Makundi ya kigaidi na dhana ya Tagh...

Egypt's Dar Al-Ifta

Makundi ya kigaidi na dhana ya Taghuti (Shetani)

Question

Kwa kiasi gani makundi ya kigaidi yalibadilisha matumizi ya dhana ya Taghuti (Shetani)?

Answer

Kwa hakika makundi ya kigaidi yalibadilisha matumizi ya neno "Taghuti" (Shetani) kinyume cha maana yake ya asili, wakalitumia kuashiria watawala na mataifa, kwa madai ya kwamba watawala hawafuati Sheria za Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa madai yao potofu, nao mataifa wanakubali hilo bila ya kupinga hata kidogo, lakini ukweli ni kanuni za Sheria ya Kimisri hutokana na hukumu za sheria ya kiislamu, vile vile katiba ya Kimisri imepitisha katika mada No. 2 kuwa Sheria ya Kiislamu ndiyo chanzo kikuu cha Sheria, na kwamba dini ya Uislamu ndio dini rasmi ya nchi, Kiarabu ndiyo lugha yake rasmi , kwa upande wa Qur`ani Takatifu, neno la Taghuti limetajwa katika Aya nyingi kama vile kauli yake Mwenyezi Mungu (S.W.): {Huwaoni wale wanao dai kwamba wameamini yaleyaliyo teremshwa kwako na yaliyo teremshwa kabla yako? Wanataka wakahukumiwe kwa njia ya upotofu} [An-Nisaa: 60] neno lenyewe linaweza kutumika kwa maana kadhaa na kutumika kwa kuashiria mmoja na wengi, wa kiume na wa kike, naye Imamu Al-Maturidy alisema kuwa "Taghuti" (Shetani) ni kila linaloabudiwa mbali na Mwenyezi Mungu, na kwamba Aya hii imeteremshwa kwa kuashiria baadhi ya wanafiki waliokuja kwa Mtume (S.A.W.) kwa kuomba hukumu yake kuhusu masuala kadha wa kadha, na alipotoa hukumu ya haki wakaikataa hukumu ile kwa kuwa ilipinga matamanio yao.

Share this:

Related Fatwas