Idadi ya rakaa za Sunna na nyakati ...

Egypt's Dar Al-Ifta

Idadi ya rakaa za Sunna na nyakati zake

Question

Rakaa ngapi za Swala ya Sunna na nyakati zake?

Answer

Swala inayoswaliwa kabla au baada ya Swala tano za Faradhi ima ni Sunna inayosisitizwa, nayo ni aliyoifanya Mtume (S.A.W) mara kwa mara, nayo ndiyo iliyotajwa katika Hadithi tukufu. : “Mwenye kung’ang’ania kuswali rakaa kumi na mbili mchana na usiku ataingia Peponi; Rakaa nne kabla ya adhuhuri na rakaa mbili baada yake, rakaa mbili baada ya Swala ya Magharibi, rakaa mbili baada ya Swala ya Isha, na rakaa mbili kabla ya alfajiri.” Imepokelewa kutoka kwa An-Nasaai

Au ni Sunna zisizosisitizwa ambazo zimependekezwa kufanywa bila ya usisitizo, nazo ni rakaa mbili kabla ya Swala ya alasiri, rakaa mbili kabla ya Swala ya Magharibi, na rakaa mbili kabla ya Swala ya Isha, kwa kuzingatia Hadithi iliyopokelewa kutoka kwa kundi kutoka katika Hadithi ya Abdullah Ibn Mughaffal (R.A): kwamba Mtume (S.A.W) amesema: “Kati ya kila Adhana na Iqaamah, kuna Swala, Kati ya kila Adhana na Iqaamah, kuna Swala, kisha akasema katika mara ya tatu: “Kwa amtakaye.” Ili watu wasiichukulie kama Sunna. Sunna hizi zinaitwa Swala ya suna ya hiari (isiyo sisitizwa) na ya kujitolea.

Share this:

Related Fatwas