Uhusiano wa kundi la kigaidi la Ikh...

Egypt's Dar Al-Ifta

Uhusiano wa kundi la kigaidi la Ikhwanul Muslimin, na vikundi vya msimamo mkali na madhehebu ya kisasa ya Makhariji.

Question

Kwa nini kundi la Ikhwanul Muslimin ni mama wa vikundi vikali na mama wa madhehebu ya kisasa ya Alkhawariji?

Answer

Kiakili, fikra za Hassan Al-Banna ambaye ni muasisi, na mwandishi  mwananadharia Sayyid Qutb ambayo yalitolewa na Al-Banna na Mawdudi ni miongoni mwa mambo yanayochochea makundi ya kigaidi Mashariki na Magharibi, hususan vitabu viwili: (Maalim Fi Attariq) na (Fii Dhilal Al-Qur'an) Hasan Al-Banna na Sayyid Qutb ni miongoni mwa mababa wa kiroho wa makundi haya katika historia ya kisasa.

Ama kwa upande wa kihistoria, jinai la kundi la Ikhwan la kigaidi lilikuwa ni jinai la kwanza la kigaidi katika zama hizi. Katika miaka ya arubaini ya karne iliyopita, waliwauwa Mawaziri Wakuu wawili na mshauri katika mahakama! Katika miaka ya hamsini, walijaribu kumuua marehemu Rais wa Jamhuri, Gamal Abdel Nasser, na walikaribia kufanikiwa katika hilo, na wana uhusiano mkubwa na mauaji ya hayati Rais Muhammad Anwar As-Sadat..

Imebainika kuwa wengi wa waanzilishi na wanachama wa makundi ya kigaidi walikuwa na uhusiano mkubwa na kundi la Ikhwanul Muslimin, kwa mfano: Shukri Mustafa, muasisi wa kundi la Takfir Wal-Hijrah, alikuwa mkwe wa mmoja wa wanachama wa kundi hilo. na alikamatwa mwaka 1965 BK. pamoja na wanachama waliokamatwa miongoni mwa wanachama wa kundi la Ikhwanul Muslimin, kabla ya kuanzisha kundi lake mwenyewe.

Share this:

Related Fatwas