Msimamo wa watu wema waliotangulia ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Msimamo wa watu wema waliotangulia kwa Alkhawariji

Question

Ni upi  msimamo wa watu wema waliotangulia kwa  Alkhawariji

Answer

Watu wema waliotangulia  – wakiongozwa na Maswahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) walishughulika na Alkhawariji kwa uthabiti wote tangu kudhihiri  kwao kama madhehebu ya Kiislamu katika zama za Imam Ali bin Abi Twalib, Mwenyezi Mungu amuwiye radhi, mwanzoni mwa jambo,alimtuma bwana wetu Abdullah bin Al-Abbas, kuwaonesha. upotofu wao na kujibu matatizo yao ya kifikra yaliyowafikisha hapo walipofikia, wengi wao wakarejea kutoka katika mawazo hayo yasiyo ya kawaida. Na waliobaki wakasisitiza kuendelea na msimamo wao, hivyo Imam Ali akashughulika nao kwa makali ya upanga kwa sababu ni mtawala halali na mlezi wa taifa la Kiislamu wakati huo, na katika utekelezaji wa wasia wa Mtume (S.A.W.) pale aliposema: “Hao ni wabaya wa viumbaji wote, heri kwa mwenye kuwapiga na kuwaua, wanakilingania Kitabu cha Mwenyezi Mungu na hawana chochote katika hayo, anayepigana nao ana haki zaidi kwa Mwenyezi Mungu kuliko wao...”

Share this:

Related Fatwas