Hukumu juu ya msemo: "Chochote kinachohitajika nyumbani ni haramu kwenda msikitini"
Question
Ni ipi hukumu ya msemo: “Chochote kinachohitajika nyumbani ni haramu kwenda msikitini”?
Answer
Msemo uliotajwa hapo juu ni methali ya kawaida kwenye ndimi za Wamisri inayoelezea maadili ya kitamaduni yanayotafsiriwa katika maagizo ya kisharia ambayo yanamlazimu Muislamu kupanga vipaumbele vyake kulingana na mahitaji ya hekima. Kwa dhahiri inaashiria kuwa hakuna sadaka isipokuwa baada ya kujitosheleza, maana yake ni kwamba kujenga mtu kunatangulizwa kuliko kujenga majengo, na kwamba mtu anatakiwa atoe sadaka katika mambo mbalimbali ya hisani, kuanzia katika kujenga upya misikiti na kuwajali masikini, hadi mambo mengine ya wema, kila mmoja kwa kadiri ya hali yake na uwezo wake wa kifedha, na ni lazima aanze na yeye mwenyewe kisha anaowalisha kwanza, na ikiwa anacho chochote baada ya hapo; Ni bora kwake kuzitumia katika fedha hizi kwa kiasi na wastani katika kutoa.