halisi” kwa sababu yanapotajwa maji yenyewe hayatajwi, na kufikiwa hilo ikiwa tutapiga mfano ndani ya jumba la mtu kuna maji ya kisima au maji ya bahari au maji ya chemchem au maji yaliyokamuliwa kwenye mti au matunda kisha akaambiwa mwenye nyumba: Lete maji basi kutakuwa akilini mwa mwenye kuambiwa isipokuwa haya maji ya kwanza, wala hatumaanishi maji halisi au maji ya sharti isipokuwa aina hizi, na hukumu yenyewe ni Twahara pindi yanapokosekana maji halisi,kwa maana: Kukosekana maji halisi (Hupelekea kutayamamu) Mwenyezi Mungu Amesema: {Na msipate maji, basi ukusudieni mchanga} [An-Nisaa: 43….] Mwelekeo wake ni kuwa kufanya kazi kwenye viungo hivi ni jambo la kiabada wala haipelekei kwenye jambo lisilotamkwa, maana yake ni kuwa sharti la kulinganisha hukumu asili isiwe mbali na ulinganishaji, tofauti na kuondoa najisi yenyewe inafahamika maana ya uwepo wake kwa kuonekana basi inafaa kukutanishwa na kauli ya Imamu Abu Hanifa na Abu Yusuf.
Twahara: Kutawadha je ni jambo la kiibada?
Kauli kuwa kutawadha ni jambo la kiibada ni kauli dhaifu, lakini kauli inayokubalika kuwa ni jambo lenye maana inayofahamika, kwa sababu Ibada ya Swala ni kuzungumza na Mola Mtukufu hivyo kunahitajika usafi kwa ajili ya hilo, lakini kumehusishwa kupangusa kichwa kwa vile mara nyingi ni chenye kufunikwa, hivyo inatosha kwa usafi wowote mdogo tu, na viungo vinne vimehusishwa na kutawadhwa kwa sababu ni sehemu ya kuchumia dhambi([82]).
Kulinganisha najisi ya nguruwe kwa najisi ya mbwa:
Sheikh Al-Jamal Al-Shafi amesema: “Kulinganishwa najisi ya mbwa na najisi ya nguruwe kwa watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi, imepokewa kwao kuwa kuhusishwa idadi ya uoshaji wa mara sababu na sharti la kufuata mpangilio ni mambo ya kiibada, na mambo ya kiibada hayana ulinganishi. Hoja hii imejibiwa kuwa kulinganisha katika asili ya najisi ikiwa imethibiti basi italazimika kuosha mara saba kwa kutumia udongo, na Ibada ya Imamu Al-Mahilly: Pima na linganisha juu ya kulamba kwake ni kama mkojo wake na jasho lake, kwa sababu ikiwa inawajibisha kwa yaliyotajwa katika mdomo wake pamoja na kuwa ni sehemu safi zaidi kutokana na kubwekea kwa wingi basi kwa vitu vingine ni najasi zaidi, na kauli yake “Kwa sababu ikiwa ni lazima” mpaka mwisho, ni ishara kuwa kulinganisha kwa upande wa hukumu kwa najisi na ikathibiti basi lazima kuosha mara saba kwa kutumia mchanga ambapo hakuna tofauti kati ya kinyesi chake basi yamedondoka yaliyosemwa hakuna kulinganisha katika mambo ya kiibada”([83]).
Kuleta Takbiira katika Ibada ya Swala hakulinganishwi:
Watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi wanaona kuwa Takbira katika Swala ni maalumu isiyofahamika maana, hivyo haiwezi kulinganishwa na kitu kingine, na watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa wanaona kuwa, maana ya Takbira inafahamika nayo ni kumtukuza na kumkuza” ([84]).
Wajibu wa Swala kwa kuashiria kwa kope:
Hilo ni kwa mwenye kushindwa kutekeleza Swala kwa kulinganisha na wajibu wa kuswali kwa kukaa kwa mwenye kushindwa kusimama, au kuashiria kwa kichwa chake pia kwa mwenye kushindwa, wote hao tamko kwao limekuja katika hali ya kushindwa, nalo ni: Kushindwa kuitekeleza Swala kwa ukamilifu wake ([85]).
Makubaliano ya Wanafiqhi kuwa mwenye kuswali ikiwa atashindwa kusimama ataswali kwa kukaa, ikiwa hawezi kukaa basi atalala ubavu kwa kuashiria kwa kichwa, kisha watu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa wakatofautiana na Jamhuri ya Wanafiqhi kuhusu kushindwa kuashiria kwa kutikisa kichwa chake je anapaswa kuashiria kwa kope au jicho lake au hapana?
Kauli inayotegemewa katika Madhehebu ya Imamu Malik na Imamu Shafi ni wajibu wa kuashiria kwa kope ([86]), na kwa upande wa Madhehebu ya Imamu Hambali, ikiwa atashindwa kuashiria kwa kichwa ataashiria kwa upande wake, kwa maana ya jicho lake, Mwanachuoni Al-Bahuuty anasema: Ahmad Amesema: Lazima afanye kitu huku akijatambua, na katika kitabu cha Attabswarah: Ataswali kwa moyo wake, au kwa jicho lake, na katika kitabu cha Al-Khilafu: Ataashiria kwa jicho lake na kope zake, au kwa moyo wake…. Kwani Swala haiondoshwi kwa mgonjwa madamu akili yake ni yenye kuthibiti kwa uwezo wake wa kuashiria kwa jicho lake pamoja na nia kwa moyo wake ([87]).
Kwa vile ameshindwa kuihudhurisha akili na kufahamu cha kuzungumza pamoja na uwepo sababu za wajibu, na kufaa kupata dhambi basi Swala inalazimika kwake, wala amri ya Swala haiondoki, wakati ni mwenye uwezo wa kuashiria kwa kichwa chake basi ataitekeleza vile awezavyo, na hilo ni kwa dalili ya kauli ya Mtume S.A.W.: “Pindi ninapowaamrisha jambo basi litekelezeni vile muwezavyo” ([88]).
Imenukuliwa kutoka kwa Zafar na Hassan Ibn Ziyad katika watu wa Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa, nao ni upokezi kutoka kwa Abu Yusuf kuwa anapaswa kuashiria kwa kope zake au jicho lake, Zafar akachukua dalili kuwa Ibada ya Swala ni faradhi ya kudumu haiondoki isipokuwa kwa kushindwa, kile atakachoshindwa kukitekeleza kinaondoka na anachoweza atalazimika nacho kwa uwezo wake, ikiwa ataweza kwa kutumia kope zake mbili basi kuashiria kwa kope hizo ni bora zaidi, kwa sababu kope zipo karibu zaidi na kichwa, ikiwa atashindwa ataashiria kwa macho yake, kwa sababu hayo macho ni katika viungo vya wazi, na mwili wote una nafasi katika Ibada hii na vile vile macho mawili, ikiwa atashindwa basi ataileta kwa moyo wake, kwa sababu moyo ni katika jumla ya sehemu ya Ibada hii nayo ni nia, na nia ni sharti la kufaa kwake, pindi anaposhindwa huielekea kwa moyo wake ([89]).
Kilichopitishwa kwenye Madhehebu ya Imamu Abu Hanifa ni kuwa, mwenye kuswali ikiwa atashindwa kuashiria – wala kuashiria kwao hakuwi isipokuwa kwa kutikisa kichwa, ama kutikisa jicho na kope kunaitwa kuashiria ([90]) – basi hana anachowajibika nacho, wakachukua dalili za Hadithi zinazoonesha kuwa mgonjwa mbele ya Mwenyezi Mungu amesamehewa katika hali hii, lau atalazimika kuashiria kama ilivyotajwa asingekuwa mwenye kusamehewa, kwa sababu kuashiria si Swala kwa hakika, kwa sababu hiyo haifai kuswalia Swala ya Sunna, lau ingekuwa Swala ya lazima ingefaa, kama angeswali Swala ya Sunna akiwa amekaa, isipokuwa huko kukaa kunachukua nafasi ya Swala Kisharia, na Sharia imeelezea kuashiria kwa kichwa hivyo haiwezekani kwa kiungo kingine, na nafasi ya kuleta rai mbadala ([91]) kunazuiliwa wala hakuna kulinganisha na kichwa, kisha ikiwa itaondoshwa Swala kwake kwa hukumu ya kushindwa basi ikiwa atafariki kutokana na hayo maradhi atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa hakuna jambo lolote kwake, kwa sababu hakupata muda wa kulipia Swala ([92]).
Kiwango cha kuhitaji kwao kutothibiti Ibada ya Swala kwa kuashiria kwa kope kunafungamana na kuwa kwake Swala ya nje ya jumla ya Swala Kisharia zilizothibiti kwa Sharia, na ambazo zinafahamika kuwa za kiibada, hivyo haifai kuzithibitisha kwa kulinganisha.
Wanajibiwa kuwa sisi tunazuia masuala ya Swala kuwa kuashiria kwa kope kunapelekea wajibu wa Swala nyingine zaidi ya Swala tano za Kisharia, bali sisi tunazingatia ni katika jumla ya matawi yanayotokana chini ya asili katika asili, wala hatuoni kizuizi cha tawi kulipa hukumu ya asili wakati itakapoonekana sababu ya asili, sababu hii imefikiwa katika tawi.
Kwa hakika Swala hii ni Swala iliyoandaliwa ya ahadi ambayo inafahamika kupokewa kiibada, kwa hakika vitendo vyake vingine vya Swala vinaondoka kwa udhuru, vilivyobakia vinavyowezekana ni wajibu, hapa kulinganisha si kuthibiti kwa Swala mpya, bali kubakisha wajibu, vile vile kutoondolewa hakuoneshi kutokufaa ([93]).
Swala: Kurukuu na kusujudu ni amri ya kiibada:
Imesemwa kwenye kitabu cha Majmaa Al-Anhaar: “Kurukuu” nako ni kuinama, na “Kusujudu” nako ni kuweka paji la uso au pua juu ya ardhi kwa njia ya unyenyekevu kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Rukuuni na msujudu} [Al-Hajji: 77], kusudio la kusujudu ni zile sijida mbili, kwa sababu jina maalumu huonesha idadi ya Maimamu wa Kiarabu isipokuwa ni tofauti na yale waliyoyafikia Wanachuoni wetu, na Masheikh wetu wahakiki wamesema: “Ni amri ya kiibada haifahamiki maana yake” ([94]).
Wajibu wa Zaka ya madini yanayochimbwa:
Wanachuoni wametofautiana katika masuala haya kwa kauli tatu:
Watu wa Madhehebu ya Abu Hanifa wamesema kuwa madini yote yaliyochimbwa ardhini ambayo huchomeka kwa moto – kwa maana yanayayuka kwa moto – yanapaswa kutolewa Zaka, ama madini yanayochuruzika au yasiyochuruzika ambayo hayachomeki kwa moto kwa upande wao hayana Zaka, isipokuwa wamesema hivyo ikiwa ni kulinganisha madini ya dhahabu na fedha ambayo yamethibiti wajibu wa Zaka kwenye madini hayo kwa andiko na kwa makubaliano ya Wanachuoni, hivyo hulinganishwa na madini hayo yale yaliyofanana nayo, na hayo ndio katika madini yanayoyayuka kwa moto([95]).
Wakawajibisha kutolewa sehemu ya tano, na wakachukua dalili kutoka ndani ya Qur`ani Sunna na Qiyaas, wakalinganisha madini na hazina, kwa zote kuthibiti ngawira kila moja.
Watu wa Madhehebu ya Imamu Malik na Imamu Shafi wamesema kuwa madini yaliyochimbuliwa ardhini ikiwa ni madini ya dhehebu na fedha kunawajibika kutolewa zaka, ama madini yasiyokuwa hayo hayana zaka ([96]), Imamu Annawawi amesema: “Dalili yetu: Ni kuwa asili ni kutokuwa wajibu, na imethibiti katika dhahabu na fedha kwa makubaliano ya Wanachuoni, hakuna wajibu kwa madini yasiyokuwa hayo isipokuwa kwa dalili ya wazi” ([97]).
Watu wa Madhehebu ya Imamu Hanbal wameelezea wajibu wa kutolewa Zaka kila madini yanayochimbwa ardhini ambayo yanathamani, ni sawa sawa madini ya chimbwa yakiwa ni yenye kuyayuka kwa moto au si ya kuyayuka, au katika madini yanayochuruzika kama vile mafuta ya petroli dizeli na sulfuri, kila kinachoitwa jina la madini ndani yake kuna zaka ([98]).
Watu wa madhehebu ya Imamu Hanbal wamechukua ya kuingia kila kinachochimbwa ardhini kuanzi madini magumu au ya maji ni katika madini yanayopaswa Zaka kwa ujumla wa kauli ya Mwenyezi Mungu: {Na katika vile tulivyo kutoleeni katika ardhi} [Al-Baqarah: 267]. Inaonesha juu ya kukusanya vyote vinavyochimbwa ardhini.
Kwa kulinganisha: Madini kwa upande wa lugha inakusanya madini yote, hufungamana na Zaka yanayochimbwa ardhini kama vile dhahabu na madini ya fedha, vile vile yenyewe ni mali lau yatapatikana kwenye vita ni lazima kutolea Zaka moja ya sehemu ya tano, ikiwa yatachimbwa miongoni mwa madini inapaswa kutolewa Zaka kama vile madini ya dhahabu ([99]).
Kulinganisha vyakula vyote vilinavyotolewa Zaka ya Fitri:
Miongoni mwa mifano ya kulinganisha ambayo imefanywa na Wanafiqi katika masuala ya Zaka: Ni kuwa Mtume S.A.W. ameweka Sharia ya kutoa Zaka ya Fitri kwa baadhi ya nafaka na matunda kama vile ngano tende na zabibu, watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi wakalinganisha na kila kinacholiwa, au chakula kikuu cha mji au nchi, au chakula kikuu cha mtu mwenyewe, wala hawakufanya jinsi hizi zilizochukuliwa kukusudiwa zenyewe kiibada hivyo hakuna kuzilinganisha ([100]).
Kukataza kuuza chakula kabla ya kuwa nacho je jambo la kiibada:
Baadhi ya watu wa Madhehebu ya Imamu Malik wametaja katika kauli yake S.A.W.: “Mwenye kununua chakula asikiuze mpaka akijaze”, katika mapokezi mengine: “Mpaka kikamilike” na mapokezi mengine: “Mpaka akimiliki” ([101]), wametofautiana kwa upande wa uharamu ikasemwa: Kiibada, na ikasemwa: Kuna sababu kuwa lengo la Sharia ni kurahisisha kukifikia chakula, ili kumfikie mtu mwenye nguvu na mnyonge ([102]).
Kulinganisha mchimbua makaburi na mwizi:
Watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi wanaona kulinganisha mchimbua makaburi na mwizi katika wajibu wa kukatwa mkono kwa wote kuchukuwa mali za wengine kwa kujificha ([103]), wakalinganisha hilo na mlango wa adhabu.
Kulinganisha muuaji wa makusudi katika wajibu wa kafara:
Watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi wanaona kulinganisha muuaji wa makusudi na muuaji kwa makosa katika wajibu wa kafara kwa mauaji yote ni kinyume na haki ([104]), wakalinganisha hilo katika mlango pia wa adhabu.
Kugharamia: Kulinganisha kumgharamia mke na kafara:
Watu wa Madhehebu ya Imamu Shafi wanaona kulinganisha kugharamia mke na kafara katika kukadiria kwake kwa mtu mwenye uwezo kwa vibaba viwili kama katika fidia ya Hija, na asiye na uwezo kibaba kimoja kama vile katika Kafara, vyote hivyo viwili ni mali ya lazima kwenye Sharia na inakuwa katika dhima ya mtu, asili ya tofauti ni kutokana na kauli ya Mola Mtukufu: {Mwenye wasaa atoe kadiri ya wasaa wake} [Atwalaq: 7].
Katika Eda za wanawake ni za kiibada na zingine zinafahamika maana:
Al-Baaly Al-Hambali amesema: “Neno Eda limetokana na idadi, kwa sababu nyakati za Eda ni idadi za nyakati na hali kama vile hedhi na miezi, makusudio yake mara nyingi ni kufahamu kutokuwepo kwa mtoto tumboni, nayo Eda inagawanyika sehemu nne: Eda kiibada kama vile Eda ya kifo, au Eda inayokutana na mambo mawili sehemu kubwa ni ibada, kama vile mke aliyefiliwa inawezekana mimba yake pindi zikipita siku zake ndani ya miezi, na kinyume kama vile Eda ya mke aliyeingiliwa ambaye inawezekana ujauzito wake ni katika anayezaliwa wa mfano wake, nayo ni kusubiri muda mdogo Kisharia, hakuna Eda ya lazima mume aliyehai anapomuacha mke kabla ya kuingilia na kabla ya kuwa siri kati yao wala kumbusu wala kumgusa”([105]).
Kuchinja: Kwa kutumia mfupa:
Katika Madhehebu ya Imamu Shafi imekatazwa kuchinja kwa kutumia mfupa, ikasemwa: Ni jambo la kiibada, na kauli hiyo imechukuliwa na Ibn Swalah amesema: “Baada ya utafiti sijakuta Mwanachuoni yeyote ametaja kwenye hilo kuna maana inayofahamika, kana kwamba kwao ni jambo la kiibada”, na yamesemwa hayo pia na Ibn Abdilsalaam, na An-Nawawi akasema katika sherhi Muslim: Maana yake msichinje kwa kutumia mfupa kwani wenyewe hunajisi kwa damu ([106]).
Hitimisho:
Katika maelezo yaliyopita yamekuwa wazi kuwa kanuni ya (Hakuna ulinganishi katika ibada) haifai kutumika moja kwa moja, kwa sababu kutumika kwake kunaitoa kwenye wigo wa Fiqhi na kiasili ambako kunazungumziwa na Wanachuoni, pia tumetaja tofauti za Wanachuoni katika sababu za ibada na ulinganisho wake kwenye Madhehebu mbili.
Tumetaja masuala mengi ambayo yameelezewa na Wanachuoni wa Madhehebu manne au baadhi yao kufanyika ulinganishi wa masuala kwa kuwa kwake yanafahamika kimaana, au kutofanyika ulinganishi kwa kuwa kwake ni masuala ya kiibada.
Katika wigo huu yanabainika yanayowezekana kuchambuliwa kifiqhi na Wanachuoni wengi wa sasa katika kuzuia matumizi ya kanuni (Hakuna ulinganishi katika Ibada) kwa kutozingatia masuala je ni yenye kufahamika maana au hayafahamiki, kumepelekea makosa ya utakelezaji wa kanuni hii katika rai na mitazamo mingi ya kifiqhi kinyume na mfumo sahihi wa kifiqhi ambao umekuwa kwa Maimamu wa Umma, na kuna mifano mingi ambayo inawezekana kuitaja kwenye hili, na baadhi yake tutafupisha ili kuona kiwango cha usahihi na makosa ya utekelezaji wa kanuni hii:
Kuadhimisha mazazi matakatifu ya Mtume S.A.W.: Maadhimisho haya yamepingwa kuwa ni Ibada, kwani asili ya ibada yenyewe ni amri, na wala haipatikana amri ya kuadhimisha kuzaliwa kwake.
Jibu – kama alivyotaja Imamu Suyuutwi – kuwa utekelezaji wa Suala la Sunna wakati mwingine huwa kwa andiko, na wakati mwingine huwa kwa ulinganishi, na kuadhimisha mazazi matakatifu hata kama halijapokewa andiko lakini ndani yake kuna ulinganishi kwa asili mbili, Imamu Hafidh Ibn Hajar Al-Asqlaaniy ametaja moja, na Imamu Suyuutwi ametaja nyingine, na asili ya kukusanyika ili kuonesha alama za mazazi ni jambo la Sunna na ukaribu, na yanayopatikana ndani yake baadhi ya mambo mabaya kama vile mchanganyiko haramu ni jambo la dhambi lenye kuzuiwa, kama wakati mwingine inavyotokea wakati wa watu wanapokusanyika katika Swala ya Tarawehe au Swala ya Eid katika eneo la uwanja wa wazi, hatuzuii kukusanyika kwao kwa sababu ya mambo haya ambayo yamelinganishwa nayo, bali tunasema: Asili ya mkusanyiko kama huu ni alama ya Sunna na ukaribu, na maelezo kuwa kuadhimisha mazazi matakatifu ni ukaribu, ulinganishi juu ya asili kuu ya Sharia ni kuhimiza kuonesha kushukuru neema, na kuhimiza kusubiri kukaa kimya na kuficha mambo wakati wa matatizo, ambapo Sharia imeamrisha Aqika baada ya kuzaliwa mtoto ikiwa ni kuonesha shukrani na furaha kwa kupatikana mtoto, wala Sharia haikuamrisha mfano wa hivyo wakati wa kifo, bali imekataza kupiga kelele na kuonesha kuchoshwa, kanuni ya Sharia ikaonesha kuwa hufanywa vizuri ndani ya mwezi wa mfungo sita kuonesha furahi kwa kuzaliwa kwake S.A.W. bila ya kuonesha huzuni kwa kufariki kwake.
Al-Hafidhi Ibn Hajar amesema: “Imedhihirika kwangu kutokana kwake na asili iliyothibiti, nayo ni yaliyothibiti katika Sahihi mbili kuwa Mtume S.A.W. alifika Mji wa Madina na akawakuta Wayahudi wanafuga siku ya Ashura, akawauliza na wakasema: Hiyo ni siku Mwenyezi Mungu alimuangamiza Firauni, na kumwokoa Musa, basi sisi tunafunga ikiwa ni kumshukuru Mwenyezi Mungu…..” hufahamika hilo kitendo cha kumshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema aliyoneemesha siku maalumu au kuondoa adhabu, na hurudiwa hilo siku kama hiyo kila mwaka, na kumshukuru Mwenyezi Mungu kunapatikana kwa aina za Ibada kama vile kusujudu kufunga kutoa sadaka kusoma Qur`ani, kuna neema gani kubwa kuliko neema ya kumtangaza Mtume huyu S.A.W. na kutokana na hili inapaswa kuangaliwa siku hiyo ili kuendana na kisa cha Musa A.S. ndani ya siku ya Ashura…. Ama yanayofuatana na hilo miongoni mwa yanayosikika michezo na mengine inapaswa kusemwa: Hayakuwa hayo halali kwa sababu yanapelekea furaha kwa sababu ya hiyo siku, hakuna ubaya kuyafanya, na yaliyokuwa haramu au kuchukiza huzuiliwa, vile vile na yaliyokuwa tofauti na ya kwanza” ([107]).
Kuainisha siku ya fulani kutembelea makaburini: Kuainisha huku ni jambo linalofaa, Al-Hafidh Ibn Hajar amechukua dalili ya kufaa kwake kuwa Mtume S.A.W. alikuwa akitembelea Qubaa kila siku ya Jumamosi ([108]). Hili limepingwa kuwa halifai kulinganishwa, kwani hii ni Ibada haifai kulinganishwa Ibada, na jibu la upingaji huu lipo wazi katika maelezo yaliyotangulia.
Kuna masuala mengi ambayo yanaleta maswali mengi miongoni mwa hayo: Kama vile kumpa maiti thawabu za usomaji Qur`ani na isiyokuwa hiyo katika matendo mema, na kama kufanya Tawasuli kwa Mtume S.A.W. na kwa waja wema pamoja na kupata baraka kwa athari zao, na kama vile kutamka nia, na kutukuza utajo wa Mtume S.A.W. kwa tamko la Sayyid, na kumpa thawabu za matendo mema -wamezuia waliozuia pasi na usahihi – yote haya yanatokana kuwa mambo haya ni katika Ibada hayana ulinganishi.
Tumefahamu kupitia utafiti huu kuwa matumizi ya kanuni hii si sahihi, na haipaswi kufanyiwa haraka katika utekelezaji wa kanuni hii, bali ni lazima katika kila masuala kuyaangalia je yenyewe ni katika yanayofahamika maana yake au yasiyofahamika maana yake, kwa hilo ni lazima kuangaliwa kifiqhi kila masuala peke yake, na kukusanya dalili za Kisharia pamoja na kuangalia katika yanayofanana nayo na kuzingatia maana zake na sababu zake pamoja na hekima zake.
Mwenyezi Mungu Mtukufu ni Mjuzi zaidi
Imeandikwa Na:
Mustafa Abdillah Abdulhamid:
Mtafiti kitengo cha tafiti za Kisharia.
Iswaamu Anas Zaftawi:
Mtafiti kitengo cha tafiti za Kisharia.
Mnamo tarehe: 04/08/2008.
Imerejewa Na:
Iswaam Anas Zaftawi:
Mtafiti kitengo cha tafiti za Kisharia.
Aliyepitishwa kusambaza:
Prof. Abdillah Rabii Abdillah: Muhadhiri wa masomo ya Usuul- Alfiqhi Chuo Kikuu cha Al-Azhar.
([1]) Rejea kamusi ya LIsaanul-Araby na kamusi ya Al-Muhit, na Misbahul-Munir. Na angalia sherehy ya Mukhtasar Ibn Al-Hajib, Adhdu Deen Al-Iijy, 3/279, na kitabu cha Nihayatul-Suul sherehe ya Minhaajil-Wusuul, Jamaludeen Ai-Isnawy, 4/2, na Qiyasi kwa watu wa Usuuli Dr. Ally Jumaa, uk. 31, na kitabu cha Rakhasu Sharia wa ithbaatiha bil-Qiyaas, Dr. Abdulkareem Annimla, uk.148: 149.
([2]) Angalia kitabu cha Nihaaytul-Suul, sherehe ya Minhajil-Wusuul, cha Jamalu Deen Al-Isnawy pamoja na Hashiyatu Al-Mutii, 4/2.
([3]) Angalia kitabu cha Taajul-Aruus, cha Murtadha Zubaidy, 8/331.
([4]) Kitabu cha Al-Huduud Al-Aniiqah wa Taarifaati Daqiiqa cha Zakaria Al-Ansaary, uk. 77.
([5]) Kitabu cha Raddul-Muhtaar Alaa Darri Al-Mukhatar cha Ibn Aabideen, 1/72, na angalia pia kitabu cha Al-Huduud Al-Aniiqah cha Zakaria Al-Ansary, uk. 77.
([6]) Kuna mambo hukusanya maana ya ibada na zengine mfano wa kafara, nayo ni miradi inayozunguka kati ya ibada na adhabu, ama kukusanya kwake maana ya ibada yenyewe hutekelezwa kwa kufunga na mfano wake kama vile kutoa sadaka na mfano wake kama kutoa sadaka, na huwekewa sharti ya nia ya kafara katika utekelezaji wake.
Ama kukusanya kwake maana ya adhabu, ni kwamba haikulazimika kwa kuanzia kumtukuza Mwenyezi Mungu kama vile ibada nyengine, bali imewajibishwa adhabu ya jinai kwani yenyewe imewekwa kwa kutishia, nayo hukusanya pia maana ya kuabudu kutokana na yaliyomo miongoni mwa adhabu zilizokadiriwa kwa upande wa Sharia.
Angalia kitabu cha: Al-Mustasfii cha Imamu Ghazaly, 2/324, na kubaini ukweli wa sherehe ya kitabu cha kanzu Daqaaiq cha Zailii, 3/108, na uwiano katika ibada cha Muhammad Mandhur, uk. 421.
([7]) Kitabu cha Haashiyatu Sharbiiny, Sharehe ya kitabu cha Jamuu Al-Jawaamii, 2/136,
([8]) Hapa kusudio la misingi ya hukumu: Milango mikuu ya Fiqhi kama vile Sala, Funga, Zaka, Hija …n.k.
([9]) Kitabu cha Taqwiimul-Adillah cha Dabuusy, uk. 301, kitabu cha misingi ya Fiqhi cha Sarkhasy 2/144, na kitabu cha Bahrul-Muhit, 6/390.
([10]) Kitabu cha Al-Muraafiqaat, 3/46.
([11]) Rejea: Kamusi elezo ya Fiqhi chapa ya Kuweit, 12/201: 214.
([12]) Kitabu cha Al-Faruuku cha Al-Qurafi, 3/493. Katika jambo la ajabu limesemwa kuhusu jambo hili: Ikiwa Mwanafiqhi atashindwa kuleta sababu ya hekima husemwa: Amri hiiyo inakuwa ya kutekelezwa tu, akishindwa upande wa sarufi husemwa: Hili lipo, akishindwa kwa upande wa hukumu husemwa: Hili ni jambo maalumu. Kitabu cha Al-Ashbaha wannadhwahir cha Imamu Assuyutiy, 2/245.
([13]) Kitabu cha Al-Furuuqu cha Al-Qurafi, 3/165.
([14]) Imenukuiliwa kwenye kitabu cha Mawaahibu Al-Jaliil, 1/256.
([15]) Kitabu cha Raddul-Mukhtaar cha Ibn Aabidiin, 1/438.
([16]) Al-Bujairamy alaa Al-Khatib, 2/175.
([17]) Sherehe ya kitabu cha Al-Kaukabu Al-Munir, 2/411.
([18]) Angalia kitabu cha Al-Qiyaasi fil Ibaadati, uk. 267.
([19]) Tunakuta baadhi ya Wanachuoni wanajaribu kufanya jitihada katika kutafuta hekima kwa mfano idadi ya rakaa za Sala, pamoja na Wanachuoni wengi wamesisitiza kuwa hilo halina maana na yenyewe ni amri tu ya kutekelezwa, Mwanachuoni mmoja anajaribu kufanya Jitihada ili kufikia hekima yake. Sheikh Al-Bujairamy anasema: Hekima ya Sala za lazima kuwa na rakaa kumi na saba na wakati wa mtu kuwa macho kwa siku ni masaa kumi na saba masaa kumi na mawili ya mchana, kiasi cha msaa matatu wakati wa Magharibi na masaa mawili wakati wa Al-Fajiri, hivyo kufanya kufanya kila saa rakaa moja ikiwa kuziba mapungufu yanayotokea na hekima ya kuhusisha Sala hizi tano na wakati huu usiofahamika hekima, kama Wanachuoni wengi walivyosema na wengine kuonesha hekima zake, katika hekima iliyo nzuri zaidi ni kumkumbusha mwanadamu wakati wa kuzaliwa kwake kama vile kuchomoza kwa jua na kukuwa kwake kama kunyanyuka kwa jua, na ujana wake kama kusimama kwa jua eneo la kati kati, na utu uzima wake ni kama jua kukaribia kuzama, kifo chake ni kama jua kuzama, na kuoza kwa mwili wake ni kama kufutika athari za jua kwa kuondoka mawingi mekundu na kuja wakati wa Isha, wakati huo ni ukumbusho kama vile ukamilifu wake tumboni na kuandaliwa kutoa kama vile jua kuchomoza Al-Fajiri ambayo ndiyo utangulizi wa jua kuchomoza na wakati huo asubuhi kuingia, na hekima ya Sala ya Al-Fajiri kuwa na rakaa mbili ni kutokana na kubakia kwa uchovu na uvivu, Sala za mchana kuwa na rakaa nne nne ni kutokana na kuimarika kwa uchangamfu ndani ya nyakati hizo, maana wakati wa adhuhuri na wakati wa Al-Asri, na Sala ya Magharibi kuwa na rakaa tatu ni kwa sababu ipo mwisho wa mwa mchana, wakati wa Sala ya Isha imekutana na nyakati mbili za mchana kwa maana wakati wa adhuhuri na alasiri ili kuunganisha usiku na mchana ambapo ndani yake kuna Sala mbili za faradhi na wakati wa mchana kuna Sala tatu za faradhi ili nafsi kuwa na harakati zenye nguvu zaidi.
Al-Bujairimi kwenye kitabu cha Al-Minhaaji 2-132 – 133.
([20]) Kitabu cha Al-Qiyaasi fil Ibadati, uk. 308.
([21]) Rejea kitabu cha: Nihayatul-Muhtaaji cha Shabramalsy, 15/71.
([22]) Kitabu cha Kashfu Al-Mukhaddarati cha Baaly madhehebu ya Hanbal, 1/447.
([23]) Kitabu cha Al-Qiyaasi fil Ibadati, uk. 308.
([24]) Angalia kitabu cha Takhriiji Al-Furuui ala Al-Wusuuli cha Zaijany, uk. 111.
([25]) Imepitishwa na Maimamu wa Hadithi: Imapokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha “Zaka” mlango wa “Kuchukuwa zaka kutoka kwa matajiri na kupelekwa kwa masikini” Hadithi nambari 1425, na imepokewa na Imamu Muslim katika kitabu cha “Imani” mlango wa “Kuhitajika shahada mbili na Sharia za Uislamu” Hadithi nambari 19.
([26]) Angalia: Kitabu cha Takhriiji Al-Furuui ala Al-Wusuuli cha Zanjaji, uk. 110: 111, na kitabu cha Al-Qiyaasi fil Ibadati, uk. 368.
([27]) Kitabu cha Al-Muwafaqaati cha Shatiby, 2/236.
([28]) Kitabu cha Nihayatul-Muhtaaji, 1/481, na kitabu cha Hawashi Sharwany wal Ibady, 1/186, na Al-Baijury ala Al-Khatibu, 1/407 – 408, 13/119.
([29]) Kitabu cha Ihkaami Al-Ahkaami sherehe ya kitabu cha Umdatu Al-Ahkaami cha Ibn Daqiqu Al-Abdu Shaafi, 1/29, na kitabu cha Tarh Tathriibu cha Waliyudeen Al-Iraqy Al-Shaafi 2/134, na kitabu cha Bahru Raiq cha Ibn Najiimu Al-Hanafi, uk. 488: 489.
([30]) Kitabu cha Raddul-Al-Mukhtaar cha Ibn Aabideen, 1/482 – 483.
([31]) Kitabu cha Al-Bahru Al-Muhit, cha Zarkashy, 7/90.
([32]) Kitabu cha Hashiyatu Ibn Aabideen, 1/301, na kamusi elizo ya kifiqhi chapa ya Kuweit, 12/208.
([33]) Al-Bahrul-Muhit, 6/389.
([34]) Kitabu cha Al-Jamal alaa Al-Manhaji, 5/403.
([35]) Kitabu cha Al-Jaml alaa sherehi Al-Minhaji, 1/543: 544.
([36]) Angalia kitabu cha: Nibrasi Al-Ukuuli, cha Sheikh Isa Manuun, uk. 139.
([37]) Kitabu cha Usuuli Sarkhassy, 2/179.
([38]) Kitabu cha Usuuli Sarkhassy, 2/142.
([39]) Kitabu cha Al-Ibhaaji sherehe ya Al-Minhaaji, 2/299 – 300.
([40]) Kitabu cha Al-Bahrul-Muhit, 6/381 – 388.
([41]) Kitabu cha Ihkaami cha Aamidy, 4/272.
([42]) Kitabu cha sherehe ya Al-Kaukabu Al-Miniir, 2/406.
([43]) Ibara hii imepokewa kutoka kwa Ramly kwenye sherehe ya Zaidi kitabu kinachoitwa Ghayatul-Bayani, 1/155, kama ilivyokuja kwa Ibn Taimia kwenye kitabu cha Majmuui Al-Fatawa, 6/452.
([44]) Sanaany amesema katika kitabu chake akielezea maelezo ya Ibn Dakiki Eid: “Kuabudu husemwa katika kukutana yanayoonekana sura yake, na kukutana na mengine kwa kulinganishwa, na yasiyo kuwa hayo husemwa “ya kuabudiwa” hayana njia isipokuwa ni amri ya Sharia”.
Ikiwa kusudio la kubudu “Ni kutofahamika maana sababu” na kusimama kwenye hukumu ya Kisharia iliyotajwa, pamoja na kutofahamu sababu yake maalumu – basi maana hii inapingana na msingi wa sababu na ulinganishi, hukumu inakuwa ni ya kuabudu tu haipelekei kwenye sababu, na hii huwa katika ibada na membo mengine, wala hakuna tofauti katika hilo.
Angalia kitabu cha: Ihkaami sherehe ya kitabu cha Umdatul-Ahkaami cha Ibn Dakiku Eid, pamoja na kitabu cha Sanaany kinachoitwa “Eda”, 2/157.
([45]) Angalia kitabu cha: Kashafu Al-Qinaai cha Al-Bahuty, 2/65: 66.
([46]) Angalia kitabu cha Al-Bahrul-Muhit cha Zarkashy, 7/90, na kitabu cha Al-Qiyaasi fil-Ibadati, uk. 265.
([47]) Kitabu cha Badhlu Nadhari fill Usuuli cha Al-Asmandy, uk. 623, na angalia kitabu cha: Al-Usuulu fil-Usuuli, 4/105 -109, na sherehe ya Tanwiiji ala Tawdhiihi cha Taftazany, 2/113, na sherehe ya Mwanachuoni kitabu cha Al-Mahally ala Jam’ii Al-Jawaamii, 2/135, na kitabu cha Al-Bahrul-Muhit cha Zarkashy, 7/70.
Kuwa wametafautiana katika maelezo ya Abi Hanifa, maelezo ya Al-Asmandi Al-Hanafi yameonekana kuwa yanazuia ulinganishi katika asili za ibada, na ambayo Taji Subky aliyoelezea ni kuwa Aba Hanifa anazuia katika mambo ya adhabu kafara na ruhusa na vinavyokadiriwa, kisha akasema: “Watu wamezuia katika asili za ibada” akafanya madhehebu mengine tofauti na madhehebu ya Abi Hanifa.
([48]) Angalia kitabu cha: Al-Mahsuulu cha Imamu Ar-Razy, 5/348.
([49]) Angalia kitabu cha: Al-Mahsuulu cha Imamu Ar-Razy, 5/348. Na kitabu cha Nihayatul-Suuli cha Jamali Diini Al-Isnawi, 4/36 – 38, na sherehe ya Mwanachuoni Al-Muhilly ala Jam’I Al-Jawaami, 2/245, na sherehe ya kitabu cha Al-Kawkabu Al-Miniir, 4/220.
([50]) Kitabu cha Al-Haawi cha Mawrudi, 5/92. Na kitabu cha Majimui cha An-Nawawi, 2/56.
([51]) Kitabu cha Nihayatul-Muhataji, 9/468, na kitabu cha Hashiyatul-Jamali, 10/278. Na kitabu cha Al-Bujairamy ala Al-Minhaji, 1/435.
([52]) Kitabu cha Rawdhatul-Nadhiru, 1/317.
([53]) Sunani An-Nisaai, 5/225 Hadithi nambari 2886, na tamko lake: “Hakika Mwenyezi Mungu ameruhusu kwa Mtume wake na wala hajaruhusu kwenu bali nimeruhusiwa mimi wakati wa mchana na kurudishwa leo uharamu wake kama vile uharamu wake wa jana, aliyopo amrikishie asiyekuwepo”.
([54]) Kitabu cha Al-Burhani cha Imamu Al-Haramain, 2/895 -964.
([55]) Kitabu cha Hashiyatu Sharbiny ala sherhi Jam’u Al-Jawamii, 2/135, na yaliyomo kwenye mabano ni ufafanuzi wetu.
([56]) Angalia kitabu cha Bayani Al-Mukhtasar cha Asafahani, 2/691: 692.
([57]) Mambo haya mawili ndiyo sababu ya tafauti katika masuala ya kulinganisha katika adhabu kafara na hukumu za kukadiriwa.
([58]) Kitabu cha Mizani cha Samarmandy, uk. 629.
([59]) Baadhi yao huita “uwazi wa maana ya andiko” na dalili hii huitwa pia “Makusudio ya maelezo” kwa maana ya makusudio na malengo yake, na watu wa madhehebu ya Imamu Shafi wanazingatia ni katika “Ulinganishi wa wazi”.
([60]) Angalia kitabu cha Asili cha Sarkhasy 1/241 na kitabu cha Bahri Al-Muhitwu cha Zarkashy 5/129, na kitabu cha Taqriir wa Tahybiir cha Ibn Amir Haj 1/109 – 110, ufafanuzi wa Mwanachuoni Al-Muhilly kwenye kitabu cha Jam’ii Al-Jawaamii 2/244 – 245, na kitabu cha Sherhu Al-Kawkabi Al-Muniir 3/486, na kitabu cha Manaahiji Al-Usuuliyyin cha Dkt. Khalifa Babakri Al-Hassan, uk. 175, na kitabu cha Usuulul-Fiqhi cha Dkt. Muhammad Mustafa Shalaby 1/483, na kitabu cha Usuulul-Fiqhi Al-Islaami cha Dkt. Wahabatu Zuhaily 1/353 – 355.
[61] Kitabu cha Al-Inayaa sherehe ya kitabu cha Al-Hidaya 1/91- 93.
([62]) Imekupitishwa na Maimamu wa Hadithi: Imepokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha “Tayammum” mlango wa “Attayyamum dharbah, hadithi nambari 340. Na imepokewa na Imamu Muslim katika kitabu cha “Al-Haidh” mlango wa “Attayamum. Hadithi nambari 368.
([63]) Angalia kitabu cha Al-Bahru Al-Muhitw cha Zarkashy 5/129, na kitabu cha Taqriir wa Tahbiir cha Ibn Amir Haji 1/109 – 110, na sherehe ya Mwanachuoni Al-Mahilly ya kitabu cha Jam’u Al-Jawaamii 2/244 – 245, na kitabu cha Sherhu Al-Kawkabi Al-Muniir 3/486, na kitabu cha Manaahiji Al-Usuuliyyin cha Dkt. Khalifa Babakri Al-Hassan, uk. 175, na kitabu cha Usuulul-Fiqhi cha Dkt. Muhammad Mustafa Shalaby 1/483, na kitabu cha Usuulul-Fiqhi Al-Islaami cha Dkt. Wahabatu Zuhaily 1/353 – 355,
([64]) Kitabu cha Badhlu An-Nadhri cha Al-Asmandy, uk. 623.
([65]) Angalia kitabu cha Nibraasul-Ukuuuli cha Issa Manun, uk. 40.
([66]) Angalia kitabu cha Sherehe ya Mwanachuoni Al-Muhilly cha Jam’u Al-Jawaamii 2/245, na kitabu cha Ruhusa ya Kisharia na kuthibiti kwake kwenye ulinganishi cha Dkt. Abdulkarim An-Nimla, uk. 185, na yanayofanyiwa ulinganishi kitabu cha Muhammad Nassar Al-Hurriyyaty, uk. 173 na kuendelea.
([67]) Rejea kitabu cha Al-Burhan cha Imamu Al-Haramaini 2/911.
([68]) Kitabu cha Al-Inswaaf cha Mardawy 1/48.
([69]) Angalia kitabu cha: Fathul-Qadiir cha Ibn Al-HImam 1/215, na kitabu cha Mawaahibi Al-Jalil cha Al-Khatwabi Al-Maalikiy 1/286, na kitabu cha Nihaayatul Muhtaji cha Arramly 1/143 – 148, pamoja na kitabu cha Kasshaful-Qinaai cha Al-Bahwaty 1/68 – 69.
([70]) Angalia kitabu: Al-Muhilly cha Ibn Hazmi1/109 – 111.
([71]) Kitabu cha Al-Insaafu cha Mardawy 1/161.
([72]) Angalia kitabu: Raddu Al-Muhtaar alaa Addurr Al-Mukhtaar, cha Ibn Aabideen 1/272.
([73]) Angalia kitabu cha:Hashiyatu Al-Adawiy sherehe ya Kifaayatul-Twaalibu Arrabbany 1/195.
([74]) Angalia kitabu: Kashaf Al-Qinaai cha Al-Bahuuty 1/119.
([75]) Angalia kitabu: Sahihi Al-Bukhary katika kitabu cha “Udhu” mlango wa “Kufuta juu ya khofu mbili” Hadithi nambari 202.
([76]) Angalia kitabu cha Sahihi ya Imamu Muslim katika kitabu chake cha “Twahara” mlango wa “Kufuta juu ya khofu na kilemba” Hadithi nambari 274.
([77]) Angalia kitabu: Al-Mughny cha Ibn Qudama Al-Maqdasy 1/184 – 185.
([78]) Kitabu cha Twarhu Tathriib 1/456 – 457.
([79]) Kitabu cha Al-Insaafi cha Mardawi 2/345.
([80]) Kitabu cha Thamru dhaaty sherehe ya Risala ya Ibn Aby Zayd Qairawany 1/266.
([81]) Kitabu cha Al-Haawi cha Al-Maawurdi 1/377.
([82]) Kitabu cha Al-Inaayah sherehe ya kitabu cha Al-Hidaya 1/91 – 93.
([83]) Kitabu cha Al-Jamalu sherehe ya kitabu cha Al-Minhaji 1/543 – 544.
([84]) Rejea kitabu cha: Burhani cha Imamu Al-Haramaini 2/960 – 964.
([85]) Angalia kitabu cha: Nihayatu Al-Suul, cha Jamalideen Al-Isnawi 4/36 – 38. Na sherehe ya kitabu cha Al-Kaukabu Al-Muniir 4/ 220.
([86]) Angalia kitabu cha Hashiyatu Al-Adawi ya sherehe ya kitabu cha Kifayatul Twaalibi 1/346, na kitabu cha Al-Muhtaaji cha Muhammad Ibn Shihabudeen Arramly 1/469 – 470.
([87]) Sherehe ya kitabu cha Muntaha Al-Iraadati 1/288.
([88]) Imepokewa na Imamu Bukhari katika kitabu cha “Kushikamana na Qurani na Sunna” mlango wa “Kufuata Sunna za Mtume wa Mwenyezi Mungu S.A.W.” Hadithi nambari 6858. Na imepokewa na Imamu Muslim katika kitabu cha “Mambo bora” mlango wa “Kukubali kwake Mtume S.A.W.” Hadithi nambari 1337.
([89]) Angalia kitabu cha: Badaai Swanaaii cha Al-Kasany 1/107.
([90]) Angalia kitabu cha: Fathu Al-Qadiir cha Al-Himami 2/5.
([91]) Kwa maada ya mbadala,
([92]) Angalia kitabu cha: Badaai Swaanaii cha Al-Kasaany 1- 107 – 108, na kitabu cha Fathul-Qadiir cha Ibn Al-Hamaam 2/5.
([93]) Angalia kitabu cha: Al-khilaafu lafdhi cha Dkt. Abdulkareem An-Nimla 2/184 – 185.
([94]) Kitabu cha Majmaa Al-Anhaar 1/239.
([95]) Angalia kitabu cha: Raddul-Muhtaar alaa Al-Darri Al-Mukhtaar cha Ibn Aabideen 2/318, na kitabu cha Fathul-Qadiir cha Ibn Al-Himam 2/233. Na kitabu cha Fiqhi Zakaat cha Dkt. Al-Qardhawi 1/438.
([96]) Angalia kitabu cha: Sherhul-Kifayatu Twaalibi cha Rabbany – pamoja na kitabu cha Hashiyatul-Adwaa – 1/490, na kitabu cha Nihaayatul-Muhtaaji, cha Ramli 3/96.
([97]) Kitabu cha Al-Majmuu cha Imamu An-Nawawi 6/39.
([98]) Angalia kitabu cha: Kashaf Al-Qinaai cha Al-Bahuuty 2/222 – 223, na kitabu cha Al-Mughny cha Ibn Qudama 2/330.
([99]) Angalia kitabu cha Al-Mughny cha Ibn Qudama 2’330 – 331.
([100]) Angalia kitabu cha: Al-Majmuui cha An-Nawawi 6/95. Na kitabu cha Fiqhi Zakaatu cha Dkt. Yusuf Al-Qardhawi 1/28 – 29.
([101]) Imepokewa na Imamu Muslim katika Sahihi yake, mlango wa kubatilika kuuza kabla ya kumiliki, Hadithi nambari 3925, na nambari 3919, na nambari 3921.
([102]) Angalia kitabu cha: Al-Majmuui cha An-Nawawi 6/95, na kitabu cha Fiqhi Zaatu cha Dkt. Yusuf Al-Qardhawi 1/28 – 29.
([103]) Al-Muhilly alaa Jam’ii Al-Jawaamii 2/135.
([104]) Al-Muhally alaa Jam’I Al-Jawaamii 2/135
([105]) Kitabu cha Kashfu Al-Mukhadarati cha Al-Baaly Al-Hambaly 1/447.
([106]) Kitabu cha Al-Iqnaai cha Al-Khatibu Sharbiiny 2’232, Al-Jamal alaa sherhi Al-Minhaji 10/353.
([107]) Angalia kitabu cha: Husnul- Maqswad fii amalil-maulidi cha imamu Suyuutwi, uk. 51, 53, 56, 63, 64.
([108]) Imepokewa na Imamu Bukhari 1193. Na Imamu Muslim 1399.