Kusimama juu ya kaburi baada ya kuzika.
Question
Nini hukumu ya kusimama kwenye kaburi baada ya kuzika ili kumfanyia duwa maiti na kumuombea msamaha?
Answer
Kusimama kwenye kaburi baada ya kuzika ili kumuombea msamaha maiti na kumfanyia duwa ni katika Sunna za kufuatwa, kutoka kwa Amiri wa Waumini Othmani Ibn Affan R.A amesema: Mtume S.A.W alikuwa anapomaliza kuzika anasimama mbele ya kaburi na anasema:
“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumuombee kauli thabiti, kwani hivi sasa anaulizwa”. Imepokewa na Abu Daudi.
Imamu An-Nawawy anasema katika kitabu cha Al-Adhkaar 1/161: (Ni Sunna kubaki baada ya kumaliza kuzika angalau saa moja, na watu wakashughulishwa na kisomo cha Qur`ani na maombi kwa maiti pamoja na kupeana mawaidha na simulizi za watu wa kheri na hali za waja wema. Imamu Shaafi na watu wake wamesema: Ni Sunna kumsomea maiti sehemu ya Qur`ani, wakasema: Na kama watakamilisha Qur`ani yote basi hilo ni zuri zaidi).