Kumtafunia mtoto mchanga.

Egypt's Dar Al-Ifta

Kumtafunia mtoto mchanga.

Question

Nini maana ya kumtafunia mtoto mchanga, na nini hukumu yake na hufanyika namna gani?

Answer

Kumtafunia mtoto mchanga ni: Kutafuna kitu kitamu kama vile tende au asali ya nyuki na mfano wake kisha kumuwekea mtoto mchanga mdomoni na kumsugulia nacho. Wanachuoni wameelezea Sunna hii, na hilo ni kwa kufanya kwake Mtume S.A.W kutoka kwa Abi Musa Al-Ash’ary R.A amesema:

 “Nilipata mtoto na nikampeleka kwa Mtume S.A.W akampa jina la Ibrahim na akamtafunia tende”. Hii ni pamoja na kufahamu kuwa inapaswa mtu wa kufanya hivyo awe ni katika watu wenye uzoefu wa jambo hili, ili kusipelekee madhara kwa mtoto na kumuharibu huku akidhani anamuimarisha na kumtengeneza.

Share this:

Related Fatwas