Hesabu ya theluthi ya usiku na nusu yake.
Question
Namna gani huhesabiwa theluthi ya usiku na nusu yake?
Answer
Hesabu ya usiku ni kuanzia kuzama kwa jua mpaka machomozo ya alfajiri, kati ya nyakati hizi mbili ndio usiku, na ili kufahamu nusu yake uhesabiwa idadi ya saa kati ya nyakati mbili na kugaiwa mara mbili, kisha huongezwa nusu kwenye wakati wa Magharibi, hupatikana wakati wa nusu ya usiku, au hugawanywa sehemu tatu kisha huongezwa theluthi kwenye wakati wa Magharibi na kupatikana wakati wa theluthi ya usiku.