Dhana mbaya.

Egypt's Dar Al-Ifta

Dhana mbaya.

Question

Mchumba wangu mara nyingi ananidhania vibaya ni namna gani niende naye kwenye hili?

Answer

Kuvuruga mahusiano kati ya wachumba kwa dhana mbaya, na kufuatilia kasoro na kuharibu kuaminiana kati yao kunapingana na hekima pamoja na maadili ya kijamii ambayo yamekusudiwa na Sharia Takatifu katika kuhalalisha uchumba.

Mwenyezi Mungu Mtukufu katika maeneo mengi ndani ya Kitabu chake amekataza waja wake Waumini kudhaniana vibaya, miongoni mwake ni kauli ya Mola Mtukufu:

{Enyi mlio amini! Jiepusheni na dhana nyingi, kwani baadhi ya dhana ni dhambi. Wala msipelelezane} Al-Hujraat: 12.

Na Imamu Ibn Kathiir katika tafasiri yake 7/377.  Mwenyezi Mungu Anasema – kwa maana ndani ya Aya hii, akiwakataza waja wake Waumini kujiepusha na dhana nyingi, nayo ni tuhuma na hiyana kwa ndugu watu wa karibu na watu wengine, kwa sababu baadhi ya hizo dhana zinakuwa ni dhambi moja kwa moja, basi na ajiepushe na kudhani kwingi kwa akiba, na imepokewa kutoka kwa Amiri wa Waumini Omar Ibn Khattab R.A amesema: Wala usidhanie neno lilotoka kwa ndugu yako Muislamu isipokuwa kwa dhana njema, nalo utalikuta ni lenye kubeba kheri.

Share this:

Related Fatwas