Ukumbusho wa siku ya arobaini na kila mwaka kwa aliyefariki
Question
Nini hukumu ya ukumbusho unaofanywa siku ya arobaini na kila mwaka kwa aliyefariki?
Answer
Wanachuoni wa Fiqhi walio wengi wanaona kuwa muda wa kutoa rambirambi ni siku tatu tu, na baada ya hayo haipendezi, isipokuwa kwa wale ambao hawakuwepo kisha wakahudhuria, au kwa wale ambao hawakujua juu ya kifo hicho isipokuwa baada ya muda huo kupita. Kwa sababu (kuendelea kutoa rambirambi) kuna ndani yake kurejesha huzuni, na kuwapa familia ya mfu wasichoweza kustahimili.
Hakuna pingamizi la kisharia kukusanyika kwa watu ili kumpa marehemu thawabu ya jambo jema. kama vile kulisha chakula, na kusoma Qur’ani; iwe katika siku ya arobaini au katika kila mwaka.