Zabuni.
Question
Ipi hukumu ya kushikiri katika zabuni za serikali au binafsi, na kulipia gharama kwa ajili hiyo?
Answer
Zabuni ni makubaliano halali Kisharia, mfano wake ni kama mnada ambapo hutekelezwa hukumu zake, hakuna kizuizi Kisharia kulipia gharama za kuingia kwenye zabuni kwa kiwango kisichozidi thamani yake halisi.
Zabuni ni moja ya njia inayofahamika katika kupitisha mikataba ya kiidara ambayo hufanywa na taasisi za kiserikali na sekta binafsi, kama vile mikataba na makubaliano ya manunuzi au ukandarasi, yenyewe ni katika mambo ya kisasa katika mfumo wa miamala ya kifedha, hufuatwa kwa mwenye kutaka kupata bidhaa, au huduma, kama vile mnada hutekelezwa hukumu zake, kisha hatua zinazofuatwa katika mikataba ya zabuni ikiwa ni pamoja na kuandikwa kuandaliwa na kusimamiwa. Masharti ya kiidara au kisheria lazima kutopingana na hukumu za Sharia za Kiislamu, hakuna kizuizi Kisharia kulipia gharama za kushiriki isiyozidi thamani yake.