Hukumu ya kuzuia bidhaa na kupotosha wauzaji katika bei zake na kujipatia faida za binafsi kwa kutegemea hali za kiuchumi
Question
Ni ipi hukumu ya wafanyabiashara wanaozizuia bidhaa kwa manufaa yao wenyewe?
Answer
Wafanyabiashara wanaozizuia bidhaa zisiuzwe kwa lengo la kupandisha bei yake au wanaoziuza bidhaa kwa bei zaidi kuliko bei ya kawaida wakinufaika na hali ya kiuchumi na kutotulia kwa soko ni wakosaji kisharia, na wateja / wanunuzi wanatakiwa kutowasidia kufanya hivyo, basi wasinunue bidhaa isipokuwa kwa kadri wanavyohitaji tu, yaani wasinunue kiasi kikubwa zaidi ya mahitaji yao.