Kutoa khutba kabla ya mazishi na kaburini baada ya kuzikwa
Question
Ni ipi hukumu ya kutoa khutba kabla ya swala na pia kwenye kaburi baada ya kuzikwa?
Answer
Inapendekezwa, kwa mujibu wa sharia, kutoa khutba au mawidha wakati waombolezaji wakisubiri mazishi kufika ili kuuswalia, na pia kwenye kaburi baada ya kuzikwa. Hadithi Sahihi zinasema kwa uwazi kwamba Mtume (S.A.W) alikuwa akiwahubiria maswahaba zake baada na kabla ya kuzika maiti. Kutokana na hayo ndiyo Iliyopokelewa kutoka kwa Imam Ali (R.A) katika Hadithi iliyokubaliwa, amesema: Tulikuwa mazikoni kwenye, Baqi‘ al-Gharqad. Akatujia Mtume (S.A.W) akakaa kitako, na sisi tukaketi kumzunguka, vile yeye akiwa na kijibakora. Akainama chini, na kuanza kuchimba-chimba kwa kijibakora chake. Kisha akasema:
“Hakuna yeyote hapa, wala kiumbe chochote chenye kupumua, isipokuwa na Menyezi Mungu amesajili mahali pake, iwe Peponi au Motoni, na hivyo amesajiliwa kimaandishi kuwa ni mtu muovu au mtu mwema.”
Basi mmoja akuliza kwa kusema: “Basi kwanini tusibweteke, tu, kufuata tuliyo kwisha andikiwa kuyatenda!?”
Mtume (S.A.W) akamjibu kwa kusema: “Aliyesajiliwa kuwa ni mja mwema, basi ataendelea kutenda mambo mema, na aliyesajiliwa kuwa ni mja muovu, basi ataendelea kutenda mambo maovu.” Kisha akamalizia kwa kusema: “Hivyo endeleeni kutenda; maana kila mmoja atarahisishiwa tulitendalo. Mtu mwema atarahisishiwa kutenda mema, na mtu muovu atarahisishiwa kutenda maovu.” Kisha akatusomea aya zifuatazo:
“Ama mwenye kutoa na akamcha Mwenyezi Mungu. Tutamsahilishia yawe mepesi. Na ama mwenye kufanya ubakhili, na asiwe na haja ya wenzake. Na akakanusha lilio jema, Tutamsahilishia yawe mazito.” (Al-Layl, 92:5-10)