Kukusanya funga kati ya nia ya kulipa na funga ya siku sita za mfungo mosi.
Question
Ipi hukumu ya kukusanya funga kati ya nia ya kulipa na funga ya sita ya mfungo mosi?
Answer
Inafaa kwa Muislamu kunuia nia ya funga ya Sunna pamoja na nia ya funga ya lazima au ya faradhi, atalipa siku zilizompita za funga ya Ramadhani ndani ya mwezi wa mfungo mosi na inatosha kwa kila siku anayolipia kufunga siku ya funga ya sita ya mfungo mosi, na kwa kufanya hivyo anapata malipo ya aina mbili, ukamilifu zaidi na kilichobora ni kufunga kila funga peke yake.