Hukumu ya kusujudu kwa kusoma Qur`ani bila ya kutawadha
Question
Ni ipi hukumu ya sijda ya kisomo bila ya kutawadha?
Answer
Kusujudu kwa kusoma katika sehemu maalumu katika Qur’ani Tukufu ni Sunna iliyothibitishwa kwa mujibu wa Wanachuoni wa Fiqhi wengi kuanzia kwa Imamu Maliki, Shafi na Hanbali kwa mwenye kusoma na mwenye kusikiliza. Atakayeifanya atalipwa na mwenye kuiacha hatapata dhambi na sharti kwake kuwa Twahara kutokana na Hadathi kubwa na Hadathi ndogo, kwa mujibu wa makubaliano ya Wanachuoni wa Fiqhi walio wengi kuanzia kwa Imamu Hanafi, Maliki, Shafi na Hanbali. Kwa sababu ni Swala au kwa maana ya Swala, na Swala haiwi sahihi bila ya Twahara. Imepokelewa kutoka kwa Abdullah Ibn Omar, (R.A), alisema: “Mtu hasujudu isipokuwa ametwaharika.” Hadithi hii imejumuishwa na Imamu Malik katika “Al-Muwatta’”, na Al-Hafidh Ibn Hajar ameitaja katika “Fath Al-Bari” (2/554) na akasema: “Mlolongo wake wa upokezi ni sahihi.”
Kuna nafasi ya kumtaja Mwenyezi Mungu kwa asiyesujudu kwa udhuru, hata kama ametwaharika. Kama kusema: Mwenyezi Mungu ametakasika, sifa njema ni za Mwenyezi Mungu, hapana mungu ila Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu ni Mkubwa (asema hiyo mara nne).