Kuunda makundi yanayopinga mfumo wa kijumla yanayochochea kuasi nchi
Question
Je, inaruhusiwa kuunda makundi yanayopinga mfumo wa kijumla yanayochochea kuasi nchi?
Answer
Haijuzu kuunda makundi yanayopinga mfumo wa kijumla yanayochochea kuasi nchi, hayo ndiyo misingi ya Uislamu kwa kile kinachohusika na vitendo vya kutisha watu na kuharibu nchi, kutia wasi wasi na hofu nyoyoni, kueneza chuki na migongano kati ya watu, kupoteza amani na utulivu katika jamii, hivyo kupoteza makusudio makuu ya sheria ambayo Mtume (S.A.W.) alitumwa kwa ajili ya kuyahakikisha, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: {Kama wanafiki na wale wenye maradhi nyoyoni mwao, na waenezao fitna katika Madina hawatoacha, basi kwa yakini tutakusalitisha juu yao, kisha hawatakaa humo karibu yako ila muda mchache tu* Wamelaanika! Popote watakapo onekana watakamatwa na watauliwa kabisa} [Al-Ahzaab: 60 - 61]. Kwa hakika nchi ndiyo jumuiya ya kikweli kwa mujibu wa istilahi iliyoelezwa katika Sunna za Mtume, kwa hiyo kuunda makundi mengine yanayoipinga nchi na kueneza fitina humo ndani ni uhalifu, Mtume (S.A.W.) amesema: "…kwa Yakini Mwenyezi Mungu huwa na walio wengi pamoja, hali ya kuwa anayejitenga huwa anajikurubisha kwenye moto" [Imesimuliwa na Tirmidhy], kwa hiyo, wanachi wanapaswa kushirikiana katika kufanya mema na ucha Mungu, kukataa maovu na uadui, kutomshawishi mmoja ajitenge na utiifu, kutoshawashika na madai matupu yanayoenezwa na waovu.