Eda ya aliyefiliwa na mume wake.
Question
Ipi eda ya aliyefiliwa na mume wake? Na je inafaa kwake kutoka kipindi cha eda?
Answer
Eda ya kufiliwa na mume ni miezi minne na siku kumi kwa miezi ya Kiislamu, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:
{Na wale miongoni mwenu wanao kufa na wakaacha wake, hawa wake wangoje peke yao miezi mine na siku kumi} Al-Baqarah: 234.
Inafaa kwake kutoka kwa siku moja nyumbani kwa marehemu mume wake, pamoja na kuchunga kulala kwake alale nyumbani kwa marehemu mume wake kipindi chote cha eda.
Mwenyezi Mungu Anajua zaidi.